Makapuku Forum

Makapuku Forum

Today, we celebrate Africa. [emoji288][emoji93]

#CAFAwards2022 | #AfricanFootball
Screenshot_20220721-164048_OGInsta%2B.jpg
 
Msemaji wa Yanga, Haji Manara ametoa kauli ya kwanza baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutojihusisha na soka kwa miaka miwili ameandika haya;
"Iwe ni jambo la kheri au shari, neno langu kuu ni kumshukuru Muumba mbingu na ardhi Kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana. AL-HAMDULILLAH [emoji1317] Thanks football [emoji122],"
Screenshot_20220721-143835_OGInsta%2B.jpg
 
Kiungo mkabaji wa Simba, Taddeo Lwanga ameonyesha mjengo wake wa gorofa moja aliojenga huko Uganda baada ya kuposti picha kwenye mitandao ya kijamii na kuandika 'Welcome to the Oasis'

Kiungo huyo alisaini Simba Disemba 2020 akiwa kama mchezaji huru kuja kuziba nafasi ya Gerson Fraga ambaye alisitishiwa mkataba wake.

Screenshot_20220721-165032_OGInsta%2B.jpg
 
MASTAA wa Yanga wanatarajia kurejea kambini muda wowote kuanza sasa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya lakini benchi la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi wana siri nzito kwenye mafaili yao.

Kazi ya kwanza ni kuwaimarisha kimbinu, kiufundi na kifiziki wawe tayari kuhimili ushindani lakini pili ni kumaliza sintofahamu ya mikataba yao ya kazi ambayo huenda wakasaini muda mfupi baada ya kuwasili kutegemeana na uharaka wa mazungumzo.

Lakini jambo la tatu kubwa ambalo ni siri kubwa ya Nabi na wasaidizi wake ni kutoa uamuzi wa mpangilio wa kikosi hasa kwa nyota wa kigeni katika msimu ujao kutokana na ujio wa wachezaji wapya.

Tayari wameshachukua uamuzi kumtema Chico Ushindi na kumtoa kwa mkopo Sogne Yacouba, kibarua kigumu ambacho kipo mbele yao kwa sasa ni mkakati wa kupata nyota nane wa kigeni ambao watakuwa tegemeo katika kikosi chao msimu ujao kulingana na matakwa ya kikanuni.

Kwa mujibu wa kanuni ya idadi ya wachezaji wanaopaswa kutumika katika mchezo mmoja, kila timu inaruhusiwa kusajili wachezaji 12 wa kigeni lakini itawatumia wachezaji nane tu katika mchezo mmoja na wanaobakia ni lazima wawe wazawa.
Screenshot_20220721-165156_OGInsta%2B.jpg
 
STRAIKA mpya wa Simba, Habib Kyombo amekabidhiwa majukumu mapya baada ya kupewa jezi namba tatu aliyokuwa anavaa staa wa zamani wa timu hiyo, Bernard Morrison.

Morrison ambaye amejiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao, akiwa na jezi hiyo kwenye kikosi cha Simba, ameonyesha ubora upande wa mashindano ya kimataifa baada ya kupiga pasi nne za mabao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na kuifanya Simba kuingia hatua ya robo fainali msimu uliopita.

Kyombo kwa mara ya kwanza alivaa jezi hiyo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ismaily nchini Mirsi na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Screenshot_20220721-165258_OGInsta%2B.jpg
 
Katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi, watu wawili wanaosadikika kuwa ni wapenzi wameuawa kwa kuchomwa vitu vyenye ncha kali kifuani na tumboni na watu wasiofahamika ndani ya nyumba katika mtaa wa Msangalee jijini Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martine Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanakusanya taarifa hizo ambazo watazitoa baadaye.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ibenzi Ernest alithibitisha kupokelewa kwa miili ya wawili hao ikiwa imechomwa chomwa na vitu vyenye ncha kali.

Screenshot_20220721-165414_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Morogoro, Ngollo Malenya ( wa kwanza kulia) ameagiza kukamatwa kwa wazazi wawili Thomas Ulanda na Adelyda Nakashawa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa madai ya kuwatelekeza watoto wao watatu wanaoishi Kijiji cha Gombe.

Kwa mujibu wa watoto hao wamesema wazazi hao waliachana, mwanamke akaolewa na mwanaume mwingine na baba akaoa mwanamke mwingine na kuwatelekeza watoto kwenye nyumba ambayo inaweza kuanguka muda wowote kutokana.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa wilaya amefanya jitihada za haraka za kuwanusuru watoto hao ikiwa ni pamoja na kumtafuta mdau Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Faru Graphite, John De Vries ambaye amesema atawajengea watoto hao nyumba na kuwahudumia mahitaji yote maalumu ikiwemo kuhakikisha wanasoma.

Screenshot_20220721-165508_OGInsta%2B.jpg
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne leo amefika kwenye eneo la Msewe Golani Wilaya ya Ubungo ambako usiku wa kuamkia leo mida ya saa tisa Vijana walivamia kwenye nyumba kadhaa ikiwemo hosteli za Mama Msangi na kuibia Watu simu, laptop, pesa za kawaida za matumizi na kuvunja vioo vya magari.

"Tumebaini Wahalifu hawa pia walikua wakisema wanalipiza kisasi cha mwenzao kuuawa, sasa tunachunguza mwenzao aliouawa ni nani na alikua anafanya shughuli gani ? kwahiyo pamoja na tukio hili tunachunguza kwa kina kujua ni kitu gani kilichosababisha tukio hili lifanyike, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litafatilia na kushughulika nao vikali kama Wahalifu wengine"

“Kila kilichoibwa katika eneo hili kitapatikana, wito wangu mwingine nimeubaini katika eneo hili la Golani mifumo ya kiusalama ya eneo hili imezorota, ni eneo lenye Vijana wengi nguvu kazi ya kutosha lakini mifumo ikiwemo falsafa ya ulinzi shirikishi eneo hili wameiua, hilo nalo ni jambo ambalo nitafatilia” ——— amesema Kamanda Muliro.
Screenshot_20220721-165635_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF kutangaza kumfungia Msemaji wa Yanga Hajis Manara kwa miaka miwili na faini ya milioni 20 baada ya kumkuta na hatia ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia, Msemaji huyo amesema neno lake moja tu kwa sasa ni Al-Hamdulillah.

“Iwe ni jambo la kheri au shari, neno langu kuu ni kumshukuru Muumba Mbingu na ardhi kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana, AL-HAMDULILLAH [emoji1317], Thanks football [emoji122]” ——— Haji Manara.
Screenshot_20220721-165848_OGInsta%2B.jpg
 
Mwigizaji Farida Sabu maarufu Mama Sonia ambaye alikua Msanii wa Kaole Sanaa Group na kuigiza kwenye maigizo kama Dira, Gharika, na Taswira amefariki Unguja, Zanzibar.

Imeelezwa kwamba Farida alikwenda Zanzibar kuitembelea familia yake akaugua na leo akafariki.

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Chiki Mchoma ameiambia @ayotv_ kwamba msiba upo hukohuko Unguja na Marehemu atazikwa kesho Zanzibar saa saba mchana.

“Bi Farida Bibi Sonia amefariki Zanzibar Unguja, mwezi mmoja uliopita alikwenda kwaajili ya kupumzika na Watoto wake lakini akapatwa na maradhi na leo asubuhi Mungu akamchukua” amesema Chiki Mchoma M/Kiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania. #MillardAyoUPDATES [emoji1545] #RIPFarida
Screenshot_20220721-165955_OGInsta%2B.jpg
 
Mchezaji wa Simba SC. Taddeo Lwanga (28) ambaye ni Raia wa Uganda ameuonesha Mjengo wake alioujenga kwao Uganda kwa lengo la kuwakumbusha Vijana wote kwamba yeyote mwenye bidii anayo nafasi ya kutimiza ndoto zake siku moja na haijalishi itachukua muda gani kuzifikia.

Nyumba hii ya Lwanga ambaye ni Baba wa Watoto wawili ni ya gorofa moja na inapatikana Kajjansi barabara ya kuelekea Entebbe “ni hisia za furaha na zisizoelezeka kumiliki nyumba hii” alisema Lwanga.
Screenshot_20220721-170135_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220721-170149_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220721-170205_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220721-170224_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa ameteua Kamati maalum itakayokuwa na jukumu la kuratibu mdundo wenye asili ya kitanzania ambapo ndani yake kuna Ma-DJ wawili, Producers watatu na Msanii mmoja.

Mwenyekiti wa Kamati hii ambayo imetakiwa kufanya kazi toka jana July 20 2022 ni Dr. Kedmon Mapana ambaye ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo Katibu wa Kamati akiteuliwa kuwa Dr. Herbert Makoye, Mkuu wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo huku Wajumbe wakiwa ni kama ifuatavyo.

DJ JD (John Dilunga Matlou),
DJ Fetty (Fatuma Hassan),
Producer P Funk Majani (Paul Mattysse), Producer Master J (Joachim Kimario), Producer Humphrey Domboka (Wanene), Msanii Mwana FA.

Wengine walioteuliwa ni Chifu wa Mwanza Aron Mikomangwa akiwa ni mzoefu wa midundo ya asili, Mkuu wa Kikundi cha Ngoma cha Taifa Zanzibar Abdallah Othman Abdallah na mwisho ni Mtangazaji Mkongwe Masoud Masoud kutoka TBC.
Screenshot_20220721-170458_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amefanya uteuzi wa Kamati maalum kwa ajili ya kuratibu upatikanaji wa vazi la Taifa ambapo amemteua Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo huku Katibu wa Kamati akiwa ni Dr. Emmanuel Temu ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni.

Wajumbe walioteuliwa ni Chifu Antonia Sangalali akiwawakilisha Machifu, Wabunifu wa mitindo Khadija Mwanamboka na Mustafa Hassanali, Msanii Mrisho Mpoto pamoja na Mtangazaji/Mchora katuni Masoud Ally (Kipanya) ambapo kamati hii imetakiwa kuanza kutekeleza majukumu yake toka jana July 20 2022.
Screenshot_20220721-170550_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom