Makapuku Forum

"Mpira wa Afrika kuuendesha ni changamoto kubwa hivyo ni wakati wa wadhamini kujitokeza kwa ajili ya timu hizi kutokana na kuamini soka letu ni pana sana na wenzetu waliokuwa kwenye biashara wanaliona hili," Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji.
 
Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji amesema kitendo cha kuingiza timu mbili kwenye robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kimeitangaza nchi vizuri kwa maana ya nje ya mipaka ya Afrika.

"Mafanikio haya yameihakikishia nchi yetu kupeleka timu nne Kimataifa msimu ujao lakini pia kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kununua kila bao Sh5 milioni kimeleta motisha kubwa."

 
Mwandishi Mwandamizi wa michezo wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Charles Abel amesema kitendo cha timu za Simba na Yanga kufuzu hatua za makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kuna faida kubwa kwa sababu inatoa fursa kwa wachezaji wengi wazawa kuonekana Kimataifa.

"Wachezaji wetu wanakutana na watu tofauti ambao mataifa yao yameendelea hivyo kuwaongezea ujuzi na hata pia kwa makocha wa timu hizo kwa maana wanapata mbinu mbalimbali za kiufundi," amesema Abel.
 
Mgombea urais mkuu wa upinzani nchini Nigeria ambaye katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita alishika nafasi ya pili, Atiku Abubakar amewasilisha ombi rasmi mahakamani la kutaka kubatilisha
ushindi chama tawala uliopata.

Katika maombi yake, Abubakar wa Peoples Democratic Party (PDP) anadai uchaguzi huo ulikuwa batili kwa sababu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilishindwa kuzingatia sheria ya uchaguzi kwa kutopakia matokeo.

Aliyekuwa Gavana wa Lagos na kiongozi mkuu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC), Bola Tinubu alishinda uchaguzi huo kwa takriban asilimia 37 ya kura lakini vyama vya upinzani vimedai kuwa kucheleweshwa kwa upakiaji wa matokeo kwa njia ya kielektroniki kulichangangia kuwepo kwa kiwango kikubwa cha wizi wa kura.
 
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 37 anakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Milca (48) kufariki dunia wakati wakifanya mapenzi kichakani eneo la Mbita katika Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya.

Tukio hilo limetokea jioni ya Jumapili ya Machi 19 mwaka huu baada ya wapenzi hao waliokuwa wanarejea nyumbani kuamua kuingia kwenye kichaka eneo la Got Rateng kwa ajili ya kufanya kitendo hicho walipokuwa wametoka kunywa pombe, tovuti ya TUKO imeripoti.

Chifu wa eneo hilo amesema kuwa wawili hao awali walikuwa wameonywa wasishiriki tendo wakiwa wamelewa lakini hawakutii, mshtakiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo baada ya kukiri chanzo cha kifo hicho.

 
Jumla ya mitumbwi 212 imepasuka baada ya kujibamiza kutokana na mawimbi, huku 38 ikiharibika kabisa baada ya kuibuka kwa upepo mkali ndani ya Ziwa Victoria katika mialo ya Busekela na Buira wilayani Musoma.

Tukio hilo limetokea Machi 20, 2023 saa 11 jioni wakati wavuvi wakijiandaa kuingia ziwani kwa ajili ya kufanya shughuli zao kama ilivyo kawaida.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi, Diwani wa Kata ya Bukumi yalipotokea maafa hayo, Munubi Musa amesema kuwa mbali na mitumbwi hiyo. Pia nyavu zinazotumiwa na wavuvi hao pia zimeharibiwa.
 
Farhan Jr

Clatous Chama mchezaji ambaye ni mvivu, hakabi, anapoozesha timu na Kocha Robertinho anapaswa kumtupa bench ameibuka tena kinara wiki hii baada ya kubeba bao bora pamoja na kuingia kikosi bora cha wiki huku sasa akipambania nafasi ya Mchezaji bora wa wiki kwenye KLABU BINGWA AFRIKA.

Ikumbukwe kuwa Mchezaji huyo mvivu na hafai kwenye soka la kisasa aliingia kikosi bora wiki mbili nyuma na alikuwa Mchezaji bora wa wiki pia, akitwaa na sasa itakuwa mara mbili mfululizo kwenye michuano hiyo.

Mchezaji huyo mvivu ana takwimu kali zaidi ligi ya ndani na sasa kimataifa, Watalaam wa mambo wanadai hiki anachokifanya kwenye hizi nafasi hakuna Mchezaji amewahi kufanya, ni namna nzuri sana ya Mchezaji anayepoozesha mpira kuonesha uwezo wake.

Neno moja kwa Mchezaji mvivu na asiyefaa kwenye soka la kisasa akiwa tu anatamba kwenye mechi dhidi ya Dar City pekee

 
Farhan Jr

Mchezaji mvivu zaidi kwenye kikosi cha Simba ana mabao 15 kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, yupo kwenye orodha ya Wafungaji bora 10 wa muda wote barani Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa.

Mvivu Clatous Chama ambaye hakabi anafungana mabao na nyota Yannick N’Jeng ambaye ni straika.

Kwenye orodha hiyo ya wafungaji 10 bora Afrika kuna Viungo Washambuliaji wawili tu ambao ni Mohamed Aboutreika na Mvivu Clatous Chama.

Sisi ambao tunamkubali Kiungo huyu mvivu tunasema ni yeye tu na Mbwana Samatta ambao wamecheza Tanzania wapo kwenye orodha hiyo!

Tukisema ni Mchezaji bora wa muda wote kwanini hamtaki?

Basi na uvivu uendelee

 
Farhan Jr

A message to the future! Mnaitazama hii picha leo March 20, 2509 najua kizazi chetu hakikuacha picha nyingi za maana, mabango ya Ujugu hayana maana, hatujaacha vitu vingi sana zaidi ya stori za Mashalove na Mfalme Zumaridi, hatujaacha urithi wa kutisha zaidi ya Harmorapa na Kikombe cha Babu.

Licha ya uzuri wetu wa mkakasi ila ndani kipande cha mti! A message to the future sahauni kuhusu stori mtakazoziona Youtube kuhusu Fair Competition au Kocha Adel kuwaacha wakina Zimbwe, tunajua hatuna vingi vya maana ila kuna hazina tumewaachia.

Nani mwenye hekima na busara kati yenu mtachaguana! Nani anajua kubadili picha kuwa maneno kama The Great Lufufu Mkandala au Juma Khan? Basi mtumeni mpaka Ghorofa ya 10 pembezoni mwa Bahari ya Hindi, kuna urithi wenu tumewaachia.

Atakayefunga safari kwenda Posta mwambieni asigeuke nyuma kwakuwa atapishana na wadada wenye shape kali akatengua udhu yake, mwambieni picha ya upako wa vizazi na vizazi ikafuatwe ile picha irejeshwe Makumbusho pale Jangwani, avae kanzu asiwe na tamaa! Mezani ataikuta.

Urithi pekee wa maana katikati ya penzi la Whozhu na Sepetu Wema, katikati ya hekaya za Kaka Vunjabei na Hamisa, Manara na Rushayna basi sie tumewaachia kumbukumbu bora katika picha, itunzeni sana! 25 ni Kennedy Musonda na 9 ni Fiston Mayele.

A message to the future msiipoteze hiyo picha! Itunzeni vizazi na vizazi! Ina maana kubwa sana kwa Yanga na harakati zao kwenye soka la Afrika.

Wenu Mtiifu, Babu Farhan Kihamu aliyepumzika kwenye makaburi ya Ifakara, Kilombero, Morogoro
Itunzeni hiyo picha
 
TOP 10: WAFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE LIGI YA MABINGWA AFRIKA
.
1. Tresor Mputu — 39
2. Mohamed Aboutrikq — 31
3. Mahmud El Khatib — 28
4. Flavio Amado — 27
5. Emad Moteab — 24
6. Ali Zitouni — 23
7. Mbwana Samatta — 21
8. Dioko Kaluyituka — 20
9. Gamal Abdel-Hamid — 20
10 CLATOUS CHAMA — 19
 
MAYELE AOMBA KUBAKI CONGO
.
Straika wa Yanga, Fiston Mayele ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya DR Congo
kinachojiandaa na mechi za kufuzu Afcon dhidi ya Mauritania Ijumaa hii, amesema hatarudi tena Tanzania ataungana na Yanga huko huko.
.
DR Congo mara baada ya mchezo wao wa kwanza kukamilika Ijumaa hii watakuwa na kibarua kingine Machi 28 mchezo wa marudiano ugenini na baada ya hapo atawasubiri Yanga wanaokwenda kuvaana na TP Mazembe.
.
Mayele amesema ameshawasiliana na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kuwasilisha ombi hilo hivyo hataweza kujiunga na wenzake mara baada ya kulitumikia taifa lake na atabaki kuwasubiri Yanga tayari kuwavaa TP Mazembe Aprili 2.
 
NYOTA WAWILI SIMBA KUIKOSA RAJA
.
Mohammed Hussein ‘Zimbwe’ na Kibu Denis watakosa mechi ya mwisho ya Simba ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ugenini baada ya kutimiza kadi ya pili ya njano kwa kila mmoja kwenye mechi ya Jumamosi waliyoibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…