Makapuku Forum

Mabao 200 kwa Harry Kane ndani ya EPL akiwa ni Mfungaji wa tatu wa muda wote nyuma ya Wayne Rooney na Alaan Shearer.

Harry pia amefikisha mabao 267 ndani ya Spurs na ndie mfungaji wao bora wa muda wote.
 
Miili miwili ya Watoto walioongezeka na kufanya idadi ya Watu waliofariki kwa ajali Korogwe kufikia 20, imejumuishwa katika zoezi la kuaga lililoongozwa na RC Tanga Omary Mgumba leo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kalist Lazaro alithibitisha ongezeko la vifo hivyo na kusema vifo vitatu vilivyoongezeka vyote ni vya Watoto ambapo Watoto wawili walikuwa wanatibiwa Mkoani Tanga na mmoja Muhimbili.

Watoto wawili (Doris Mrema na Tony Mrema) waliokuwa wanatibiwa Hospitali ya Bombo, Tanga wamejumuishwa kwenye zoezi la kuaga Tanga, huku mwili wa Mtoto ambaye alikuwa anatibiwa Muhimbili ukisafirishwa moja kwa moja kupelekwa Kilimanjaro.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewaonya Vijana kuacha kubahatisha maisha kwa kuendekeza kucheza kamari (Ku-Bet) na badala yake ameaataka wajifunze ujuzi mbalimbali ili wajiajiri na kukuza uchumi wao.

Kauli hiyo ameitoa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki “Maisha sio kubahatisha, mnakuwa Watumwa, tafuteni Vyuo vya Ufundi kama VETA mpate maarifa mjiajiri, najua wengi hawatafurahishwa na hili lakini huo ndio ukweli”

“Vijana siku nzima bize kwenye mkeka, Bet, unajiuliza hivi Kijana wewe , Kijana rijali kabisa mzima una mwili wenye nguvu, unakaa unasubiria eti niandike kwenye karatasi Timu fulani na Timu fulani itashinda hii, ili uishi”

“Sasa najua kuna Watu nawaharibia biashara lakini lazima tuambiane ukweli, tuachane na mambo ya kuishi kwa bahati nasibu tuchonge laini fanya biashara inayokupa matokeo mwishoni, achana na hii unatafuta Elfu 20 kila siku kwenda kumpatia Mtu mwingine anapata huko wewe unabakia unapiga miayo”
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu akiwa na muasisi wa chama hicho, Augustine Makelele baada ya kuwasili wilayani Ikungi mkoani Singida.

Lissu amewasili Ikungi kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe katika Uwanja wa Stendi Mpya.

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema ujenzi wa soko la Kariakoo inatarajiwa kukamilika Oktoba 2023.

Mradi huo ulianza kutekelezwa Januari mwaka 2022 na ujenzi wake ulitokana na kuungua moto kwa soko hilo.

Makalla ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Februari 5, 2023 alipohotubia katika maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM.

Amebainisha ujenzi wa soko hilo utakapokamilika wafanyabiashara 3,500 wataingia ukilinganisha na 1,200 waliokuwepo awali.

 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga amewaongoza wabunge na wenyeviti wa halmashauri za Wilaya za mkoa huo kupiga magoti mbele ya wanachama wa CCM kushukuru ujio wa mradi wa maji.

Lakini pia viongozi hao walikuwa wakishukuru utekekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku wakimuomba Rais Samia Hassan Suluhu kumuacha Njombe, mkuu wa Mkoa huo Antony Mtaka.

Kwa muda mrefu baadhi ya miji ya mkoa huo imekuwa ikihaha kupata maji ya uhakika.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga alisema zaidi ya Sh1.073 trilioni zitatumika kutekeleza miradi maji kwenye miji 28 ya Tanzania, Njombe ikipata ndani ya miji mitatu.

 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu atapokewa kwa mila za kabila la Kinyaturu kwa nguo zake alizopigwa nazo risasi kutolewa rasmi, kufuliwa na kupewa wazee kwa ajili ya kuzivaa.

Akizungumza na Mwananchi, Katibu wa Chadema Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Ibrahim Saidi alisema mkutano wa leo utakuwa na ajenda kadhaa, lakini kubwa ni mapokezi ya Lissu kurudi nyumbani.

Alisema nguo za Lissu, zikiwamo shati, suruali, koti, viatu na soksi ambavyo vilihifadhiwa vikiwa na damu vitatolewa siku ya Jumatatu (kesho) kwa ajili ya kumwagiwa mafuta aina ya samli na baadaye zitafuliwa na watapewa wazee wazivae hadi zitakapochakaa.

Lissu alikuwa mbunge wa Singida Mashariki tangu mwaka 2010, alivuliwa ubunge Juni 28, 2019 akiwa kwenye matibabu nchini Ubelgiji kwa madai ya kutoonekana bungeni bila Spika kuwa na taarifa ya maandishi na kutojaza fomu ya tamko la mali na madeni.

Mwanasiasa huyo alikumbwa na mkasa wa kupigwa risasi zaidi 30 Septemba 7, 2017 na kujeruhiwa akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma alipotoka kuhudhuria vikao vya Bunge.

 
Simba imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa Mkapa, Dar. Bao la Hilal limefungwa na Makabi Lilepo na Simba Habib Kyombo.

Kipa wa Simba, Beno Kakolanya licha ya kuruhusu bao moja ameokoa baadhi ya mashambulizi ambayo yalikuwa hatari langoni mwake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…