Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Ezekiel Olesow Laizer (30) kwa kupatikana na bangi misokoto 202.

Kamanda wa Jeshi la polisi Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema Mtuhumiwa Laizer ni mchimbaji wa madini mkazi wa Ngaramtoni Arusha.

ACP Kuzaga amesema tukio hilo limetokea 25/10/2021 huko katika geti la ukuta wa machimbo ya Tanzanite Mirerani ambapo hukumu hiyo imetolewa 22/07/2022 mjini Orkesument Wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.
Screenshot_20220726-052355_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imewahukumu kifungo cha miaka 30 au faini ya shilingi Million 350 laki 8 na Elfu 50 Watu wawili Halfani Kiumbili (41) na Zahoro Myovela ( 63 ) kwa kosa la kukutwa na vipande vinne vya pembe za ndovu vilivyokuwa na thamanai ya shilingi Milioni 35 na Elfu 85.

Watuhumiwa hao walikamatwa na pembe za ndovu novemba 12 mwaka 2020 katika kijiji cha kisilwa kilichopo Isimani Iringa vijijini wakiwa katika harakati za kuuza vipande hivyo vinne vya pembe hizo za ndovu ambazo ni sawa na Tembo mmoja.

Akitoa hukumu hiyo Hakim mkazi mkuu Saidi Ally Mkasiwa amesema kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 9 ambao walileta vielelezo vya ushahidi na kuthibitisha kuwa watuhumiwa hao walikuwa na pembe za ndovu kinyume na sheria.

Kesi hiyo ilisimamiwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Reuben Lubango ambapo aliiambia mahakama kuwa Tembo ni mnyama mwenye kuvutia na watalii wengi wamekuwa wakija nchini kutalii na hivyo kuingizia serikali mapato na kuendelea kupungua kwa tembo kutasababisha serikali kukosa mapato kwa ajili ya kufanya maendeleo ya nchi hivyo kuiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo.

Aidha Mahakama ilipowapa nafasi ya kujitetetea watuhumiwa wote wawili waliiomba mahakama waachiwe huru kwa sababu vipande hivyo vya meno ya tembo hawahusiki navyo, hata hivyo mahakama ikawahukumu kifungo cha miaka 30 kila mmoja au faini ya shilingi Million 350 laki 8 na elf 50 kwa kila mmoja.
Screenshot_20220726-053211_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom