Makapuku Forum

Makapuku Forum

KWA MAANDALIZI HAYA MTAUMIA
.
Nyota wa Kikosi cha Simba [emoji1241] wanashuka tena dimbani kesho kucheza mchezo wa TATU wa kirafiki dhidi ya timu ya Haras El Hodood iliyopanda daraja ya kushiriki Ligi Kuu ya Misri [emoji1093] msimu ujao mtanange utakaopigwa katika Mji wa Cairo.
.
Mchezo huo utapigwa kesho saa 10 Jioni kwa saa za Misri ambapo ni sawa na saa 11 kwa hapa nyumbani.
…………….
Screenshot_20220726-195236_OGInsta%2B.jpg
 
MMEMSIKIA KOCHA ZORAN, ANATAKA PIRA LA KASI [emoji298]️
.
[emoji860]"Mimi ni muumini wa soka la kasi, sitaki mchezaji akae na mpira muda mwingi na sitaki pasi za nyuma, katika mchezo uliopita kipindi cha kwanza wachezaji walikuwa wanakaa sana na mpira na kupiga pasi zisizokuwa na faida.
.
“Lakini kipindi cha pili kasi iliongezeka na wachezaji walikimbia kuelekea mbele ndo maana tukaweza kupata magoli matano ukilinganisha na kipindi cha kwanza ambacho tulifunga goli moja pekee,"
Screenshot_20220726-195340_OGInsta%2B.jpg
 
Beki Kibwana Shomari msimu ujao atakuwa kwenye mtihani mwingine kwenye kikosi cha Yanga kuhakikisha anaonyesha ubora wake kwa mara nyingine.

Kibwana alisajiliwa kama beki wa kulia na Yanga akitoka katika kikosi cha Mtibwa Sugar, lakini alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutopata nafasi upande wa kulia mbele ya Djuma Shaban na kugeukia upande wa kushoto, ambako alikuwa anacheza dhidi ya Yassin Mustapha na David Bryson baada ya wawili hao kusumbuliwa na majeraha.

Upande wa kushoto alijihakikishia namba mbele ya Bryson na Yassin, ambao majeraha kwao yaliwafanya warudi nyuma kwani hata Kibwana akiwa hayupo bado alikuwa anacheza Farid Mussa kwenye eneo la beki wa kushoto.

Msimu huu unaonza, Yanga imemsajili beki wa kimataifa, Joyce Lomalisa kucheza upande wa kushoto na atakuwa sambamba na David Bryson, kwani Yassin Mustapha ameshaachana na timu hiyo na tayari ameshajiunga na Singida Big Stars.

Hivyo, Kibwana atakuwa kwenye mtihani mwingine msimu ujao kushoto (Lomalisa) na kulia (Djuma), lakini upande wa Kibwana anaweza kumpiku Lomalisa kutokana na uzoefu wa Ligi Kuu na tayari alishafanya kazi chini ya kocha Nasreddine Nabi.

Screenshot_20220726-200207_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi leo amepokea tuzo yake ya Kocha Bora wa msimu wa 2021/22 baada kurudi kutoka mapumziko ambapo hakuwepo kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Julai 7 kwenye ukumbi wa Rotana Hotel Jijini Dar es Salaam.
Screenshot_20220726-200408_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Barcelona, Xavi amedaiwa kutaka kumrudisha Lionel Messi, akimtaka rais wa klabu hiyo, Joan Laporta kumrudisha nyota huyo wa PSG msimu wa 2023/24.

Messi aliondoka Barca msimu uliopita baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Barca na kuiacgha miamba hiyo katika hali mbaya kiuchumi.

PSG ilijitosa kumsajili nyota huyo mwenye miaka 35, ambaye alikwenda kushinda tuzo ya saba ya Ballon d’Or, mwishoni mwa mwaka jana.
Screenshot_20220726-200509_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Simba kesho Jumatano itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Haras El Hodoud ambao utapigwa jijini Cairo.

Haras inashiriki Ligi daraja la pili nchini Misri ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi 60 katika mechi 30 ilizocheza.
Screenshot_20220726-200637_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji599]| Baada ya Ronaldo kuripoti Carrington leo hii alihudhuria kikao cha wachezaji na bench la ufundi ambapo Kocha alizungumza kwa saa zima kuhusiana na ziara yao.

Kuhusu suala la Ronaldo ni kuwa msimamo wa United RONALDO HAUZWI ingawa walipokea wazo kutoka kwa Jorge Mendes kuwa waongeze mkataba kisha wamtoe kwa mkopo akacheze UEFA, United hawapo tayari kumtoa.

Bado haijulikani kama atacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wrexham siku ya kesho ila mpaka sasa msimamo wa United ni kuwa hauzwi.
Screenshot_20220726-200808_OGInsta%2B.jpg
 
“Kylie Walker ndie mchezaji mgumu zaidi kwangu kuwahi kukutana nae kwenye EPL, ana nguvu kuliko mimi na ana kasi kuliko mimi” Eden Hazard, akijibu swali la Mwandishi wa ESPN
Screenshot_20220726-200910_OGInsta%2B.jpg
 
“Sijali sana kuhusu kombe la dunia lijalo kwakuwa kwangu sio kombe la dunia, sipingani na mpango wa kupeleka mpira sehemu zote duniani kama Afrika Kusini na Amerika, ila Qatar sio nchi ya mpira na hawana huo utamaduni bali ni pesa tu” Eric Cantona
Screenshot_20220726-201005_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji3578] Shaffih Dauda

Mara kadhaa nikipata wasaa wa kuzungumza na vijana wangu au mtu yoyote mwenye ndoto huwa napenda kumsikiliza zaidi yeye, nijue kama anajiamini kwenye chochote anachokipigania.

Kama jibu ni NDIO basi ni rahisi kuisukuma ndoto hii na kuifanya iishi, cha kwanza lazima moyo wako uwe tayari kisha acha kila kitu na wekeza kwenye hiyo ndoto, amka sali sana, pakikucha kapambane sana.

Hakuna uchawi wowote, believe me there is no magic kwenye mafanikio, ni matokeo tu ya kutoka kwenye dimba la kubweteka na kusimama kila leo ili kuwa mpya.

This is my very humble advise kwa yoyote mwenye ndoto, nawaamini sana wale wanaoota ndoto na kutaka kuiishi, kwa nafasi yako, kwa nguvu zako kwa ajili ya kesho yako.

Hakuna jipya duniani, hakuna siri ya mafanikio zaidi ya kufanya ambacho moyo hautaki tena kwa kujilazimisha, ushindi upo hapo.

NDOTO, NDOTO, NDOTO amka kaiishi ndoto

DiGALA
Screenshot_20220726-201144_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom