Makapuku Forum

Hafla ya kumtangaza Mfalme Charles III zimeanza leo Jumamosi Septemba 10, 2022 katika kasri la St. James’s jijini London.

Charles ambaye ni baba wa William na Harry, ndiye anayeshika kiti cha Malkia wa Uingereza, Elizabeth II kutokana na kifo cha mama yake.
 
Mfalme Charles III leo Jumamosi Septemba 10, 2022 atakutana na viongozi wa dini na kisiasa wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Uingereza katika Kasri la Buckingham.

Taarifa iliyotolewa leo na Kasri hilo imesema pia Mfalme atampokea Askofu Mkuu wa Canterbury na msimamizi wa Westminster.

Aidha mfalme huyo atakutana pia na wajumbe wa Baraza la Mawaziri watakaokuwa wameambatana na Waziri mkuu wa nchi hiyo, pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani.

Mfalme mpya huyo anatangazwa leo katika hafla inayofanyika katika Kasri la St. James’s jijini London.
 
Mfalme Charles wa III ametangazwa rasmi kuwa Mfalme mpya wa Uingereza, katika sherehe zilizorushwa moja kwa moja kupitia Televisheni.

Sherehe hizo zinafanyika katika Kasri la Mtakatifu James mjini London, zinahudhuriwa na Baraza maalumu linahusika na kutawaza Ufalme na linaundwa na Wanasiasa waandamizi na Maafisa wengine washauri wa Ufalme.

Charles wa III alichukua mikoba ya Ufalme moja kwa moja mara baada ya kifo cha Mama yake Malkia Elizabeth wa Pili kilichotokea siku ya Alhamisi lakini sherehe za kutawazwa ni hatua muhimu ya kikatiba ya kumtambulisha Mfalme mpya nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kufanyika tangu mwaka 1952 wakati Elizabeth alipotawazwa rasmi kuwa Malkia, Mfalme Charles wa III ameahidi kufuata nyayo za mama yake wakati wa hotuba yake ya kwanza aliyoitoa hapa jana.
 
Nini kimetokea Auntie?
Mashangazi tumefanyaje tena?
Mweh!!!

Maana mahali niko saa hii hata kumwambia mtu "muone" siwezi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…