[emoji3578] Scanda24
FOOTBALL ECONOMY || Emotional Intelligence [emoji419]
.
BYUTI BYUTI
Umetoka kuchukua vikombe heshima ya mashindano yote rasmi yanayotambulika na shirikisho, umetoka kufanya Uchaguzi na Usajili makini na kila siku unajinasibu wewe ni timu ya WANANCHI.
.
THEME ya kuelekea siku muhimu ya kufungua msimu unakuja na masihara ya kauli mbiu isowaunganisha wananchi wako. Byuti Byuti Ndio nini na inawakilisha nini katika safari yetu ya ubora na pesa..?
Bora wangeniomba niwape #HeshimaFullTank ili ibebe maono ya Heshima waloiweka kuanzia kwenye makombe hadi kushinda vita za usajili. #HeshimaFullTank ingewakilisha mustakabali wa Kibiashara na kuwafanya wananchi watambe.
.
#HeshimaFullTank[emoji736]️[emoji736]️
#ByutiByuti [emoji777]️[emoji777]️[emoji777]️
.
.
HATUZUILIKI, HATUSHIKIKI
Umetoka kwenye msimu hujashinda kitu chochote, umetoka kwenye msimu mgumu wa mashindano ya ndani na nje ya nchi kisha unasema HATUZUILI, HATUSHIKIKI. Wapo nyuma ya muda kuna sehemu wana shida kwenye kuwasiliana.
.
Kampeni ya mwaka huu ilipaswa kuwaleta watu pamoja sio kuwapa sifa wasokua nayo ni kukejeli mioyo ya ushabiki. Badala yake walipaswa kuwapa nguvu, kuwapa moyo na kuwashikanisha, ilitakiwa itengenezwe THEME kama vile tunarudi kwenye wakati wetu.
.
Wangeniita mimi ningewapa #NguvuMojaExtra ni slogan ya timu lakini ni kuamka kutafuta tena heshima waloipoteza. NGUVU MOJA EXTRA ingewapa mashabiki morali wa kwenda kuipigania timu mara mbili ya ilivyokua na mwisho kuonesha nguvu ya UDHAMINI.
.