Makapuku Forum

Makapuku Forum

[emoji3578] Jemedari Said

HILI OMBI AU AGIZO? NANI YUKO NYUMA YAKE?

Ukisikiliza hapa halafu uambiwe huyu anaeongea hapa ni Mwananchi wa KAWAIDA anamuomba Mh: Waziri Mohamed Mchengerwa utakataa. Haishangazi kupelekwa maadili na akakutwa na HATIA.

(The guy totally doesn't know how to communicate ethically...!!)

Kama una akili sawaswa unajiuliza NANI YUKO NYUMA YAKE, Kama yuko peke yake KWANINI HAKEMEWI?

Wapi Mh: Waziri Mchengerwa aliagiza Haji ahukumiwe? Au mimi ndo sikuelewi hotuba yake. Tena eti aliagiza kwa MBWEMBWE na anamtaka akasimamie haki ya kiapo chake, kwa MBWEMBWE hizo hizo. No ethics of communication! Kama vile Mh: Waziri kamteua yeye, hakuna heshima kabisa!

Nimejiuliza nafasi ya Klabu kama muajiri wake katika hili nikaona WAMELIZIMA tu, nikajiuliza KWANINI wapo kimya? Kuna kitu hakiko sawa.

Tangu sakata hili limeanza Klabu imekaa kimya kabisa. Rais wa Klabu aliambatana nae kwenda kuomba msamaha ambao leo ni kama vile ameukana.

Hiki chaweza kuwa kipimo cha uongozi mpya ambao hauna hata mwezi madarakani. Unawezaje kuayaendea mambo mazito au magumu yanapotokea.

Leo ukiangalia matamko ya Wazee ambayo ymefanyika Klabuni, Afisa wao anapambana na mamlaka na kuihusisha Serikali (Waziri) kwenye kuhukumiwa kwake, kama anataka kuigombanisha Klabu na Serikali na Viongozi wako kimya. Wazee wanasema wanamtaka Rais wa nchi, yeye anaitaka Serikali iingilie kati, viongozi kama hawaoni.

Viongozi wapo nyuma ya mtu huyu au wamemtuma? Rais na Makamu wa Rais wa Klabu wasisahau Afisa wao huyu alitamka hadharani kwenye Press Conference kwamba wao ni RAFIKI ZAKE!

Nadhani wanapaswa kuwa Smart sana juu ya hili vinginevyo wanaingia mkenge kwa kuendekeza urafiki na kuogopa kuudhi washkaji.

NB: Ukiona hujjaelewa lala, hili sio saizi yako.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
Screenshot_20220726-041050_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Scanda24

FOOTBALL ECONOMY || Bingwa La Kufeli [emoji367]
.
Andiko langu lililopita watu wengi hamkulielewa sababu nimetumia lugha ya FASIHI kutoka kwa Mwalimu Bora wa Kiswahili kutokea Tanzania, Bi Tunu Msangi alinifundisha Nikaiva. Niliandika ili kutoa msaada kutokana na Tatizo.
.
Hakuna nguvu yoyote nyuma ya Haji, ndio maana unasikia hizi kelele kungekua na nguvu kusingekua na Kelele, kungekua na manung'uniko ya watu wanaompiga SPANA. HAJI hayupo sawa, Saikolojia yake haipo Vizuri na anaelekea kubaya.
.
Unachukuaje mamlaka ya Mheshimiwa Rais na kumtuma mteule wake kwa lugha Utakayo..? Namuhurumia hayupo sawa, ubinadamu umeniingia anatakiwa apewe msaada asipewe kichwa anazidi kupotea. Kuna muda kabla hujanyanyua silaha kwenda vitani waza matokeo.
.
Uongozi wa Yanga na Wazee kaeni naye, hii vita haina maslahi kwenu katika wakati huu mpo bora, msimuache Haji aende pekee yake bila ushauri, msimuache apigane Vita kiasi hiki, hana uwezo wa kushinda kwa Hoja. Haji amejaa usela ndio maana ilikua rahisi kufika hapa.
.
Yanga inaweza kuishi bila Haji ila Haji hana maisha kwa Sasa Bila Yanga. Anagalieni namna mtamsaidia ili abaki kwenye mstari asizidi kuharibu kila sehemu. Kama kabadili ushabiki basi abaki mshabiki wa Yanga apambanie nje ya Uongozi.
.
NB:
End Of An Era [emoji419]
Screenshot_20220726-041050_OGInsta%2B.jpg
 
FOOTBALL ECONOMY || Be Inspired [emoji419]
.
Timu ya Taifa ya wanawake ya Afrika ya Kusini imeshinda Kombe lake la Kwanza la Maifa ya Afrika kwa wanawake. Imewachukua safari ya maisha kuweza kushinda.
.
Kocha wa Timu ya Taifa #BanyanaBanyana Disiree Ellis imemchukua uzoefu wa kushinda Tuzo tatu za kocha bora wa mwaka wa CAF kwa wanawake. Hii sio safari rahisi, ni ubora ndio unakupa matokeo.
.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kila kukicha huwapa moyo mabinti zetu katika namna ya kipekee ili kuweza kulitetea Taifa letu katika medani za kimataifa. Muda wetu ni leo, kesho hata siku zote.
.
BE INSPIRED [emoji921]
.
NB:
Ubora ni safari.
.
Screenshot_20220726-042655_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji3578] Scanda 24

FOOTBALL ECONOMY || Heshima Full Tank [emoji921]
.
Nawaona mabrother zangu wanapigana vikumbo, wapo wanaojishusha utu wao, wapo waliovaa vazi la haki na ukweli na wapo wa Bei rahisi.
.
Niwaambie tu, msipambane hata kidogo, pigeni hatua zenu kimahesabu na wala hii sio hesabu rahisi. Geji ya Heshima ipo kwenye FULL, Haishuki ila inashuka na mtu.
.
ILIKUA NI KAZI RAHISI KUZUIA HUKUMU LAKINI SIO RAHISI KUPINDUA HUKUMU. Ninachokiona saa hizi ni kelele za Kufeli na wala sioni nguvu, kungekua na hiyo nguvu ingetumika kuzuia hukumu.
.
Wallace Karia na Shirikisho lake hawawezi kukubali kufa hali ya kuwa ni watu waliodhalilika kwa bei rahisi. Ni heri Makao makuu yavunjike kuliko heshima na Hadhi ya mamlaka kudhihakiwa.
.
NB:
End Of An Era[emoji354]️
Screenshot_20220726-041050_OGInsta%2B.jpg
 
CR7 ANAREJEA ENGLAND
.
[emoji599] | Cristiano Ronaldo yupo njiani kuelekea England kufanya mazungumzo na mabosi wa Manchester United juu ya hatma wake.
.
Kitendo cha Ronaldo kurudi Manchester inaelezwa kuwa ni ishara nzuri na huenda akakipiga OT msimu ujao.
.
Ronaldo anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na kocha Erik Ten Hag katika siku chache zijazo.
Screenshot_20220726-043250_OGInsta%2B.jpg
 
Morrison apangua namba Yanga
.
Heshima ya nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto anayevaa jezi namba tatu imemfanya winga mpya Bernard Morrison kupangua jezi za mastaa wa timu hiyo baada ya kushindwa kupata namba yake pendwa (3) kutoka kwa Mwamnyeto.
.
Imemlazimu Morrison kumvua jezi namba 33 beki wa kushoto, David Bryson. Baada ya kuchukua namba 33, Bryson ameshuka kwa mshambuliaji Yusuph Athuman nakuchukua jezi namba 21 huku Athuman akichukua namba 14 iliyokuwa inavaliwa na Paul Godfrey ‘Boxer’ aliyetimkia Singida Big Stars (SBS).
.
Haikuishia Lazarous Kambole amepewa namba 17 iliyokuwa ikivaliwa na kiungo Balama Mapinduzi, kiungo mpya Gael Bigirimana namba 27 iliyokuwa ya Deus Kaseke. Beki mpya wa kulia Joyce Lomalisa namba 13 iliyokuwa ya kipa Ramadhan Kabwili.
Screenshot_20220726-043402_OGInsta%2B.jpg
 
MAYELE AONGEZA MZUKA KAMBINI
.
Straika wa Yanga, Fiston Mayele jioni ya leo anatarajia kutua jijini Dar na kuelekea kambini kwao Avic, Kigamboni na huko hakuna kucheka ni dozi kali wachezaji wakijifua chini ya makocha wao Cedrick Kaze na Nasreddine Nabi.
Screenshot_20220726-043457_OGInsta%2B.jpg
 
ZORAN: WAWILI BORA ZAIDI WATAANZA
.
“Kuhusu Ouattara uwepo wa mchezaji wa daraja lake ndani ya kikosi chetu ni faida kubwa kwani ana uwezo mzuri wa kucheza beki wa kati na kutimiza majukumu ya kiulinzi,
.
“Faida nyingine ya Ouattara ni kucheza kiungo mkabaji. Ana uwezo mkubwa na hilo kila mmoja atakuja kuliona kwenye michezo ya mashindano ila kuhusu kucheza kikosi cha kwanza hilo sio rahisi kwani Onyango na Henock Inonga nao wapo kwenye ubora.
.
“Ushindani kati yao watatu Ouattara, Inonga na Onyango wawili watakaokuwa bora zaidi katika maandalizi ya mchezo husika watapata nafasi.” - Zoran Maki.
Screenshot_20220726-044831_OGInsta%2B.jpg
 
BASI LA TFF KUKAMATWA
.
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuliamuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulipa deni la Sh 56,446,700, wakili wa Taasisi za Filbert Bayi, Karoli Tarimo amefungua maombi kukazia hukumu akiiomba mahakama iruhusu kulikamata basi la TFF lenye namba za usajili T581 CGR liuzwe ili kulipa deni hilo.
.
Taasisi hiyo inaidai TFF fedha hizo kwa miaka mitatu ambazo kwa mujibu wa Tarimo zilikuwa ni gharama ya kambi kwa timu za vijana chini ya miaka 13, 15, 17 na ile ya wanawake katika taasisi hiyo Kibaha mkoani Pwani.
Screenshot_20220726-045255_OGInsta%2B.jpg
 
EL FIDEO ON FIRE [emoji91] Angel Di Maria tayari anauwasha sana kwenye uzi wa Juventus, bila shaka atakuwa na wakati bora sana ndani ya SERIE A, tayari mechi za kirafiki amekuwa bora sana

Hapa Angel pale ni Paul Pogba [emoji119]
Screenshot_20220726-051156_OGInsta%2B.jpg
 
Cristiano Ronaldo amewasili jijini Manchester tayari kuanza mazungumzo na Kocha Erik Ten Haag, bado haipo wazi kama atasalia au kuondoka ila Kocha anamuhitaji sana Mreno huyo kikosini mwake.
Screenshot_20220726-051308_OGInsta%2B.jpg
 
Hii ni TOKYO, Japan [emoji627] na huyu Jamaa anaitwa Dan Orlowitz ni Mwandishi pia wa michezo huko akiandikia JAPAN TIMES na JT Sports, aliipenda sana jezi ya Yanga na akaulizia namna ya kuipata mtandaoni hatimae akaipata.

Ilibidi aombe msaada kutoka kwa Mwandishi wa Ghana, Nuhu Adams amsaidie namna ya kuipata hii jezi, sio yeye peke yake ni wengi huwa nawaona wanaulizia sana hii jezi kupitia Twitter, alisema anaitaka jezi kwa gharama yoyote imfikie.

Imagine jezi imesafiri maili zaidi ya 7,012 kutoka Dar Es Salaam mpaka Mashariki ya mbali, nimefuatilia pia Yanga jezi zao zinanunuliwa sana Amerika ya Kati na Kusini, watu wanaagiza sana online.

Nafikiri iko haja kwenye App yao waweke option ya kuuza jezi mtandaoni ili iwe rahisi zaidi na zaidi kwao kwakuwa biashara hii inaonekana inapendwa sana duniani, nadhani ni kutokana na rangi zao pia.

Huo ni uzi wa Wananchi kwenye jiji la Tokyo, zipo picha nyingi pia kwenye majiji mengine makubwa! Naaam ni habari nzuri [emoji123]
Screenshot_20220726-051442_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamke aitwae Maria Sakware (49) mkazi wa Kijiji Cha Gabadaw amefariki katika Kituo cha afya Bashnet (Burma) Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara wakati akipatiwa matibabu baada ya kudaiwa kupigwa na Mume wake.

RPC Mkoa wa Manyara ACP Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea 20/7/2022 huku chanzo cha tukio hilo ikiwa ni ulevi kwa mume wa marehemu aitwae Petro Fabiano Basso (38) ambae alimshambulia mke wake kwa fimbo na kumsababishia majeraha mwilini na kumvunja mkono wa kushoto

Rpc Kuzaga amesema mtuhumiwa alimtuhumu marehemu kuwa amechukua pesa yake shilingi elfu 10 ambapo Polisi walipokwenda kumkamata Mtuhumiwa walimkuta amelewa.
Screenshot_20220726-051841_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom