Makapuku Forum

Makapuku Forum

Asubutuu huyo ndiyo anapendwa sasa

Na huyo 'anayeonewa huruma' ndiyo ana afadhali

Kwanza hata kina 'Ruge' ndiyo huwa wanatoa hela lakini wanaopendwa ni wale kina 'Bill Nass' ambao hawatoi chochote tena ndiyo kwanza wanapewa [emoji16][emoji16]
Huyo Ruge na bil nas ndio maex zako au ndio wa sasa hivi?
Inamaana yule andunje mwenye kichwa kama kibaraza mshaachana?
 
Raia wa kawaida na Wanajeshi wa Taiwan wameendelea kushiriki mazoezi ya kijeshi na kutumia silaha ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kujilinda dhidi ya tishio la vita kufuatia mgogoro unaoendelea kati ya China na Taiwan ambayo inaungwa mkono na Marekani.

Wiki chache zilizopita Rais wa Marekani Joe Biden aliionya China kuhusu Taiwan lakini China kupitia kwa Waziri wake wa Ulinzi, Jenerali Wei Fenghe ikapingana vikali na Marekani “Naomba niweke wazi hili ikiwa kuna Mtu atathubutu kuitenga Taiwan kutoka China, hatutasita kupigana, tutapigana kwa gharama yoyote na tutapigana hadi mwisho, hili ni chaguo pekee kwa China,"

Rais wa Marekani Joe Biden ameiambia China kwamba inachezea hatari kwa kurusha ndege zake za kivita karibu na Taiwan na akaapa kuwa Marekani itakilinda Kisiwa cha Taiwan kijeshi iwapo kitashambuliwa.

Taiwan, ambayo inajiona kuwa Taifa huru, imedaiwa kwa muda mrefu na Uchina ambayo inaamini Taiwan ni Kisiwa chake lakini Taiwan pia inaihesabu Marekani kama Mshirika wake mkubwa, na Marekani ina sheria inayoitaka kusaidia kisiwa hicho kujilinda.

Kuongezeka kwa matamshi hayo kunakuja wakati China inazidi kutuma ndege za kivita katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan zikiruka safu yao kubwa zaidi ya mwaka mwezi uliopita tu wakati Amerika imetuma meli za wanamaji kupitia maji ya Taiwan.
Screenshot_20220619-034245_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya juu zaidi nchini Nigeria imetoa uamuzi wa kuwaruhusu Wanafunzi wa kike wanafunzi wavae Hijab bila kusumbuliwa au kubaguliwa.

Serikali ya jimbo la Lagos ilikuwa imepiga marufuku matumizi ya Hijab ikidai kuwa sio sehemu ya sare za Shule zilizoidhinishwa za Wanafunzi.

Marufuku hiyo ilipingwa na wanafunzi Waislamu mwaka 2015, waliosema kuwa marufuku hiyo inakiuka haki zao za mawazo, za kidini na za elimu, mvutano wa kisheria kuhusiana na marufuku hiyo umedumu kwa muda wa miaka saba.

Uamuzi wa Mahakama hiyo ya juu zaidi nchini Nigeria hatimaye unaweza kumaliza utata huo uliowaathiri zaidi Wanafunzi katika Shule zisizo za kidini nchini Nigeria ambapo Mahakama imesema kuzuai Hijab ni kuwabagua Wanafunzi Waislamu.
Screenshot_20220619-035252_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin katika hotuba yake aliyoitoa katika mkutano wa kimataifa wa Uchumi mjini St Petersburg, amesema uamuzi wa Urusi wa kuanzisha kile alichokiita operesheni maalumu nchini Ukraine ulikuwa mgumu lakini walilazimishwa kufanya hivyo.

Putin amesema operesheni hiyo ililenga kuwalinda Warusi na Watu wa Donbas, mashariki mwa Ukraine, huku akiendelea kurejelea madai kwamba walikuwa wanakabiliwa na mauaji ya kimbari

Putin amesema ‘’Nchi za Magharibi zinaendelea kuisukumia Ukraine silaha na kuchochea vita lakini malengo yote ya operesheni maalumu yatafikiwa bila wasiwasi"
Screenshot_20220619-035353_OGInsta%2B.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema Walimu wote Tanzania wapo tayari kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi ili kuitikia wito wa Rais Samia kwa vitendo ambapo amesema wanatumia mbinu ya kuwatumia Wanafunzi kama Jeshi la kufikisha ujumbe kwa Wazazi wao kuhusu sensa.

“Sio sisi Walimu tu hadi Jeshi letu lote yaani Wanafunzi wapo tayari na tunaendelea kuwakumbusha mara kwa mara kupeleka ujumbe kwa Wazazi wao, kwa njia hii kila Familia au Kaya itapata ujumbe na kwenda kuhesabiwa”

Sensa inatarajiwa kufanyika Jumanne August 23,2022 na mara kadhaa Rais Samia amekuwa akiwakumbusha Watanzania kujitokeza siku hiyo kuhesabiwa ili kuisaidia Serikali kupanga vyema mipango yake ya maendeleo “Hili sio jambo geni kwa hiyo ni muhimu na tujitahidi kukamilisha mipango hii kwa manufaa ya Taifa letu"
Screenshot_20220619-035524_OGInsta%2B.jpg
 
Back
Top Bottom