[emoji3578] Khalid
Jemedari Said na Harakati za Mzee wetu Nelson Mandela .
Kipindi Taifa la Watu Afrika Kusini liko kwenye utawala wa Waholanzi kulikuwa na wanaharakati wengi ambao walipambana kuona Afrika kusini Siku moja inakuwa huru kutoka kwenye mikono ya Wa “ Dutch” Mapambano ya wanaharakati wengi yalionekana kugonga Mwamba na wengine kufa ,akiwa Gerezani Nelson aliwaza juu ya Taifa lake la Afrika kusini , alilifikilia zaidi Neno Afrika kusini kuliko familia yake , watu wa Jamhuri ya Afrika Kusini walikuwa Wapole mpaka Mwaka 1990 Nelson Mandela alipoachiwa huru na Frederik Willem De Klerk kutoka gereza la Robben kuja kulifanya Taifa la Afrika kusini kuwa huru .
Story inafanana Jemedari Said “ Bin Kazumari “ labda watu wengi walikuwa hawamfahamu ila ni mmoja Kati ya wana harakati wa Soka la Tanzania kabla hata ajaanza kufanya kazi kwenye Radio na Televisheni , watu wanaomfahamu wanasema Jemedari anaishi robo tatu ya Maisha yake kwenye mpira , anapenda mpira , anafatilia mpira , Anajua mpira na nzuri zaidi amecheza mpira na anajua kuongelea mpira .
Tangu amepata nafasi ya kusikika Kwenye Radio Jemedari amekuwa kama Nelson Mandela amewafungua watu wengi masikio hasa pale anapoongea kuhusu mpira , anagusa hisia na masikio ya watu wengi juu ya ukweli wa mpira wetu wa Tanzania.
Tasnia ilikosa watu wa jamii ya Jemedari kwenye kusema ukweli wa Mpira wetu , Nina Heshima kubwa na Wakubwa wetu kama Edo Kumwembe, Shaffih Dauda , Salahe Jembe na wengine wengi wamecheza vizuri nafasi zao kuongelea mpira wetu ila Jemedari amekuja kupiga Rangi sehemu ambazo zilisahaurika na Wana habari wakongwe wa Nyuma .
Mpira wetu unaitaji watu wakweli na wasiogopa kusema ukweli kama Jemedari Saidi .
Naona baadhi ya mambo yameanza kukaa sawa na Maji yameanza kujitenga na mafuta , tumeanza kuona tofauti ya Kunde na njegere.
Kila la Kheri Bin Kazumari .
[emoji860]@jemedarisaid ( The Voice of the Voiceless)