Shaffih Dauda
Wakati nikiwa Belgium nilikutana na CEO wa klabu ya K. Beerschot V.A Mr. Frederic Van den Steen, katika mazungumzo yetu kuhusu soko la wachezaji wa Afrika barani Ulaya aliniambia siku hizi hawaangaalii kipaji peke yake kuna vitu vingi wanazingatia ikiwa ni pamoja na aina ya uchezaji wa mchezaji husika na aina ya uchezaji wa timu yao.
Aliniambia siku hizi mambo yamebadilika sana, hatuendi tena Afrika kutafuta mchezaji mwenye kipaji tu! Bali tunaenda kutafuta mchezaji mwenye aina fulani ya uchezaji kulingana na aina ya uchezaji na mahitaji ya timu.
Kwa mfano timu inahitaji mshambuliaji, kipaumbele sio rekodi yake nzuri ya magoli aliyowahi kufunga huko nyuma au katoa assist ngapi kwenye msimu.
Wao wanataka mchezaji ambaye anapiga kazi kweli, timu yao inacheza high-line pressing, kwa hiyo wanahitaji aina ya mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufanya pressing kuanzia juu.
Wanajua hawezi kufaya pressing kwa dakika zote 90 lakini angalau aweze kufanya hivyo kwa dakika 55 hadi 60. Muda wote huo aweze kukimbia kati ya dakika 90.
Kwa hiyo wao wanahitaji mshambuliaji kulinagana na work-rate yake uwanjani sio kafunga magoli mangapi. Wakipata mchezaji wa aina hiyo wanamchukua kwa sababu atawasaidia, wakati anafanya pressing wachezaji wengine wanatengeneza nafasi za kufunga wakitokea nyuma bila ya kuwa na presha.