Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv kwa ziara yake ya kwanza ya kushtukiza na iliyofanywa kwa usiri mkubwa kwasababu ya tahadhari za kiusalama, hii ni ziara ya kwanza ya Biden nchini Ukraine tangu kuanza kwa vita ya Ukraine na Urusi mwaka mmoja uliopita.

Ziara hiyo ya kushtukiza ameifanya wakati akisafiri kwenda nchi jirani ya Poland kukutana na Rais Andrzej Duda, New York Times wanaripoti kwamba safari hiyo ya siri ya Biden kwenda Ukraine imefanywa kupitia treni kutoka mpaka wa Poland.

Ripoti zinasema Biden aliondoka pia Marekani bila taarifa na hata taarifa zilipovuja kuwa ataenda Ukraine, Maafisa wa Marekani walikanusha.

Kabla ya mkutano na Waandishi wa Habari, Joe Biden amefanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kuwamwagia sifa Ukranie kwa mapigano yao ya kishujaa licha ya ukosefu wa uzoefu wa kijeshi “Tena cha kustaajabisha ni kwamba Watu wa Ukraine ni Raia wa kawaida ambao hawakuwahi kupata mafunzo ya kijeshi lakini jinsi walivyopiga hatua ya kishujaa ni jambo ambalo na Ulimwengu wote unajivunia.
Screenshot_20230221_045653_OGInsta%2B.jpg
 
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imetangaza kuanzisha utaratibu mpya wa ukataji wa tiketi kwa njia ya kadi katika kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi Luis Dar es salaam badala ya mfumo uliokuwa unatumika hapo awali wa kukata risiti za karatasi.

Mfumo huo mpya wa kadi za N-CARD unaanza rasmi siku ya leo February 20 2023 ambapo Abiria yeyote ambaye tayari alikuwa ana kadi hiyo akiitumia kwenye maeneo mengine kama Uwanja wa Taifa au Magogoni Ferry, ataendelea kutumia kadi hiyohiyo huku Abiria ambaye sio Mkazi wa Dar es salaam na anatumia mara moja kituo hicho cha mabasi atapatiwa kadi ya kutumia mara moja.

Kaimu Afisa Habari Manispaa ya Wilaya ya Ubungo Joina Nzali amewaambia Waandishi wa Habari kuwa kila anayeingia kwenye kituo hicho kwa sasa atapaswa kulipia ushuru getini kupitia kadi ya N-CARD hata kama tayari ameshakata tiketi ya basi tofauti na awali ambapo ilikua Abiria aliyekata tiketi ya Basi alikuwa anapita bila kulipia ushuru wa getini.

Mfumo wa kukata unakadiriwa kukusanya mapato ya Bilioni 5.4 kwa mwaka huku kwa mwezi ikikadiriwa kukusanya makusanyo ya shilingi milioni 420 wakati mfumo wa ukataji tiketi wa zamani kwa mwaka 2021/2022 uliingiza Bilioni 3.7 pekee.
Screenshot_20230221_045754_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za uwepo wa kimbunga "Freddy" zinazosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua taharuki kwa Jamii.

“Kwa takribani wiki sasa Mamlaka imekuwa ikifuatilia mwenendo wa kimbunga "Freddy" kilichopo Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi karibu na Pwani ya Madagascar na kujiridhisha kutokuwa na madhara
ya moja kwa moja kwa sasa kwa maeneo yaliyoko nchini kwetu”

“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa kina mwenendo wa kimbunga hiki na itatoa taarifa punde tu kutakapokuwa na haja ya kufanya hivyo”

“Aidha, Mamlaka inapenda kuikumbusha Jamii na Umma kwa ujumla kuwa kwa mujibu
wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya 2019, Mamlaka ya Haliya Hewa Tanzania ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutoa taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa na ni kosa kisheria mtu mwingine kufanya hivyo”
Screenshot_20230221_045843_OGInsta%2B.jpg
 
AL AHLY NA RAJA CASABLANCA NANI ALIKUWA BORA !?
.
“Al Ahly walifika kwa Mkapa siku chache baada ya kucheza pambano bora dhidi ya Bayern Munich katika klabu bingwa ya dunia na bado wakafungwa. Hawakuwa bora kuliko Raja? Je Simba wameshuka kiwango kutoka kule kwa kina Luis Miquissone na kufikia hatua ya kudhalilika kwa Mkapa? Au kuna mambo ya nje ya uwanja hayakufanyika kiasi cha kuleta tofauti kati ya Simba ile na Simba hii?
.“Vyoyote iliyo Simba ya juzi ilikuwa hoi na haikuwa Simba ile ambayo tulifahamu na kuiona kama fahari ya Taifa katika mechi za kimataifa.”

- Edo Kumwembe [mwanaspoti]
Screenshot_20230221_050105_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya kusambaa kwa video ikionyesha basi la timu ya Simba likiendeshwa kinyumenyume (reverse) muda mrefu, dereva wa basi hilo na meneja wa timu, wamevunja ukimya wa tukio hilo huku jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani likieleza kuendesha gari kinyumenyume umbali mrefu ni kosa.

Mwanaspoti imezungumza na dereva wa basi hilo Peter ambaye alisema hayuko tayari kuzungumza lolote, lakini atakata meneja wake azungumze kwa niaba yake kwani walikuwa pamoja.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema hiyo si mara ya kwanza kwa basi hilo kuendeshwa hivyo, ingawa video zinazosambaa zimekuzwa kutokana na mechi yao na Raja Casablanca ya Morocco ya hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa.

"Lile ni basi letu ndiyo, na si mara ya kwanza kuendeshwa hivyo japo si kweli kwamba lilitoka Keko hadi kwa Mkapa likiendeshwa kinyumenyume," alisema na kuongeza

"Ile video pale ni Masaki, kwenye hoteli ambayo timu iliweka kambi (aliitaja) gari haliwezi kugeuza, inabidi lirudi kinyumenyume,"
Screenshot_20230221_050252_OGInsta%2B.jpg
 
KUMEKUWA na fununu nyingi juu ya kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya kutakiwa na timu kadhaa za ndani na nje ya nchi wakati mkataba wake ukielekea ukingoni na fasta mabosi wa klabu hiyo wamefanya jambo kwa kumuita kipa huyo mezani ili kuzungumza naye.

Simba imeamua kukaa mezani na Kakolanya aliyewahi kuzichezea Tanzania Prisons na Yanga, kwa nia ya kujadiliana juu ya kumpa mkataba mpya mara watakapoafikiana.

Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu na Kakolanya, zinadai baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, walimuita kipa huyo huyo na kuzungumza naye wakimuwakilisha mwenyekiti wao, Salim Abdalah ‘Try Again’ aliyekuwa bado hajarudi nchini na mchezaji akiwa keshaingia kambini Jumanne iliyopita.

Chanzo hicho kililiambia Mwanaspoti, katika majadiliano hayo wajumbe walimuambia kipa huyo, Simba ipo tayari kumpa Sh 60 milioni, lakini Kakolanya aliwataka waongezewe mzigo.

“Wajumbe walitaka kumpa mkataba wa Sh60 milioni, ila jamaa akitaka Sh100 milioni, hivyo kushindwa kumalizana na kuahidiana kukutana tena baada ya mechi ya juzi.”

Screenshot_20230221_050358_OGInsta%2B.jpg
 
Licha ya ushindi wa mabao 3-1 ilioupata Yanga dhidi ya TP Mazembe kuna winga Phillipe Kizumbi wa Mazembe alikuwa msumbufu kwa beki wa Yanga akipiga chenga na kuweza kuingia karibu na goli la Yanga.

Screenshot_20230221_050503_OGInsta%2B.jpg
 
Kwenye press baada ya mchezo wao na Raja, Kocha wa Simba alisikika akilaumu kuwa hakuwa na timu pre season hivyo kuna ugumu anapata, lakini Kocha huyu wakati anatambulishwa alisema anafahamu malengo ya Simba na yupo tayari kudeliver.

Kocha hana solution?___
Screenshot_20230221_050940_OGInsta%2B.jpg
 
FARHAN KIHAMU

Huwa napenda sana kumsoma Emiliano Butragueno na falsafa zake kuhusu mpira, kisha Washindi kama Pep Guardiola, Wajivuni kama Jose Mourinho na Wajuzi kama Zinadine Zidane bila kusahau hekima kama za Carlo Ancelloti.

Kwa Butragueno aliwahi kusema mpira ni mchezo wa nyakati na timu ikipoteza atasemwa hata Mlinzi wa klabu ili mradi ipatikane sehemu ya kushikia lakini ukweli ni kuwa mpira una matokeo yake na maajabu hutokea, upe heshima mpira usilaumu.

Kwa Upara Pep Guardiola yeye mara zote anaamini Mashabiki au watu wa mpira wana tabia ya kukinai kisha kuhukumu, Simba inaweza kufungwa halafu mjadala ukawa Aishi au ghafla Zimbwe, au Bocco mzee ama Kapombe amechoka, hapo wamekinai hata kama hakuna uhalisia, Pep huwa hasikilizi Mashabiki kwakuwa anawajua.

Jose Mourinho mjivuni sana lakini its okay to be arrogant! Sioni sababu ya Simba kupoteana kisa mechi mbili, waliwahi kuwa na nyakati ngumu kama hizi na bado walipenya, waliwahi kuwa kundi moja na Vita, Ahly na JS Saoura, nani aliwapa nafasi Simba? Lakini walipenya.

Wala huhitaji propaganda ama Afisa Habari akuhamasishe bali rekodi zipo wazi na vitabu vinajieleza! Ilishawahi kuaminika Simba hatoki mbele ya Zamalek, ilitokea nini? Ilishawahi kuaminika Simba ana wazee wengi, je wamecheza robo ngapi? Nani anawazidi Afrika Mashariki? Ni sahihi kuwa na kiburi kwakuwa Historia ipo na ndio njia ya kupita nyakati ngumu.

Timu ambayo imetoka kufanya vizuri playoffs inakuwaje mbaya ghafla!? Timu ambayo imefanya pre season vizuri inakuwaje mbaya ghafla? Na kama Shabiki unaamini vipi kirahisi kuwa timu mbovu? Lazima uheshimu nyakati kwenye mpira, ni kawaida kila timu inapitia.

Mashabiki, Wanachama na Viongozi wanapaswa kutulia na kuwa ushirikiano kama Wavuta Sigara! Football is a game of Mathematics, zinahitajika tu hesabu nzuri ili wakae sehemu nzuri, haipaswi kuiondosha Simba kwenye michuano.

Hard times, create strong People and character! Time to wake the Lion and he has to roar, sure he has to! Another day, another fight!
Screenshot_20230221_051552_OGInsta%2B.jpg
 
Tafiti: Kifaa cha mbao kinachosemekana kuwa na umri zaidi ya miaka 2,000 katika utafiti mpya kimeonesha kuwa huenda kilikua kikitumika kama kifaa cha ngono kwa wanawake (sex toy).

Kifaa hicho kina urefu wa inchi 6.2 inaelezwa kuwa kilitumiwa na Warumi miaka 2,000 iliyopita!

Kiligunduliwa mwaka 1992 katika ngome ya Vindolanda Roman huko Northumbria, Uingereza.

Screenshot_20230221_051910_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom