[emoji3578] Shaffih Dauda
Kuna vitu vingi vinavyosababisha mashabiki wa mpira wetu kuamini wachezaji wa nje ya nchi ni bora kuliko wachezaji wazawa.
1. BRANDING
Kwa miaka ya hivi karibuni kwa kujua au kutokujua, tumekuwa tukiwa-brand wachezaji wa kigeni.
Mchezaji wa kigeni anavyozungumzwa, matarajio na namna ambavyo wanapewa thamani.
2. VILABU
Namna mchezaji wa kigeni anachopewa thamani [anavyolipwa, anapokaa, aina ya usafiri] ni tofauti na mchezaji wa nyumbani.
Kaangalie mchezaji kama Dickson Job analipwa mshahara kiasi gani ukilinganisha na mgeni? Halafu rudi uwanjani angalia kazi zao!
Kuna mtu atasema malipo yanatokana na makubaliano binafsi, wala sipingi lakini anavyosikilizwa mchezaji wa kigeni wakati wa makubaliano ni tofauti na mazawa.
Mchezaji mzawa anaweza kuambiwa kuna kiasi fulani, kama hutaki basi! Yani kuna kuwa kama kuna kiwango cha wachezaji wa zawa hawapaswi kuvuka kiasi fulani.
3. MEDIA
Vyombo vya habari pia vimekuwa vikiwagawa wachezaji kwenye kuwapa thamani.
Anakuja mchezaji wa kigeni namna anavyoeezewa kwenye vyombo vya habari lazima watu washtuke. “Mtambo wa mabao umefika, matatizo yote kwisha.”
Kwa kuwa mashabiki hawajawahi hata kumwona, mzigo wanaotwishwa wakisikia anavyoelezwa kichwani inakuja picha ya Sadio Mane, Didier Drigba, Mo Salah!
Kwa upande wa wazawa huwezi kumpa sifa ambazo hana kwa sababu watu wameshamuona akicheza na wanajua uwezo wake.
Kuna namna vyombo vya habari tunajenga picha kubwa za wachezaji wa geni akilini kwa mashabiki mwisho wa siku wanaona bora timu zisajili wachezaji wa kigeni.
4. CHUKI
Wakati mwingine mashabiki wanaamua tu kutomkubali mchezaji mzawa kwa sababu ya wivu na kuona atafanikiwa au atapata.
Imekuwa kama hulka hivi watu kutokubali mafanikio ya mtu mwingine na hii sio kwenye mpira tu bali hata kwenye maisha yetu ya kila siku.