Shaffih Dauda
Kwenye umri wa miaka 22 tayari George Best alikuwa staa za Ireland Kaskazini na Manchester United, huku akiwa ametwaa Ballon dor
Alipofikisha umri wa miaka 28 tayari alikuwa na makombe sita makubwa ikiwemo UEFA na mabao 181 kwenye jezi ya Manchester United, lakini alishindwa kumudu presha ya umaarufu na pesa
Pombe na wanawake zilikuwa starehe zake kubwa sana George Best, ilifika wakati alidiriki kusema alijaribu kuacha wanawake na pombe kwa dakika 20 tu lakini zilikuwa dakika ngumu zaidi kwenye historia ya maisha yake
Matumizi ya kupitiliza ya pombe yalimsababishia maradhi ya ini huku pia wanawake wakimfanya awe na afya duni pia, stori ilibadilika ghafla sana
Wakati anakimbizwa hospitalini baada ya hali kuwa mbaya zaidi 2005, aliwaambia watu wake wanunue kurasa kwenye gazeti fulani na akaweka tangazo “TAFADHALI MSIFE KAMA MIMI”
Ujumbe kwenu vijana, msife kama yeye
DIGALA