GagfatyaujH£#@&"*Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo akiwa Dodoma amekutana na Waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi ishu ambayo imekua gumzo nchini kuhusu masuala ya tozo kwenye miamala ya simu na benki ambapo amesema “Mimi nasema tu atakayetaka kutukana atukane tu, hata kama nitakosa Rafiki hata mmoja sawa tu lakini lazima niseme ukweli hata Mtu ana ng’ombe Elfu 12 mnataka Bwawa lake lijengwe kwa kodi ya Nesi au Mwalimu”
Yaani hata waelezee wamevua nguo, hawawezi kueleweka.Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa leo Dodoma amezielezea faida ya tozo kwenye sekta ya afya, elimu na miundombinu katika nukuu zifuatazo “Tozo zimeboresha miundombinu, kwa kipindi ambacho Rais Samia amekuwa madarakani katika Tarafa 570 tayari tumeshajenga vituo vya afya kwenye Tarafa 207 ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani”
“Pia kuna maeneo ambayo ni magumu kufikika tuliyabainisha na kwa kipindi ambacho Serikali ya awamu ya sita imekuwa madarakani kupitia tozo za miamala ya simu tumejenga vituo vya afya 234 kwa Bilioni 117 kwenye tarafa nilizozitaja na maeneo magumu kufikika na kila kituo cha afya kimetugharimu Tsh. Bilioni 500, tangu Uhuru na awamu zote za Serikali ambazo zimekuwepo kujenga vituo vya afya 234 sio jambo la kawaida, tunamshukuru sana Rais”
“Vituo vya afya hivi lazima tuvipeleke vifaa vya kisasa Serikali ilituwezesha TAMISEMI Bilioni 149.5 tumeshakamilisha hatua za manunuzi ili tupeleke vifaa tiba kwenye vituo vya afya “
“Watanzania hapa hoja sio nanufaika vipi na tozo ishu ipo kwenye maeneo ambayo Waziri Mwigulu ameyasema, tusingeweza kujenga vituo vya afya 234 ndani ya mwaka mmoja kama sio hizi tozo, tozo hizi zina faida”
View attachment 2342276
Cha kujitetea hawana aibuYaani hata waelezee wamevua nguo, hawawezi kueleweka.