Farhan Jr
Fanya ufanyavyo ila Matajiri wengi wanapenda vitabu vibalance, wanapenda kuona CEO anaokoa hata mia mbovu ambayo ingekuwa hasara kwa Boss.
Roman Abramovich pale Chelsea alikuwa na Marina ambaye alimtoa kwenye kampuni zake za mafuta, hakuwa na interests za kimpira ila alikuwa na interests kubwa za kibiashara, yani Chelsea ikuwe na Boss asipasuke sana.
Nyote mnakumbuka namna Marina alivyosajili sana kwa bei rahisi na kuuza wachezaji kwa bei mbaya sana, nyote mnakumbuka namna Chelsea ilivyopanda thamani na NIKE walivyodouble pesa pale.
Huyu Barbra kutoka London School of Economics, anaweza asiufahamu sana mpira kama wengine ila anaifahamu biashara ndani ya mpira, anafahamu KPIs za biashara ya mpira, Boss MO amerelax tu huko Dubai.
Katika hali ya kawaida Bwana Dejan angeweza kudai mabillion ya pesa kwenye mkataba ule wa miaka mitatu lakini kwa hesabu kali za kimpira huenda akailipa Simba au waamue tu kumwachia, hesabu hizo za mpira.
Ingekuwa zamani MO angepigiwa simu na kuambiwa Boss tunapaswa kumlipa Dejan! Naam ni akili kama hizi za biashara ambazo zinachukuwa sana kwenye mpira kwakuwa wao mpira sio sifa bali BIASHARA.
Huyu akisema aseme yote yanayoendelea maishani mwake atajaza vitabu, kama ambavyo Marina alivyoingia na kugundua mengi ya Michael Emenalo na namna ambavyo sometimes alikuwa anafuja mtonyo wa Roman.
Nipo zangu kwenye Abood naelekea Nyumbani Morogoro nataka niwahi ugali na mlandu kaliandili, wapi ndipi ramani na Baunsa kutoka Mto Lumemo na Kivukoni, Ifakara
View attachment 2372077