Makapuku Forum

Makapuku Forum

[emoji599] EXCL: Taarifa kutoka kwenye vyanzo vya ndani ya Simba zinasema, straika mpya Cesar Manzoki, huenda akajiunga na kikosi hicho dirisha dogo linalofunguliwa Desemba mwaka huu.
.
Habari za Ndani zinasema, licha ya straika huyo kusainishwa mkataba wa awali, lakini mabosi wake wa zamani, Vipers ya Uganda wameleta ugumu kwa kutaka ilipwe Dola 200,000 (zaidi ya Sh 450 milioni za miezi miwili iliyosalia za mkataba na mchezaji huyo)
.
Inaelezwa Vipers imekomaa mchezaji huyo amebakiza mkataba wa miezi miwili na kama Simba inamtaka basi ilipe fedha hizo, kitu ambacho mabosi wa Msimbazi wameona isiwe tabu, wanamwacha aendelee kukipiga Vipers, kisha wambebe Disemba kama Mchezaji Huru.
Screenshot_20220725-043937_OGInsta%2B.jpg
 
KESSY ATUA DODOMA JIJI
.
Dodoma Jiji haijamaliza usajili, kwani imeendelea kukusanya kijiji kwa kumbeba, Hassan Kessy aliyekuwa KMC.
.
Usajili wa nyota huyu unafanya idadi mpya ya wachezaji wapya kwa timu hiyo kufikia 12 baada ya usajili wa awali wa wachezaji 11, huku idadi ikitarajiwa kuongezeka wakati wowote.
.
Mchezaji huyo anaungana na Daniel Mgore, Jimmy Shoji, Amaan Kyata, Christian Zigah, Collins Opare, Hassan Mwaterema, Paul Peter, Rashid Chambo, Randy Bangala, Mwana Kibuta na Salum Kihimbwa.
Screenshot_20220725-044039_OGInsta%2B.jpg
 
JOYCE: WANAONIBEZA NITAWAJIBU KWA VITENDO
.
Beki wa kushoto kutoka DR Congo, Joyce Lomalisa amesema mashabiki wa wapinzani wao wanalibeza jina lake, lakini atawanyamazisha kwa kazi atakayoionyesha uwanjani, kwani anajua kilichomleta Jangwani.
.
“Hili jina halina shida wanaojua hawawezi kushangaa, lakini nimeambiwa ni watu wa timu pinzani (Simba), waambieni watanyamaza tu kwa kazi nitakayoifanya uwanjani nikiwa na Yanga,” amesema Joyce na kuongeza;
.
“Mimi nimecheza soka sehemu mbalimbali ikiwamo Ulaya na hapa Afrika, sina wasiwasi kabisa watanyamaza tu hao kwa kutumia hii miguu yangu uwanjani.”
Screenshot_20220725-045121_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji599] HATARI INAKUJA !!
.
MANCHESTER City ilimaliza msimu uliopita bila ya kuwa na straika na bado ilitwaa ubingwa ikifunga mabao 99 ambayo ni mengi kuliko timu yoyote ya ligi zote tano kubwa za Ulaya.
.
Na sasa imemsajili Erling Haaland ambaye leo kaweka kambani, ikumbukwe ameifungia Dortmund, mabao 86 katika mechi 89.
Screenshot_20220725-045337_OGInsta%2B.jpg
 
Kuna JITU limekufa 4-0 ..!! Na mbona mko kimya [emoji38]
.
Arsenal katika Pre-season
[emoji736] 4-0 v Chelsea
[emoji736] 3-1 v Orlando
[emoji736] 2-0 v Everton
[emoji736] 5-3 v Nurnberg
.
The GUNNERS ON FIRE [emoji91]
Screenshot_20220725-045440_OGInsta%2B.jpg
 
GUNDU: VIGOGO WOTE ULAYA HAWAMTAKI RONALDO
.
Ndo hivyo, ukichoka watu wanakuchoka zaidi. Supastaa Cristiano Ronaldo na mpango wake wa kuachana na Manchester United dirisha hili unazidi kugonga mwamba baada ya Barcelona nao kutupilia mbali ofa ya kumchukua fowadi huyo.
.
Barca walipelekewa ofa ya kumsajili Ronaldo mapema mwezi huu, lakini mabosi hao wa Nou Camp wamemkataa. Ronaldo amedhamiria kuachana na maisha ya Old Trafford kwenye dirisha hili akikacha kwenda pre-season na wenzake kwa madai ya kuwa na matatizo ya kifamilia.
.
Wakala wake Ronaldo, Jorge Mendes amekuwa akimtoa ofa mchezaji huyo klabu mbalimbali za Ulaya, lakini hakuna hata moja iliyoonyesha dhamira ya kutaka huduma yake.

…………….
Screenshot_20220725-045527_OGInsta%2B.jpg
 
“Kwa namna ambavyo nataka tucheze naona bado kuna wachezaji nawakosa, tutaona cha kufanya kabla dirisha halijafungwa” Mikel Arteta, Kocha wa Arsenal

Yani Chelsea kafa nne wakati huo Arsenal haijakamilika[emoji3]
Screenshot_20220725-045709_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom