Makapuku Forum

Makapuku Forum

Club ya Azam FC leo imemtambulisha golikipa wa Timu ya Taifa ya Comoro Ali Ahamada (30) kuwa Kipa wao mpya, Ali aliwahi kucheza Toulouse ya Ligi Kuu Ufaransa (2011-2016).

Ali Ahamada ni Mfaransa mwenye asili ya Comoro na amewahi kucheza Timu ya Taifa ya Ufaransa U-21 (2011-2012) kabla ya kuamua kurudi Comoro kwenye asili ya wazazi wake.

Azam FC kwa muda mrefu wamekuwa na wakati mgumu katika eneo la magolikipa toka aondoke Aishi Manula na Razack Abarola
Screenshot_20220714-044200_OGInsta%2B.jpg
 
Watu watatu wa familia Moja wamefarikia Dunia mara baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Afrika Mashariki inayopita kata Muriet Mashariki Mkoani Arusha .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa kata hiyo wamesema barabara hiyo imekuwa ikisababisha vifo vya mara kwa mara na hao waliogongwa ni kaka ,dada na mtoto mdogo waliokuwa wametoka Hospitali kumpeleka mtoto kupata matibabu.
Screenshot_20220714-044736_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkazi wa Buhongwa, Omary Lucas (48) kwa tuhuma za kumuua mke wake, Elizabeth Lusana (61) kwa kumkata mapanga kutokana na wivu wa mapenzi.

Akizungumza leo Jumatano na waandishi wa habari leo Julai 13, 2022 jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng'anzi (Pichani) amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Julai 11 mwaka huu baada ya kuibuka ugomvi baina ya wanandoa hao.
Screenshot_20220714-044850_OGInsta%2B.jpg
 
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema baadhi ya maeneo katika baadhi ya mikoa yatakosa umeme leo Jumatano Julai 13, 2022 kutokana na upungufu kwenye mitambo ya uzalishaji umeme.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, upungufu huo umesababisha jumla ya megawati 91 kutokua kwenye mfumo wa usafirishaji umeme hivyo baadhi ya maeneo yatakosa nishati hiyo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 12 jiioni.
Screenshot_20220714-044958_OGInsta%2B.jpg
 
DEAL DONE: [emoji1076] ALI AHAMADA [emoji3591] AZAM FC [emoji838]

Matajiri wa Ligi Kuu, AZAM FC wamethibitisha kukamilisha usajili wa golikipa wa kimataifa wa Comoros [emoji1076], Ali Ahamada kwa mkataba wa miaka mitatu.
Screenshot_20220714-045330_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji1241] NDEMLA [emoji3591] SINGIDA BIG STARS [emoji294]️
.
Klabu ya Singida Big Stars imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo kutoka Simba SC, Said Khamis Ndemla kwa Mkataba wa Miaka miwili.
Screenshot_20220714-050407_OGInsta%2B.jpg
 
KOCHA wa zamani wa Singida United na Yanga, Hans Van der Pluijm ametua nchini leo tayari kwaajii ya kumalizana na matajiri wake wa zamani Singida Big Stars.

Singida imepanda daraja msimu huu na ikiungana na Ihefu ambazo zimepishana na Mbeya Kwanza na Biashara United walioshuka daraja.

Ujio wa Pluijm ndani ya timu hiyo utakuwa ni wa pili baada ya awali kuinoa timu hiyo 2016/17 ilipopanda daraja ingawa sasa imebadilishwa jina ikijulikana kama Singida BigStars.

Pluijm ametua mchana na ndege ya Shirika la Ethiopian Airline huku maafisa waliompokea wakizuia asipigwe picha.
Kocha huyo mwenye uzoefu na Ligi Kuu Bara ana historia kubwa ndani ya Yanga akiwafundisha kwa awamu mbili tofauti tangu mwaka 2014. Katika vipindi hivyo alifanikiwa kunyakuwa mataji mawili ya Ligi Kuu, moja la FA na kufanikiwa kuipeleka Yanga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho mwaka 2016.
Screenshot_20220714-050607_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Simba baada la leo kumtambulisha kiungo mshambuliaji, Augustine Okra sasa ipo mbioni kuwatambulisha wachezaji wengine watatu kuendelea kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa 2022/23 akiwa beki mmoja, kiungo na mshambuliaji.

• Lobi Manzoki-Vipers, Uganga
• Nelson Esor Okwa-River United, Nigeria
• Mohamed Ouattar-Al Hilal, Sudan.
Screenshot_20220714-050710_OGInsta%2B.jpg
 
ALIYEKUWA mshambuliaji wa Kagera Sugar, Peter Mwalyanzi yuko mbioni kujiunga na Ihefu iliyopanda Ligi Kuu.
Juzi Kagera Sugar ilitangaza kuachana na mchezaji huyo aliyewahi kucheza Simba na Mbeya City.

Rafiki yake wa karibu ameiambia Mwanaspoti kuwa tayari kashapokea ofa zaidi ya tatu kutoka timu tofauti za Ligi kuu ikiwemo Ihefu.

"Ihefu ina nafasi kubwa ya kupata huduma yake," amesema rafiki huyo aliyeomba jina lake kuhifadhiwa.
Mwanaspoti lilipomtafuta Mwalyanzi amethibitisha uwepo wa timu nyingi zinazomuhitaji akisema mambo yakikaa sawa ataweka wazi.
Screenshot_20220714-050818_OGInsta%2B.jpg
 
Mabingwa wa Ligi Kuu NBC kwa msimu wa 2021/ 22, Yanga muda wowote watakata kiu ya mashabiki wao ambao wanasubiri kwa hamu utambulisho wa staa anayetajwa sana kutua klabuni hapo Stephane Aziz Ki.

Kiungo huyo atakuwa wa tano kutambulishwa na mabingwa hao baada ya Bernard Morrison, Gael Bigirimana, Lazarous Kambole na Joyce Lomalisa.

Screenshot_20220714-051043_OGInsta%2B.jpg
 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva baada ya kushinda kesi yake dhidi ya klabu aliyokuwa anachezea ya Wydad Casablanca amesema hata ikitokea ofa yeyote ya Morocco haitaki.

"Morocco kwa kweli nisiseme uongo staki hata kupaskia kwenye maisha yangu, kwanza staki kuskia meno Morocco hata ikitokea safari yeyote niende Morocco siwezi kwenda kwasababu sipapendi ni nchi nzuri lakini sababu ya mtu mmoja amefanya nisiipende ile nchi". amesema msuva.
Screenshot_20220714-051920_OGInsta%2B.jpg
 
KIUNGO nyota wa Yanga, Aboubakar Salum Jr ‘Sure Boy’ amesema kwa aina ya mastaa waliotua Yanga mpaka sasa msimu ujao utakuwa balaa.
Staa huyo wa Taifa Stars, amekiri kwamba atahitaji kufanya kazi ya ziada kutetea namba yake lakini anaamini timu hiyo itafanya vizuri zaidi kwenye mashindano yote kuliko misimu iliyopita wakianza na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Agosti 13.
“Sina hofu yoyote kwa ujio wa mastaa hao zaidi unanipa morali ya kupambana zaidi, uwezo nilionao ukichanganya na uzoefu wa Ligi sina sababu ya kuhofia usajili unaoendelea, nina imani na kipaji changu,” alisema na kuongeza;
“Naheshimu sajili zote, naamini utakuwa chachu ya kufanya vyema na bora kwetu. Kuhusu kucheza, kila mmoja ana umuhimu wake kwa nafasi yake. Nina uhakika wa kucheza najiamini nina kipaji, nimetoka Azam FC vikosi vingi vilipangwa wakiniondoa lakini nimetua nimecheza,” alisema.
Screenshot_20220714-053606_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano binafsi ya kumsajili beki wa Napili, Kalidou Koulibaly kuja kuziba pengo la Antonio Rudiger aliyetimkia Real Madrid.
Chelsea kwa sasa inajiandaa kuwasilisha ofa ya Euro 38million kwa Napoli ili kupata saini ya beki huyo baada ya ofa ya kwanza ya Euro 35million kukataliwa.

Screenshot_20220714-053658_OGInsta%2B.jpg
 
Straika Mnigeria, Nelson Okwa ambaye ameliambia Mwanaspoti kwamba atatua Dar es es Salaam punde akiwa tayari kukiwasha Msimbazi kwani kwa sasa kuna ishu kidogo tu za kukamilisha.
Kumbuka kuna mashine nyingine mpya ambazo ni Moses Phiri, Habibu Kyombo, Kapama, Victor Akpan ambao wameshatangazwa. Mohamed Outtara, Cesar Manzoki, Nelson Okwa na Augustine Okrah watafuata muda wowote kuanzia leo.

Mwanaspoti limeelezwa usajili wa Okwa uliwagharimu Simba Sh140 milioni kwavile bado alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Rivers United ya Nigeria.

Alipotafutwa Okwa alisema zaidi ya asilimia 80, kila kitu amekubaliana na Simba ila kilichobakia ni mambo mawili malipo ya timu pamoja na yeye binafsi kisha atawasili nchini kukiwasha.
Screenshot_20220714-053811_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

MTAKATIFU AUGUSTINE OKRAH MAGIC [emoji881][emoji837]

SHILLING 10 YA MAAJABU

Alipokea simu ya Simba baada ya kusikia kuna uhaba wa virutubisho vya kiburudani, watu wana utapiamlo wa soka uliotokana na kukosa soka safi

Ugonjwa ambao umepelekea watu kutofika uwanjani kwa wingi, ugonjwa ambao umefanya watu wachukie wachezaji bila sababu za msingi

Ukisoma OKRAH 10 inasema “Na atakapoitwa na watu wa nchi ile wakihitaji huduma yake, nae ataitika na kutangazwa ujio wake mchana kweupe, hakika wamepata tiba sahihi watu wale”
Screenshot_20220714-054027_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji599]| Wakala wa Frankie De Jong amewaambia Barcelona kuwa mteja wake hana mpango wa kuondoka Camp Nou na hayupo tayari kukatwa mshahara wake.

Hii ni taarifa mbaya kwa Manchester United wanaowinda saini yake.
Screenshot_20220714-054136_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji3578] Shaffih Dauda

Kama mnaweza kufanya sajili kubwa na nzuri nyote Simba na Yanga, kama mnaweza kupambana kwenye ubunifu wa kutambulisha wachezaji, kwanini nyote mnafeli kwenye kitu kidogo sana?

Wachezaji wenu wapya mnawatambulisha kwa jezi za msimu uliopita, mnafeli kuwa hata na copy za jezi mpya ili muwatambulishe? Mnakwama wapi kuandaa jezi za msimu mpya mapema?

Vitu vidogo vidogo sana ambavyo mnapaswa kuvirekebisha kuonesha ukubwa

Coastal Union wameanza kutoa darasa la bure kabisa, wametoa mapema jezi mpya na wachezaji wao wamesaini wakiwa na jezi mpya

Vitu vidogo sana ila vina-matter sana
Screenshot_20220714-041714_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom