Makapuku Forum

Makapuku Forum

NAMUNGO YAIFUATA YANGA KIGAMBONI
.
Kikosi cha Namungo mapema wiki hii kiliamua kuifuata Yanga Kigamboni kwenda kuweka kambi yao huko kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
.
Yanga iliyoanza kambi ya mazoezi Avic Village, ambayo ndio wanayoitumia tangu kampuni ya GSM iingie Jangwani, hivyo ujio wa Namungo unafanya Kigamboni sasa kuwe na timu mbili za Ligi Kuu

…………
Screenshot_20220721-150320_OGInsta%2B.jpg
 
KABUNDA HUYO KATUA NAMUNGO
.
Moja ya wachezaji wenye mbio na chenga za maudhi uwanjani ni Winga wa KMC, Hassan Kabunda ambaye taarifa zinaeleza amejiunga na Namungo kwa mkataba wa miaka miwili.
.
Kiungo huyo alipita timu mbalimbali ikiwemo African Lyon, Ashanti United na Mwadui FC.View attachment 2298721
shangazi huwa napenda namna unavyowasilisha hz habari,una taluma ya uandishi nn
 
[emoji3578] Farhan Jr

Mwalimu wangu aliwahi kuniambia katika michezo yote duniani, basi ni mpira wa miguu ambao umebeba MTAA na MAISHA yetu ya kawaida

Mwalimu aliniambia mpira wa miguu ni mtaa ambao umewekewa mfumo tu, lakini ili mpira wenyewe uwe na mvuto basi unauhitaji mtaa kwenye mpira

Mwalimu aliniambia China wamewekeza sana ila mpira hauna mvuto licha ya kuwa asili yake ni China ila mitaa haiushi mpira kuanzia Beijing, Shanghai hadi Hong Kong, hii ipo mpaka Marekani pia

Kwakuwa mpira ni mtaa, wangapi wamewahi kuwajibu vibaya wazazi wao kwasababu ya mpira?, wangapi wamekosana na mpaka kununiana kisa mpira? Wangapi wamepigana kisa mpira?

Najua ni wengi, basi hii ni kwakuwa mpira ni MTAA na ndio MAISHA yetu halisi! Chochote kinachotokea banda umiza au uwanjani hawi Binadamu wa kawaida unaemfahamu bali kila Mtu kwenye dunia yake

Mungu akinijalia umri mrefu, Mwanangu RIYAD hata kama atanitolea lugha chafu kisa mimi Simba na yeye Yanga basi sitompa adhabu, hata Mke wangu akinimind kisa mimi Chelsea yeye Man United sitomind kwakuwa ni MAISHA halisi

Kwakuwa mpira ni Mtaa uliopewa MFUMO, basi Nikutakie mapumziko mema Kaka @hajismanara bahati mbaya tu uliuishi mtaa kwenye Mfumo, lakini pongezi kwa @tanfootball kwa kusimamia sheria kadri inavyotakiwa

Leo amefungiwa moja ya icon ya mpira wetu, aliyeuishi utamaduni halisi wa mpira kwenye dunia ya mfumo, haikuwa rahisi ila alileta kitu chake kwenye game!

Farhan ni mtafutaji wa kawaida tu kutoka Morogoro ambaye hapendi kuona watafutaji wengine wanapatwa na kadhia, kama nilivyosimama na Kocha Mbwana Makata basi hata kwa Haji pia, MUNGU AWABARIKI[emoji1488]
Screenshot_20220721-143835_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom