Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 30 au faini ya Tsh. Millioni 347.872 Mkulima Mkazi wa Idodi, Bryton Kaundama (54) kwa kosa la kukutwa na pembe za ndovu zilizokuwa na thamani ya Tsh. Million 34. 7 ambazo alikuwa akiziuza huku akijua kuwa hiyo ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mtuhumiwa alikamatwa Tareh 29/01/2021 ambapo Askari wa Hifadhi ya Ruaha walipata taarifa kutoka kwa Wasamari wema kwamba Mzee Kaundama anauza pembe hizo na wakaweka mtego wa kumkamata kwa kujifanya Kama Wateja wanaotaka kununua nyara hizo.

Baada ya Kukubaliana walikutana Eneo la Kidamali huku mzee Kaundama akiwa amebeba mfuko aina ya Shangazi kaja na pembe hizo zikiwa ndani yake na Kisha akakamatwa.

Mtuhumiwa aliomba kupunguziwa adhabu hiyo kwasababu ni kosa lake la kwanza lakini pia ana Familia kubwa ya Watoto 10 ambao wote wanamtegemea lakini hata hivyo Mahakama ikamuhumu kifungo cha miaka 30 au faini ya Shilingi Million 347.872.
Screenshot_20220619-035627_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Rwanda limesema kuwa Mwanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyebeba bunduki aina ya AK-47 amevuka mpaka na kuingia Rwanda kisha akaanza kuwafyatulia risasi Polisi wa Rwanda, kabla ya Mwanajeshi huyo kupigwa risasi na kuuawa.

Tangazo hilo limesema Polisi wawili wa Rwanda walijeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea kwenye kivuko kidogo cha mpakani kijulikanacho kama Petite Barriere.

Msemaji wa Serikali ya Congo amethibitisha tukio hilo lakini hakutoa maelezo zaidi.

Wakati huohuo duru kutoka mashariki mwa Congo zimearifu kuwa Waasi wa M23 wameudhibiti mji mwingine wa Tshengerero ulio mashariki mwa Bunagan ambao ni mji wa kimkakati kwenye mpaka kati ya Congo na Uganda, ambao uliangukia mikononi mwa M23 mapema wiki hii.
Screenshot_20220619-035810_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya Urusi imemhukumu Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani, Marc Fogel, kifungo cha miaka 14 jela kwa kosa la ulanguzi wa bangi.

Marc alikuwa akifanya kazi katika Ubalozi wa Marekani nchini Urusi lakini hadi anakamatwa alikuwa ameajiriwa kama Mwalimu wa Kiingereza katika Jiji la Moscow, Urusi.

Bangi ni halali katika maeneo mengi ya Marekani lakini bado ni haramu nchini Urusi ambapo Marc Fogel amekutwa na hatia ya usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa pamoja na uhifadhi mkubwa haramu wa dawa bila malengo ya kibiashara.

Fogel, ambaye ana umri wa miaka 60, alikuwa na takriban gramu 17 za bangi kwenye mzigo wake aliponaswa tarehe 15 Agosti 2021 kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo.
Screenshot_20220619-040005_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Tshisekedi ameituhumu Rwanda kuendesha vita ya kiuchumi na kujaribu kuinyakua ardhi ya Congo ili kujipatia rasimali kubwa ya madini, wanaripoti @dw_kiswahili.

Shirika la Habari la Associated Press limemnukuu Rais Tshisekedi akisema hali ya usalama mashariki mwa Congo inaendelea kuzorota kwa sababu Rwanda inajaribu kudhibiti sehemu ya ardhi ya Congo yenye utajiri wa madini ya dhahabu na kobalti kwa manufaa yake.

Tshisekedi amesema kinachoendelea ni vita ya kiuchumi ya kuwania rasilimali na Rwanda inayatumia magenge yake ya kigaidi, bado hakuna majibu yoyote kutoka nchini Rwanda kuhusiana na matamshi hayo ya Tshisekedi, ingawa Rwanda mara kadhaa imekanusha madai ya kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao waliukamata mji muhimu mashiriki mwa Congo mapema wiki hii.

Rais Tshisekedi amewataka Viongozi wa Kimataifa ikiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza kuikosoa Rwanda bila kificho pindi watakapohudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola baadae wiki ijayo mjini Kigali “Raia wa mashariki mwa DRC hawana hatia lakini wanashambuliwa na jirani yetu"
Screenshot_20220619-040116_OGInsta%2B.jpg
 
MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, George Mpole amewataka Watanzania kuthamini wachezaji wazawa tofauti na wanavyowachukulia.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, Mpole alisema licha ya wao kutozungumzwa sana ila wanafanya kazi kubwa ingawa hawapewi sifa kama ambavyo wageni wamekuwa wakiimbwa kila siku.

“Watanzania wanapaswa kujifunza kuthamini vya kwao sina maana wageni hawafanyi mambo makubwa ila mzani ni lazima ubalansi licha ya ukweli wenyewe tunajifunza kutoka kwao,” alisema na kuongeza;

“Siongei kwangu binafsi ila ni kwa wazawa wote, wapo ambao wanaonyesha uwezo mkubwa kuliko hata hao wageni ila kwa bahati mbaya tunawasahau na kuthamini vya nje jambo tunalopaswa kubadilika".
Screenshot_20220619-040231_OGInsta%2B.jpg
 
TEN HAG: KAMA GREENWOOD HANA HATIA ATACHEZA
.
[emoji981] Kocha mpya wa Manchester United, Erick ten Hag amefunguka juu ya Mason Greenwood: “Hebu tusubiri hukumu, kama ataonekana kuwa hana hatia atapata nafasi katika timu yangu, yeye ana kipaji cha kipekee na anaweza kucheza kwenye winga ya kushoto, winga ya kulia, katikati mbele na hata namba tisa ya uongo.”
Screenshot_20220619-040705_OGInsta%2B.jpg
 
JOYCE WA YANGA ATUA DAR [emoji929]
.
Beki wa kushoto mashine mpya ya Yanga, Joyce Lomarisa Mutambala ametua leo Jumamosi nchini akitokea DR Congo [emoji1078] tayari kuitumikia timu hiyo. Kabla ya kujiunga na Yanga, Joyce amewahi pia kuichezea AS Vita na Sagrada Esperanca ya Angola.
Screenshot_20220619-040918_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji599] YANGA REKODI ZA KIBABE
.
Hadi inafikia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Yanga imecheza mechi 34 mfululizo bila ya kupoteza (27 za msimu huu na 7 za msimu uliopita). Rekodi ya kucheza mechi nyingi mfululizo bila ya kupoteza inashikiliwa na Azam FC (mechi 38).
Screenshot_20220619-041107_OGInsta%2B.jpg
 
[emoji1241] | MKANDALA [emoji776] AZAM FC [emoji838]
.
Siku chache baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kiungo fundi wa mpira wa Dodoma Jiji, Cleophas Mkandala [emoji1241] alikuwa kwenye rada za Simba, hali imebadilika baada ya fundi huyo kutua Azam ili kwenda kuliziba pengo la Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyepo Yanga kwa sasa.
.
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu wa Mkandala zinasema kuwa, kiungo huyo na mabosi wa Azam wameshamalizana na kinachosubiriwa ni kumalizika kwa Ligi Kuu Bara ili atambulishwe rasmi.
Screenshot_20220619-041206_OGInsta%2B.jpg
 
CESAR MANZOKI ATAWALA UGANDA

Straika wa Vipers anaehusishwa kujiunga na Simba amebeba tuzo za kutosha usiku wa jana

-Mchezaji bora wa msimu
-Mchezaji bora wa wachezaji
-Mshambuliaji wa msimu
-Mfungaji bora wa msimu
-Kikosi bora cha msimu

What a player
Screenshot_20220619-042437_OGInsta%2B.jpg
 
Ni mchezaji mzuri tu Victor Akpan, alikuwa na ofa nchini Afrika Kusini na moja Kaskazini, ndani ya nchi ni Simba na Azam walipigana vikumbo

Great signing, nafahamu wangeenda nje wangelipa zaidi ya hiyo dola 40,000 kwa quality kama hii hii, ni mchezaji mzuri unless watu hawajamfuatilia

Simba wamepata kiungo mzuri, kilichobaki ni pitch
Screenshot_20220619-042626_OGInsta%2B.jpg
 
YANNICK BANGALA & DJUMA SHABAAN UPDATES [emoji599]

- Nyota wawili raia wa Kongo, Djuma Shabaan na Yannick Bangala walisaini kandarasi ya miaka miwili kila mmoja kuitumikia Yanga

- Kutokana na viwango bora walivyoonesha, Yanga wanataka kuwaongeza tena miaka miwili ili jumla iwe mitatu

- Wakala wao atawasili nchini mchana wa leo na atakuwepo Dar Es Salaam kwa muda wa siku mbili ili kukamilisha mazungumzo hayo kama yatakwenda sawa watasaini

- Mazungumzo pia na Golikipa Djigui Diarra na baadhi ya nyota wengine yanaendelea ili wahudumu Jangwani kwa muda mrefu kidogo

Screenshot_20220619-042907_OGInsta%2B.jpg
 
And i can now confirm that Stephen Aziz Ki is GREEN AND YELLOW, the famous YOUNG AFRICANS

After proving beyond reasonable doubt, a contract of two years signed and sealed [emoji736]

Welcome to Tanzania, Magician [emoji617]
Screenshot_20220619-043016_OGInsta%2B.jpg
 
CLEOPHACE MKANDALA [emoji3591] AZAM FC IS A DONE DEAL [emoji736]

I can now confirm that;

- Kiungo Cleophace Mkandala anaehudumu Dodoma Jiji amekamilisha dili lake la kujiunga na Azam FC ya Dar Es Salaam

- Mkandala anajiunga kama Free agent mwishoni mwa msimu huu kutokana na kwamba tayari anamalizia mkataba wake na walima zabibu

-Kwa mujibu wa vyanzo vyangu ni kuwa amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kwa ada inayokadiriwa kuanzia million 28

All the best Maestro, one of the best ballers in the country!
Screenshot_20220619-043115_OGInsta%2B.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

[emoji344] Inasemekana kuwa Victor Akpan amemalizana na Simba kwa ajili ya kuitumikia klabu yao msimu ujao, ngoja nikwambie kitu, Victor Akpan ni defensive midfielder ( kiungo mzuiaji ) lakini kitu cha ziada kwake ni uwezo wake wa kupiga pasi za mbele anapohitajika kufanya hivyo.

[emoji344] Twende kwa viungo waliopo Simba, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin wote ni box to box midfielders kwa maana ya viungo wanaocheza baina ya maboksi mawili, viungo wanaocheza katika patterns zote za kulinda na kushambulia ( defensive & offensive patterns ).

[emoji344] Jonas Mkude ni holding midfielder, si mzuri sana katika kukaba 1 v 1, ni nadra sana kumuona Mkude anapiga slide tackling, yeye anaweza kuutunza mpira, kupiga pasi na kuzuia eneo ( zonal marking ), kuna utofauti wa kuzuia mtu na eneo, si kama Jonas hawezi kukaba kabisa, anaweza lakini si kama anavyofanya Thadeo au Akpan.

[emoji344] Kwanini Thadeo na Akpan, hawa wote ni defensive midfielders, wanafikiria zaidi kukaba, wanafikiria zaidi kuwalinda mabeki wa kati, utawaona kwenye matukio mengi ya kugongana kwa sababu ya aina yao ya mchezo na majukumu yao ndani ya kiwanja, kwa bahati mbaya Thadeo hajarudi katika form yake kutokana na majeraha.

[emoji344] Kama Simba wameamua kumsajili Akpan ni mchezaji mzuri ingawa bado wanahitaji kuifikiri tena nafasi hiyo, bado nawaona wakihitaji kuliongezea nguvu eneo lao la kiungo wa chini, ukiwa na viungo wawili wakabaji aina ya Akpan jumlisha na Mkude ambae anaweza kutumika kama holding hiyo ni bima kwao.

[emoji344] Msimu huu wamelazimika kumtumia Sadio kama kiungo wa chini kutokana na kukosekana kwa Mkude na Thadeo, vipi kama wangekuwa na mtu mwengine wa kuziba nafasi zao? nalisema hili kwa sababu pia sioni Simba wakiendelea kudumu na Thadeo Lwanga hiyo maana yake watakuwa na Akpan pekee ambae ana sanaa kubwa ya uzuiaji.

Nb: Tusimchukulie kwa wepesi kwa sababu Akpan anatoka Costal Union, tuangalie quality ya mchezaji, Kagere alitoka Kenya, Luis alitoka Msumbiji na wachezaji wengi walioibeba Simba wametoka katika ligi dhaifu kuliko sisi, huo ni mfano tu, usiangalie nani anatoka wapi, angalia quality.
Screenshot_20220619-042626_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom