Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kwenye orodha ya habari muhimu za wiki na hii imo ambapo Kundi la kwanza lenye Wafanyakazi 18 wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps limerejea Tanzania baada ya kutokuwepo kwa takriban miaka mitatu toka kuzuka kwa corona March 2020 kulikowalazimisha kurejeshwa Marekani zaidi ya Wafanyakazi hawa 7,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani wakiwemo 158 wa Tanzania.

Baada ya mafunzo ya wiki 11 yatakayojumuisha lugha ya Kiswahili, utamaduni wa Kitanzania na ujuzi mahsusi wa kiufundi kulingana na sekta zao, Wakufunzi hawa wataapishwa kuwa Wafanyakazi wa Kujitolea ili kuanza miezi yao 24 ya utoaji huduma ambapo kulingana na maombi ya Serikali ya Tanzania, Wafanyakazi hawa wataelekezwa katika sekta ya elimu watakapofundisha Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) katika Shule za Sekondari, Kilimo endelevu na elimu ya afya ya Jamii.

Peace Corps ni mtandao wa kimataifa wa huduma wa Wafanyakazi wa kujitolea, Wanajamii, Wabia katika Nchi wenyeji na Wafanyakazi wanaosukumwa na lengo la Shirika hili la kujenga amani duniani na urafiki ambapo hufanya haya kwa kuzingatia mwaliko wa Serikali wenyeji na Wafanyakazi wake ambapo kwa Tanzania Shirika hili limehudumu kwa zaidi Ya miaka 60 toka Septemba 1961 na kuhusisha Wafanyakazi zaidi ya 3200.
Screenshot_20230226_040825_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imesema itasimamia na kugharamia taratibu zote za mazishi ya Wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji waliofariki kwa kuzama kwenye Mto baada ya mtumbwi kupinduka wakati wakielekea Shule.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema hayo baada kufika kaika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni kuaga miili ya Wanafunzi wawili waliopatikana leo kadokando ya Mto huo unaomwaga maji katika Ziwa Tanganyika.

"Kwa niaba ya Serikali ya awamu ya sita naomba niwafikishie salamu za pole kwa msiba mkubwa uliozikumba Familia hizi, tumepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa na tunaungana na Familia pamoja na Ndugu katika masikitiko haya makubwa tunajua hakuna mwenye uwezo wa kurejesha uhai uliotoweka ila tunaomba tuungane kwenye huzuni hii"

"Na serikali kwa upande wake itajitahidi kila inavyoweza ili kuwapumzisha kwa heshima Watoto wetu hawa ambao wamefariki, tutafanya tunavyoweza kuungana na Familia kuhudumia msiba ili tuweze kuwapumzisha wapendwa wetu vizuri, Serikali itaondoa changamoto hiyo kwa kutengeneza Daraja katika Mto huo"

Miili miwili iliyopatikana leo ya Wanafunzi hao ni mwili wa Tatu Sanaari na Ramadhani Nkwila(12) wa darasa la tano na wote wanazikwa leo, miili ambayo haijapatikana hadi sasa ni ya Watoto wawili Ashura Haruna wa darasa la kwanza na Zabibu, juhudi za utafutaji zinaendelea kufanywa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka Kigoma.
Screenshot_20230226_041028_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Marekani (FCC) imesema imepokea malalamiko 103 kuhusu utumbuizaji wa Mwimbaji Rihanna kwenye kipindi cha mapumziko ya mechi ya Super Bowl takribani wiki mbili zilizopita kwenye uwanja wa State Farm jijini Glendale, Arizona nchini Marekani.

Taarifa ya TMZ imesema Walalamikaji hao ambao walikuwa sehemu ya Watazamaji wa show hiyo walituma maoni yao kwa FCC na kuonesha kukasirishwa na mashairi ya Rihanna pamoja na uchezaji wake ambao walidai uliashiria vitendo vya ngono.

Malalamiko mengine yalielekezwa kwa Dancers wa Rihanna kwenye show hiyo na kusema waliwaona wakionesha ishara ambazo zilikuwa za kuudhi na zisizofaa kabisa kwa Watoto.
Screenshot_20230226_041132_OGInsta%2B.jpg
 
Watu wawili wanashikiliwa na Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchinja Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Butamo Igonzele (70) Mkazi wa kijiji cha Bumegezi Kata ya Ihanamilo Mkoani Geita.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlayi amesema Watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya uchunguzi wa awali kuonesha wanaweza kuhusika katika mauaji hayo huku jitihada zikifanyika katika kujiridhisha kupitia uchunguzi wa awali.

Watuhumiwa hao ni Joyce Julius ambaye ni Mtoto wa Marehemu na Juma Charles ambaye ni Mkwe wa Marehemu (Mume wa Joyce) ambapo inadaiwa walikuwa wanamtuhumu Marehemu (Mama yake Joyce) kuhusika na kifo cha Mtoto wao ambaye alifariki wiki moja iliyopita huku kifo chake kikihusishwa na ushirikina.

Tukio hilo limetokea February 22, 2023 usiku katika Kijiji hicho cha Bunegezi Kata ya Ihanamilo Wilaya ya Geita Mkoani humo ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua Mama yao.
Screenshot_20230226_041259_OGInsta%2B.jpg
 
Said Kibula (69) ambaye ni mmoja kati ya Watuhumiwa 8 wa tukio la wizi wa mali mbalimbali katika ajali iliyotokea hivi karibuni Wilayani Korogwe, Tanga ikihusisha Fuso iliyogongana na Coaster iliyobeba mwili wa marehemu pamoja na Waombolezaji wakitokea Dar es salaam kuelekea Kilimanjaro kuzika, amekutwa amejinyonga na chandarua shambani kwake usiku wa February 22,2023 .

Kaimu RPC Tanga, David Chidindi amesema Mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkazi wa Magira Gereza alikuwa nje kwa dhamana ya Mahakama ya Hakimu mkazi Korogwe .

Itakumbukwa wakati wa kuagwa kwa miili ya waliofariki kwenye ajali hiyo, mmoja wa Mashuhuda wa ajali hiyo aliibuka na kueleza namna alivyoshuhudia baadhi ya waokoaji walivyowaibia wahanga mali mbalimbali zikiwemo simu, nguo na fedha walizokuwa wamebeba na baadaye Serikali ilitoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka Watuhumiwa hao ambapo walifanikiwa kuwakamata Watu 12 na kati yao 8 walikutwa na hatia.

RC wa Tanga Omary Mgumba amesema mmoja kati ya Watuhumiwa 8 aliyekutwa na nguo za marehemu zikiwa na damu usiku amekutwa amejinyonga ambapo sasa wamebaki saba ambao wapo kwenye mkono wa sheria.
Screenshot_20230226_041401_OGInsta%2B.jpg
 
Simba imepata pointi 3 za kwanza katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kundi C ikiifunga Vipers bao 1-0 ugenini nchini Uganda. Bao la Simba limefungwa na Henoc Inonga dakika ya 20 likiihakikishia timu hiyo Sh5 milioni kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alisema atanunua kila bao moja Sh5 milioni katika mechi hizi zakimataifa kwa Simba na Yanga.

Simba inasogea nafasi ya 3 ikiwa na pointi ikiiacha Vipers yenye pointi 1 wote wakisubiri mechi ya Raja Casablanca (ina pointi 6) VS Horoya (ina pointi 4) saa 4:00 usiku.

Screenshot_20230226_041535_OGInsta%2B.jpg
 
Cristiano Ronaldo ametumia dakika 44 kufunga hat trick yake ya pili katika Ligi kuu ya Saudi Arabia wakati mechi hiyo ikiendelea timu yake Al Nassr ipo mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Damac FC. Katika mechi 5 alizocheza tangu ajiunge na timu hiyo amefunga mabao 8 na asisti 2 huku ikiwa hat trick yake ya 62 katika soka.
Screenshot_20230226_041657_OGInsta%2B.jpg
 
RAJA WAMESHINDIKANA !!
.
FT: RAJA CA 2-0 HOROYA AC
.
Msimamo Kundi C
1. Raja CA — 9pts
2. Horoya AC — 4pts
3. Simba SC — 3pts
4. Vipers SC — 1pts

Screenshot_20230226_041934_OGInsta%2B.jpg
 
MAMELODI WANANUSU ROBO !!
.
FT: AL AHLY 2-2 MAMELODI
34’—️ Shalulile
59’—️ Abdelmonem
74’—️ El Shahat
80’—️ Molena
.
Kundi B
1. Mamelodi — 7pts
2. Al Hilal — 6pts
3. Al Ahly — 1pts*
4. Cotton — 0pts*

Screenshot_20230226_042037_OGInsta%2B.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Home Boys
.
Haimbwi wala hatajwi kama wanavyotajwa kina Chama sababu yeye ni mchezaji mzawa.
.
Wakaona wakimpa majina mazuri watamkweza lakini wameamua kumuita PUNDA.
.
Khalid Aucho kapewa jina la Dokta, eti kwamba anajua mno kukata umeme na uwanjani anaheshimika kuliko PUNDA.
.
Sijui kacheza kiasi gani lakini macho yangu yanasema huyu ndiye MAN OF THE MATCH. Wote wanaoimbwa wamepotea.
.
Hongera Mzamiru Yassin Selemba, Home Boy.
.
NB:

Tunachukua 6 za Vipers, tunachukua 3 za Horoya kisha tunafuzu.
.
Screenshot_20230226_042457_OGInsta%2B.jpg
 
Jemedari Said

Hongera Mnyama kwa ushindi wa ugenini, haikuwa performance nzuri lakini ushindi wa ugenini siku zote ni muhimu sana.

Nafasi ya robo fainali imefufuka upya kwa ushindi huu muhimu sana.

Hampaswi kujiuliza kuhusu performance na yenu dhidi ya wale wengine kwenye makundi yao, muhimu ni robo fainali ili kuwa na consistency, hayo mengine yatajulikana siku ikifika.

BIN KAZUMARI MTIPPA (The voice of the voiceless)
Screenshot_20230226_042622_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Muhimu zaidi ilikuwa alama tatu, muhimu zaidi ni kuwa siku hizi timu imeweza kuvuna alama ugenini, muhimu ni kuwa ushindi huu wa ugenini unalipizia alama tatu zilizopotea dhidi ya Raja.

Muhimu ni kuwa msimu huu Simba ugenini imekuwa bora kuliko miaka yote, muhimu ni kuwa kimahesabu Simba anaweza kupenya akishinda tu mechi zake za home.

Muhimu ni alama tatu, kucheza vizuri sio kitu muhimu sana kwenye mechi hii muhimu na muhimu ni kuwa kila Mtu ashinde mechi zake tu
Screenshot_20230226_042734_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom