Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.
Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri
Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.
View attachment 2302843