Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230226_050251_Opera%20Mini.jpg
 
Hizi ni picha kutoka Mkoani Kilimanjaro kwenye Tigo Kili Half International Marathon ya @tigo_tanzania ambayo inafanyika leo Jumapili February 26, 2023, katika viwanja vya Muccobs, Moshi, Kilimanjaro.

Kwenye hii picha umekosekana vipiii Mzigua90 naiona kampani yako yote hapa ikiongozwa na amina
Screenshot_20230227_045001_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mbunge wa Muheza Hamis Mohamed Mwinjuma maarufu MwanaFA kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Pauline Philipo Gekul ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.
Screenshot_20230227_045155_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan amemteua Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Mashimba Ndaki ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Screenshot_20230227_045252_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan amemhamisha Ridhiwani Jakaya Kikwete kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Screenshot_20230227_045343_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu amemhamisha Waziri Kindamba kutoka Mkoa wa Songwe kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga akichukua nafasi ya Omary Tebweta Mgumba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Rais Samia amemteua pia Dkt. Francis Kasabubu Michael kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, kabla ya uteuzi Dkt. Michael alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Rais Samia pia amemteua Bibi Christina Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Bibi Sophia Edward Mjema ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi - Itikadi
na Uenezi.
Screenshot_20230227_045430_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amemuhamisha Deogratius John Ndejembi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI huku David Ernest Silinde akihamishwa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwenda kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Rais Samia pia amemuhamisha Pauline Philipo Gekul kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria huku Geofrey Mizengo Pinda akihamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria
kwenda kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba a Maendeleo ya Makazi.
Screenshot_20230227_045529_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230227_045543_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230227_045558_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230227_045615_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Ramadhani Kailima kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi alichukua nafasi ya Dkt. Wilson Mahera Charles ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Screenshot_20230227_045737_OGInsta%2B.jpg
 
Huko Laliga BARCA kapasuka !!
.
FT: ALMERIA 1-0 BARCELONA
24’—[emoji460]️ Toure
Screenshot_20230227_045915_OGInsta%2B.jpg
 
POTTER: MASHABIKI CHELSEA WANATAKA MIMI NA WANANGU TUFE
.
Kimenuka. Kocha wa Chelsea, Graham Potter amefunguka amekuwa akipokea meseji nyingi za vitisho zinazomtaka yeye na familia yake wote wafe kwa sababu tu ya matokeo mabaya inayopata The Blues.
.
“Nimepokea barua pepe si nzuri sana kwasababu mashabiki wanataka mimi nife na watoto wangu wafe. Ukweli si meseji nzuri za kuzipokea. Kama unakwenda kazini kwako na kuna mtu anajiapiza kuhusu wewe, hilo haliwezi kuwa jambo zuri, kama mnanitazama kama mtu wa hovyo zaidi kwenye historia ya klabu.
.
“Unaweza kusema, Oh, sijali lakini sitaki kudanganya kwa sababu kila mtu anajali kwa hizi meseji za mitandaoni. Nataka kufanikiwa hapa, hivyo hayo mawazo ya kwamba sijali ni ya kijinga.

“Kama nitawaambia mkaulize familia yangu maisha yamekuwaje kwangu na kwao. Nadhani msingefurahia kabisa. Naelewa mashabiki wanakwenda nyumbani wakiwa na hasira kwa sababu timu yao haijashinda. Lakini, niwaambie maisha yangu kwa miezi hii mitatu au minne iliyopita, yamekuwa magumu.”
.
Mabosi wa Chelsea wanampa sapoti kocha Potter juu ya meseji hizo za vitisho anazotumiwa na atawekewa ulinzi zaidi.

…………….
Screenshot_20230227_050247_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

ERIK TEN HAAG, heshima kwa Vinyozi wote wanyoa vipara kisha heshima kwa Makocha wote wenye vipara! Ni muda wa kulitambua darasa maarufu, The Class of Upara alikuwepo Pep Guardiola, Zinadine Zidane, Jorge Sampaoli, Luciano Spaletti na Prof Nabi! Lakini mpokeeni rasmi mgeni mpya Erik Ten Haag.

God created the world, Dutch created Holland! FIFA made football, Erik Ten Haag teaches Football! Ni mistari mipya ianze kutumika baada ya usiku huu pale Wembley, ni wasaa wa kuanza kumpa heshima yake ETH, kazi ngumu kwa sura rahisi, vitu vigumu kwa namna rahisi, United kubeba ndoo haikuwa rahisi.

Wangindo wanasema utu uzima dawa, Waluguru walisema nazi haishidani na jiwe lakini sio kwenye kamusi ya Erik Ten Haag! Amepiga Mwalimu wake Guardiola, amempiga Mikel Arteta ambaye ni Mwanafunzi mwenzake na bado Kompany na Xavi! They either hate or get motivated, ila ETH anagawa darasa la bure kabisa.

Aliongea mbele ya kipaza kuwa anaziheshimu City na Liverpool lakini zama hufika mwisho!
Screenshot_20230227_050415_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya mechi 40 za Erik Ten Haag hatimae Man United wanabeba kombe baada ya miaka sita kupita.

Nyieee mashabiku wa man u tujuaneeee
Screenshot_20230227_050629_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom