Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanaume mmoja kutoka Pakistani ambaye Polisi hawajataja jina lake ameripotiwa kuchoma moto kaburi la Mama Mkwe wake aliyefariki miaka 25 iliyopita huko Layyah, jimbo la Punjab.

Mwanaume huyo alilimwagia petroli kaburi hilo na kutishia kutuma picha za eneo hilo kwa Mke wake wa zamani, suala hilo lilikuja baada ya Mke wake wa zamani ambaye walipeana talaka miaka 10 iliyopita kutaka kuolewa tena, jambo ambalo alikataa.

Shemeji yake ambaye amefungua kesi amesema Mwanaume huyo alichoma kaburi hilo baada ya kukasirishwa na kukataliwa na Mke wake wa zamani “Kwakuwa Dada yangu amemkataa na amepata taarifa za kuolewa kwake ameamua kuchoma kaburi la Mama yetu”

Msemaji wa polisi amesema kaburi hilo limepatikana likiwa na dalili za kuchomwa moto, na Mtu huyo amekamatwa na atafikishwa Mahakamani.
Screenshot_20220620-043527_OGInsta%2B.jpg
 
Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne kesho Jumatatu Juni 20,2022 watafikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusikiliza tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo uhujumu uchumi.

Kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2022 inasikilizwa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha na mawakili wanne kutoka upande wa jamhuri ambao ni Tumain Kweka, Khalili Nuda, Verediana Mteuza na Suzy Kimaro.

Juni 7, 2022 hakimu Mshasha aliahirisha kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo Sabaya na wenzake walirudishwa katika gereza la Karanga.
Screenshot_20220620-043645_OGInsta%2B.jpg
 
SIKU ya leo itabaki kuwa kumbukumbu kwa kiungo wa Simba Rally Bwalya baada ya kuagwa rasmi kwa Wekundu wa Msimbazi hao huku akisindikizwa na ushindi wa mabao 3-1.

Ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa na nje ya kuwa mechi ya ligi lakini Simba imeitumia kumuaga kiungo wake huyo iliyemuuza Amazulu FC ya Afrika Kusini.

Bwalya alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Power Dynamos ya Zambia na katika kipindi alichokaa kikosini hapo amekuwa akicheza eneo la kiungo na kuisaidi kushinda makombe ikiwemo la Ligi Kuu msimu uliopita.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha alama 57 katika nafasi ya pili kwenye msimamo huku KMC ikibaki na pointi zake 32 nafasi ya 10.
Screenshot_20220620-043741_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Chelsea imeingia sokoni kusaka saini ya winga wa Manchester City, Raheem Sterling ikiweka mezani dau la Euro 43million kunasa saini ya mchezaji huyo raia wa Uingereza.

Chelsea inataka kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa 2022/23 baada ya msimu ulioisha ikimaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi nyuma ya Manchester City na Liverpool.
Screenshot_20220620-043839_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imetenga Sh4 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kudumu ya Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu jijini Arusha.
Screenshot_20220620-043956_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji amesema Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Mwinyi wanapaswa kukumbuka umuhimu wa Katiba Mpya kwa kuwa Tanzania inahitaji mchakato huo uanze hivi sasa.

Pia, katika mazungumzo yake na viongozi hao, Duni maarufu Babu Duni amewaambia kuhusu kupatikana tume huru ya uchaguzi itayosimamia kura ya maoni ya Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa Duni, alifikisha ujumbe alipokutana na viongozi hao wakuu wa Tanzania na Zanzibar kwa nyakati tofauti akianza na Dk Mwinyi aliyekutana naye Aprili 25,2022 kisha akaonana na Rais Samia Mei 5,2022.
Screenshot_20220620-044105_OGInsta%2B.jpg
 
CAFU: EPL DHAIFU, LALIGA BORA
.
"Ninaogopa, kadiri Wabrazili wanavyozidi kuhamia kwenye Ligi Kuu England, ndivyo inavyokuwa vigumu Brazil kushinda Kombe la Dunia. Hebu fikiria sifa za uongo zinazofanywa na vyombo vya habari kila wiki kukupamba kwamba wewe ni bora zaidi duniani, wakati huo huo hauko hata katika ubora wenyewe.
.
Ninapendelea La Liga, kwa sababu wana upeo mkubwa wa namna ya kufika fainali na kushinda. Huko La Liga hawana kelele sana za Vyombo vya habari kutoa sifa za uongo kuhusu wachezaji wa Kihispania au kuwauza ulimwengu. Wanazungumzia mpira wa miguu hapo, sio bla bla.
.
Niliwasikia wakisema kuwa beki wa kulia wa Liverpool yuko katika kiwango changu cha zamani. Sikutaka kufanya mjadala juu ya hilo kwa sababu nilijua Vinicius ataionyesha Dunia ukweli na alifanya hivyo Paris. ”
Screenshot_20220620-044226_OGInsta%2B.jpg
 
MANULA FRESHI MIWILI TENA !!
.
Klabu ya Simba imefanikiwa kumalizana na kipa wao namba moja, Aishi Manula ambaye alikuwa amewekewa mpunga mrefu na mabosi wa Azam FC.
.
Juzi usiku tajiri wa Simba, Mo Dewji alipitisha bajeti hiyo haraka na kumfanya Manula kukubali dili hilo la miaka miwili mipya abaki klabuni.
Screenshot_20220620-045004_OGInsta%2B.jpg
 
DUH!! RONALDO ANATAKA KUONDOKA
.
Kazi ipo. Kuna watu watalia kama sio kununa. Kinachoelezwa ni staa wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno [emoji1201] Christiano Ronaldo anataka kuondoka Old Trafford.
.
Mbali ya kutojiona kwenye mipango ya Ten Hag sababu nyingine inayofanya Ronaldo atamani kuondoka ni kitendo cha timu hiyo kushindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao na badala yake kucheza Europa League.
.
Timu inayopewa nafasi kubwa zaidi kwa sasa ni Roma kwa sababu ya uwepo wa Jose Mourinho ambaye naye yupo chini ya wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes.
Screenshot_20220620-045121_OGInsta%2B.jpg
 
Malengo yako binafsi yalikuwa ni kusalia kwenye jezi nyeupe na nyekundu lakini malengo ya timu isingekuwa rahisi kuiacha ofa kubwa ya Amazulu

Mtumishi bora ni yule anayeheshimu malengo ya taasisi, ukaheshimu malengo ya timu na kukubali kwenda Afrika Kusini, ndio sifa ya Mtumishi bora

All the best RB, all the best for the future Maestro
Screenshot_20220620-045434_OGInsta%2B.jpg
 
CAPTAIN SULEIMAN ABDALLAH MATOLA ‘VERON’

Attacking football[emoji119] ananikumbusha ile Lipuli pale Iringa, mazoezini anakwambia kila Mtu acheze
Screenshot_20220620-045557_OGInsta%2B.jpg
 
Unaenda kwa CR7 ambaye unafahamu anahitaji Mwanamke bora kwa watoto wake watatu ambao amewapata kwa Mama wawili tofauti, Georgina hakuwa na shaka

Unaenda kwa CR7 ambaye ana Dada wawili wenye gubu, ndio Mawifi fulani wa Kireno wenye Uafrika ndani yao[emoji3] Elma na Katia, inasemekana wadada wengi walishindwa kuendana nao

Lakini Binti huyu hakujali hilo alijiapiza kuwa hiyo ndio nafasi pekee ya binti kutoka Jaca, kaskazini mwa Hispania aliyekuwa na maisha magumu sana

CR7 kwao ni mtoto wa mwisho, Mama yake Maria anamtazama yeye kama kidonda, Dada zake wote na Kaka yake Hugo wote wanampenda sana, ndio maana wamekuwa wakiamua sana kuhusu nani awe na CR7

Gio hakufanya makosa, picha linaanza Cristiano Jr ni kama Mtoto wa kumzaa, tumia muda wako kaperuzi page yake picha nyingi amembeba Mateo au Eva na sio mwanae wa kumzaa Alana Martina[emoji3]

Hizo code ni hatari mno! Mama anapenda zaidi watoto ambao hajawazaa, ndio namna unawin game! Picha nyingi Ronaldo au Cristiano Jr ndio wapo na Alana (Bint yake wa kumzaa) yeye yupo na Wanae wa kufikia

Ndicho familia ya Ronaldo ilikuwa inahitaji, Mama wa familia zaidi! Bibie huyu kwasasa ndie kipenzi cha familia ya Ronaldo, wanacomment sana kwenye page yake na wamemkubali sana

Gio ana Dada yake anaitwa Ivana, wote mwendo ni ule ule, nafasi kubwa wamewapa watoto wa kufikia[emoji3] wanawapenda sana watoto wa CR7!

Ivana anampenda sana Mume wa Mdogo wake, mara nyingi amekuwa akimpost CR7, Ronaldo huwa hana tabia ya kula bata sana na watu tofauti na Ndugu zake na Masela zake ila kwa familia ya Gio imekuwa tofauti, kawapa nafasi kubwa

Hakuwahi mvalisha bint pete rasmi ya uchumba ila kwa Gio ameweza na ni wachumba rasmi!

Maisha yanataka nini tena kwa Gio?? [emoji3]
Screenshot_20220620-045812_OGInsta%2B.jpg
 
Barcelona wana makubaliano na wakala wa Raphina tangu mwezi Februari kuinasa saini ya fundi huyo kwa kandarasi ya miaka mitano

Changamoto iliyopo ni dau ambalo Leeds United wameliweka, wanahitaji kiasi cha Euro million 55 na hawana mpango wa kushusha, huku Arsenal wakiingia rasmi kwenye mbio za kumuwania
Screenshot_20220620-045915_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom