Makapuku Forum

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto amefariki dunia muda mfupi baada ya kutoa mahubiri katika ibada ya mazishi ya mke wa Askofu mwenzake, Hilda Lugendo iliyofanyika wilayani Muheza mkoani Tanga.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Mndolwa aliyeongoza misa hiyo katika Kanisa la Kristo Mfalme Muheza, amesema wamepewa taarifa kutoka hospitali kuwa Askofu Chiteto alipatwa na mshtuko wa moyo.

“Madaktari wametuarifu kuna kitu kinaitwa cardiac arrest. Alikuwa na shida ya pressure (shinikizo la moyo) na kisukari,”

“Yeye alikuwa mhubiri na kwa kweli mahubiri yake yaliwavuta watu na neno lake la mwisho ni mlango umeandaliwa twendeni, basi anakwenda kukaa na Mungu akamwita,” amesema Askofu Mndolwa.

Akifafanua jinsi kifo cha askofu huyo kilivyotokea, msemaji wa kanisa hilo, Maiko Luoga amesema, Askofu Chiteto alihubiri katika misa hiyo na kumaliza, kisha alipokaa aliishiwa nguvu na kukimbizwa katika hospitali teule ya Muheza.
 
Waziri wa Tamisemi, @innocentbash amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo @ortamisemi, Profesa Riziki Shemdoe kusimamia Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) kufanya usanifu kwa haraka katika maeneo ambayo yapo pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam ili kuweka mpango wa kufikisha huduma ya mabasi ya mwendokasi ikiwamo maeneo ya kama maeneo ya Vikindu, Kigambo na Chanika.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo hayo leo Jumamosi Septemba 3, 2022 alipoambatana na Kamati ya Kudumu ta Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kutembelea na kukagua miradi ya DART jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo amesema dhamira ya Serikali ni kuongeza mtandao wa barabara za mwendokasi kwa kufikisha huduma ya mabasi katika maeneo pembezoni yenye watu wengi na kuboresha huduma katika maeneo ambayo yana huduma za mabasi ya mwendokasi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…