[emoji3578] Farhan Jr
Anaweza akatokea Mtu akasema Mdhamini Mkuu kaweka mzigo mrefu kuliko Mwekezaji MO, wengine wataenda mbali watasema Simba wamepigwa ila sio kweli
MO alichokifanya ndani ya Simba ni kuipa timu thamani waliyokuwa nayo hii leo, kuifanya iwe taasisi ambayo kila kampuni inajisikia fahari kusaini nao mikataba, kwakuwa kuna SECURITY
Mafanikio ya Simba Afrika ni mikono yake na miamala yake, usajili, camping na mishahara ya wafanyakazi wote ni sehemu ya pesa zake, ndio thamani tunayosema
Ukifuatilia Roman Abramovich, hata Fahad Moshiri pale Everton thamani ya pesa waliyonunua timu haiendani na thamani ya sasa za klabu hizo, ni kwakuwa pesa ina tabia ya kuzalisha pesa
Hivi mnafahamu kuwa kwenye michuano ya Afrika pesa na posho zote zinatoka baada ya michuano kuisha? Maana yake ni nini? Maana ni kuwa gharama zote ni za MO na Makampuni ubia, lets agree amefanya kazi kubwa
MO deserves an applause ni basi tu sisi wenye vipato vyetu vya chini tuna nongwa mno[emoji3] hata Mimi kuna muda nanuna bila sababu, ni huu ufukara wetu tu[emoji3]