Makapuku Forum

Makapuku Forum

Alooooh [emoji1787][emoji1787] akifurahia yeye inatosha sanaaaa niwaze vikoba niwaze michezo niwaze na kufurahia tendo la ndoa ebu watuache kwanza tupambane na hali zetu
Screenshot_20220726-193055_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali, Marco Gaguti amethibitisha kuongezeka kwa vifo vya Wanafunzi wawili wa Shule ya King David ambao walikuwa miongoni mwa majeruhi Watano waliokuwa katika hali mbaya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Ligula.

Vifo vyao vinafanya idadi ya vifo kufikia Watu 13 huku wawili kati yao wakiwa ni Dereva na Mwangalizi mmoja wa Wanafunzi ambapo miili ya Wanafunzi hao imeagwa leo katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula. RIP[emoji1545]
Screenshot_20220726-194155_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220726-194214_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov leo amefanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ya Uganda leo.

Lavrov aliwasili jana Jumatatu nchini Uganda kwa ziara ya siku mbili.

Ziara ya Lavrov Barani Afrika ilianzia mjini Cairo ambako aliwahakikishia Viongozi wa Misri kwamba mahitaji yao ya nafaka kutoka Urusi yatashughulikiwa na kutimizwa.

Lavrov aliwasili Kampala akitokea Brazzaville, Jamhuri ya Congo na anatarajiwa kuitembelea pia Ethiopia.
Screenshot_20220726-194334_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia amemteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania The Hague nchini Uholanzi ambapo kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa kitengo cha sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Screenshot_20220726-194438_OGInsta%2B.jpg
 
Benki Kuu nchini Zimbabwe imezindua sarafu za dhahabu katika juhudi za kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni nchini humo pamoja na kukabiliana na mfumuko wa bei lakini wachumi na nchini humo wanatilia shaka jambo hili.

Katika uzinduzi rasmi wa sarafu za dhahabu mjini Harare mapema jana, John Mangudya, Mkuu wa Benki Kuu ya Zimbabwe amesema sarafu hizo zimezinduliwa ili kupunguza mahitaji ya dola za Marekani nchini humo.

Wazimbabwe kwa kiasi kikubwa wanaepuka sarafu za ndani ya nchi hiyo wakiipa kipaumbele dola ya kimarekani ambayo wanaona kuwa inakubalika zaidi nje ya nchi na kushikilia thamani yake kwa muda mrefu.

Mangudya amesema ana matumaini kwamba Wazimbabwe sasa watachagua sarafu za dhahabu, ambazo zinagharimu takriban dola 1,800 (Tsh. 4,196,700) kwa kila sarafu moja, sarafu 2,000 zitatengenezwa na uzalishaji wa baadae utategemea hamu na uhitaji wa wananchi.

Wananchi kutokea nchini Zimbabwe wamelipokea hili suala kwa mashaka, wakisema mwananchi wa kawaida hatoweza kumudu gharama za sarafu hii, na kwamba imetengenezwa kwa Watu matajiri.
Screenshot_20220726-194540_OGInsta%2B.jpg
 
“Bye dady, bye mamy.” Hayo ndio maneno ya mwisho waliyoyatoa watoto wawili wa familia moja waliofariki dunia katika ajali ya basi iliyoua watu 11 wakiwamo wanafunzi tisa, wakiwaaga wazazi wao kabla ya kuondoka nyumbani kwenda shuleni.

Akisimulia kwa uchungu, Stella Yohanna ambaye ni mama wa watoto hao wawili amesema kuwa hiyo ndio ilikuwa tabia yao na asubuhi baada ya kuwaanda walikwenda kumuaga baba yao kabla ya mama huyo kuwapeleka kwenye gari la Shule ya Msingi ya King David.

Stella ambaye ni mkazi wa Mtwara mjini amepoteza watoto wake wawili katika ajali hiyo ambayo imetokea asubuhi leo Jumanne Julai 26, 2022 eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini wakati watoto wakipelekwa shuleni.
Screenshot_20220726-194741_OGInsta%2B.jpg
 
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo (37) amerejea rasmi England leo asubuhi na kuelekea moja kwa moja katika Uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kocha Erik Ten hag ili amshawishi amruhusu aondoke klabuni hapo.

Nyota huyo wa Ureno, ameonekana akiwa ameambatana na meneja wake, Jorge Mendes wakielekea Carrington tayari kwa kikao hicho na Ten Hag ambaye ameonekana kumuwekea ngumu mshambuliaji huyo kuondoka katika kikosi chake licha ya Ronaldo kuonekana kutokuwa tayari kuendelea kusalia Manchester United.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kukutana na Ten Hag tangu alipowasilisha ombi lake la kutaka kuondoka kwa lengo la kusaka timu ambayo itampa fursa ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.
Screenshot_20220726-194856_OGInsta%2B.jpg
 
UONGOZI wa Yanga umethibitisha kuchelewa kujiunga kwa mastaa wao wawili, Bernard Morrison na Yanick Bangala kutokana na sababu mbalimbali.
Yanga tayari wameanza mazoezi ya kujiweka fiti kujiandaa na msimu mpya wa ligi sambamba na mashindano ya kimataifa wakiiwakilisha nchi Klabu bingwa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema wachezaji wote wamewasili kambini isipokuwa Bangala na Morrison ambao hadi alhamisi watakuwa wameungana na wenzao kwenye mazoezi.

"Mastaa hao taarifa za kuchelewa kwao zinafahamika lakini wote watawasili kesho na alhamisi wataanza mazoezi pamoja na wenzao ili kujiweka witi kuelekea msimu mpya," alisema na kuongeza;

"Ni wachezaji watano ambao walichelewa kujiunga na kambi ambao ni Khalid Aucho ambaye jana kaanza mazoezi, Fiston Mayele na Shaban Djuma ambao wataanza mazoezi leo baada ya kuwasili jana."
Screenshot_20220726-195004_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Juventus imethibitisha kiungo wake, Paul Pogba atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili baada ya kupata jeraha litakalomuondoa kwenye kikosi kinachosafiri kuelekea Dallas huko Marekani.

Kiungo huyo amepata jeraha hilo wiki mbili tu tangu ajiunge na miamba hao wa soka Italia.
Screenshot_20220726-195110_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom