Farhan Jr
KUFUNGWA NI MPIRA, LAKINI SABABU NI ZAIDI YA MPIRA.
FOOTBALL ni mchezo wa wazi sana, Coach Robertinho hana cha kulaumiwa na hata wachezaji hawana cha kulaumiwa haswa wa kikosi cha kwanza, wametumika sana wengine miaka mitatu sasa na michuano zaidi ya mitatu! Matokeo yake uchovu mkubwa sana.
Kocha anatamani sana kurotate kikosi ila bench halimpi nafasi hiyo! Bench lina Moses Phiri, Sakho, Banda ambao ndio wa daraja la juu! Na hakuna wengine, Mchezaji anayekaribiana na Chama bench, hakuna anayemkaribia Kapombe bench, hakuna anayemkaribia Inonga ama Saido bench! Hakuwa na namna.
Msimu umeisha kikatili sana, msimu wa pili mfululizo bila Mataji ya ndani kuanzia Ngao, Ligi Kuu na FA! Msimu mwingine tena wa kuondoka Kapa! Maana yake ni nini? Lazima kurudi kwenye drawing board na kuanza upya kuunda timu, haikwepeki, tayari timu imefikia mwisho na haiwezi kuvuka tena nje ya hapo.
TAJIRI MO kubali sasa unapaswa kuunda upya timu kuanzia Ofisini, muundo wa timu! Mifumo ya mishahara mpaka bonus! Football imefikia eneo ambalo inahitaji sana reinforcement lakini pia kukusanya nguvu ya kweli na MAONO mapya, hakuna namna.
Zidane sababu kubwa ya kuondoka Real Madrid alisema ameshinda kila kitu na kikosi hicho hivyo haoni kama wanaweza kutumana au kuwa na nguvu ya kuvuka pengine, hivyo timu iundwe upya, sauti mpya na uelekeo mpya.
Dark day in Simba Sports club history lakini the Lion has to rise again! The Lion has to wake up! Lakini mpaka kurejea drawing board na kupata njia mpya, bado tupo kwenye project ya Magori na Senzo ambayo inaishia ishia sasa, hatujaunda kitu kipya na Barbra ndio alikuwa anaimalizia kwenye zama za mwisho.
Downfall hii ni kwakuwa glory days zimeisha na project mpya haikuandaliwa, tulikuwa timu ya Media zaidi kuliko kwa ground, tukajisahau.
Kufungwa ni Football, lakini kwanini tumefungwa!? Kwanini misimu miwili bila kikombe?? Hapo ndio swali pekee, kufungwa na Azam wala sio issue!