Asante binamu yangu kwa kushukuru mkwepu jr apewe maua yake tuduh, kumbe ndiyo iko hivi. Inaweza kuwa imetafsiriwa kutoka anga za Kanada na Marikani wanakowaita 'aliens'.
Kwa hiyo Lee ni ajinabi hapa Bongo.
Makiwendo you are missed big time. Bado naendelea kuuliza kama TCRA wanawea kunipatia namba yako ya simu
Shunie mara zaote asante kwa magazeti na Je wajua
mkwepu jr popote ulipo kula chuma hicho, kivumbi leo , like-d the like
makaveli10 mdau veterani huna baya na mtu nakusalimia mwanaSimba
Makapuku, sehemu nzuri kabisa kuwepo sababu wewe upo
Ameen ufike salamaMungu Baba bariki safari yng DOM - DAR, Bariki chombo hii ya Shabiby ifike salama. Amen
Ameen ufike salama
BAADHI ya wachezaji wa Wigan wenye hasira wamepanga kufanya maandamano na waligoma kucheza mechi yao mwisho ya Ligi daraja la Kwanza dhidi ya Rotherham.
Wachezaji wa kikosi hicho cha Wigan waligoma kufanya mazoezi wikiendi iliyopita ikidaiwa kwamba mmiliki wao ameshindwa kuwapa mishahara yao yote.
Imeelezwa kuna Wachezaji ambao wamechelewa kulipwa mishahara yao, lakini wale ambao mkataba wao inamalizika mwisho wa msimu hawajalipwa mishahara yao.
Ingawa mishahara hiyo imechelewa kuingia kabla ya mechi yao dhidi ya Millers, wachezaji wa Wigan wangegoma kucheza mechi ya mwisho ya msimu huku Ligi daraja la Kwanza.
Mwenyekiti wa Wigan, Talal Al Hammad aliweka wazi mishahara haitawekwa hadi mechi itakapochezwa jambo ambalo limepingwa vikali na wachezaji wao.
View attachment 2616232
Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kati ya Baobab Queens dhidi ya Simba Queens umemalizika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo Mei 9, kwa wenyeji kupokea kichapo cha mabao 2-0.
Licha ya Simba Queens kuibuka na ushindi huo inasikilizia michezo ya JKT Queens na Fountain Gate Princess kuweza kujua hatma ya ubingwa.
Baada ya ushindi huo, Simba Queens inaongoza ikiwa na pointi 42 ikifuatiwa na JKT Queens yenye alama 40 na Fountain inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 38.
Simba Queens imecheza michezo 17 huku JKT Queens na Fountain zikiwa zimecheza michezo 16.
Mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya Fountain Gate Princess dhidi ya JKT Queens unaotarajiwa kupigwa keshokutwa (Alhamisi Mei 11) katika uwanja wa Jamhuri.
View attachment 2616233
Kinda wa Real Madrid, Rodrydo amezungumzia kuhusu mechi ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City huku akimhofia mshambuliaji wa timu hiyo Erling Haaland.
"Hakuna anayejua jinsi ya kumzuia Haaland, ila nina imani hatofunga dhidi yetu,"
View attachment 2616235