Sports Arena Tz
AZAM INATUPA UGUMU KUITETEA
.
Katika timu ngumu kuzitetea hapa Tanzania, nadhani Azam FC inaongoza. Kila inapoanza msimu inakupa matumaini kama itashindania vilivyo ubingwa wa ligi na mashindano mengine ambayo hushiriki.
.
Utaona inafanya usajili wa wachezaji ambao wanaonekana mahiri kwenye timu zao ambao huaminisha wengi kuwa watawasha moto vilivyo kwenye msimu husika.
.
Watafanya maandalizi kabambe ya kabla ya msimu (pre-season) nje na ndani ya nchi na yanaweza kukuaminisha kuwa Simba na Yanga zitakutana na ushindani mkali katika mbio za ubingwa.
.
Hata hivyo msimu ukishaanza Azam inageuka timu ya kukamia mechi mojamoja na nyingi ucheza pasipo kuonyesha timu kubwa ambayo inakiu na hamu ya kutwaa mataji.
.
Mfano mzuri ni msimu huu zikiwa zimebakia mechi tano tu kumalizika Azam inawania nafasi ya tatu dhidi ya Singida inayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu msimu huu. Sasa Unapata wapi nguvu za Kuitetea Azam pale watu wanapoikosoa
View attachment 2565898