Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220713-041909_Instagram%20Lite.jpg
 
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20, kiwango cha ubadilishaji fedha kati ya Euro na dola ya Marekani kimekaribiana kwa ukaribu zaidi ikimaanisha kuwa pesa hizo mbili zina thamani sawa.

CNN wameripoti kwamba Euro ilifikia dola moja leo Jumanne ikiwa ni chini ya takriban 12% tangu kuanza kwa mwaka huku hofu ya mdororo wa uchumi ikiongezeka kutokana na kuchochewa na mfumuko wa bei na kutokuwa na uhakika wa usambazaji wa nishati kunakosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Umoja wa Ulaya ambao ulipokea takriban 40% ya gesi yake kupitia mabomba ya Urusi kabla ya vita, unajaribu kupunguza utegemezi wake kwa mafuta na gesi ya Urusi wakati huu ambao pia Urusi imepunguza usambazaji wa gesi kwa baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya ikiwemo kupunguza kwa 60% pia usafirishaji kwenye bomba la Nord Stream linalokwenda Ujerumani.
Screenshot_20220713-044052_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom