Makapuku Forum

DERBY KUAMUA HATMA YA NABI YANGA.
.
Tayari kumekuwa na taarifa za chini chini kocha huyo Mtunisia hana muda mrefu kabla ya kutupiwa virago kwani mabosi wake hawataki kuona timu yao inapata matokeo mabaya zaidi.
 
Umeiona hii picha? Huu ni utamaduni wa Real Madrid kuwa Rais wa klabu atasafiri na Malegend kadhaa kuhudhuria tuzo ambazo Kijana kutoka Madrid atabeba tuzo, kwao wachezaji wao wa zamani ni taswira ya klabu, uhusiano wao hautamatiki baada ya kustaafu bali hudumu daima.

Zinadine Zidane, Ronaldo de Lima na Luis Figo wakiwa na Rais Perez ambaye ndie aliyewasajili kwenye zama za Galacticos hawa wote wana Ballon dor na jana walishuhudia Karim akibeba tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.
 
Karim Benzema anakuwa Mfaransa wa tano kubeba tuzo hiyo baada ya Raymond Kopa, Jean Pierre Papin, Zinadine Zidane na Michel Platin.

Baada ya nyota Stanley Mathews kushinda Ballon dor akiwa na miaka 41, Benzema anakuwa Mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo akiwa na umri mkubwa ndani ya miaka 66.
 
Farhan Jr

Super Sadio Mane alipoitwa jukwaani kuchukua tuzo ya Socrates iliyotokana na mchango wake kwa jamii ya Senegal
alipewa mic aelezee kuhusu tuzo hiyo na vitu anavofanya huko kwao.

Bahati mbaya sana MC hakuelewa utamaduni wa sisi waafrika lakini pia hakuelewa imaan ya Mane inataka nini, Mane ni Muislam na hapaswi kujisifia vile anavyofanya kwao ile ni kama sadaka hupaswi kusema.

Mane alipopewa nafasi ya kuongea ni kama alipata wakati mgumu sana kuongea, alishukuru kwanza kisha akasema “Ni kama hivyo ulivyosema tu” yani hakutaka kujazia sana maneno akamwambia MC ni kama hivyo ulivyosema.

Wakati Mane anapata hicho kigugumizi, Legend mwingine wa Afrika, Didier Drogba ambaye nae alikuwa MC aligundua mapema sana na aliona kama Mane hawezi kujielezea sana akamuwahi na kusema “Thank you Sadio” kisha Mwamba akashuka na kuondoka zake.

MANE atafundisha mengi sana, anatufundisha mstari kati ya mali na ubinadamu, umaarufu na uungwana kisha pesa na roho safi! Vyote vimekuja kwake ila Mane na imaan yake safi ya kiislam na roho yake ya kiungwana imesalia.

IMAAM wa msikiti wa Liverpool atakuwa amemmiss sana, kwakuwa alikuwa wa kwanza kuingia msikitini kusafisha miswala na kusafisha vyoo, muungwana na Mtu safi kutoka Bambali huko Senegal.
 
So sad
 
Hata kama mafanikio yanatisha lakini sio sawa na umasikini aisee!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…