Makapuku Forum

Makapuku Forum

Uongozi wa Yanga SC umetangaza kumalizana na Mchezaji Saidi Ntibazonkiza huku taarifa hiyo ikisema Mchezaji huyo amemaliza mkataba wake wa miaka miwili.

Taarifa ya Yanga imesema "Uongozi unapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mchezaji wetu Saidi Ntibazonkiza kwa utumishi wake ndani ya Yanga SC, tunamtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha yake ya soka nje ya klabu ya Yanga"
Screenshot_20220530-202621_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220530-202641_OGInsta%2B.jpg
 
Jarida la Business Insider Africa imeorodhesha nchi 20 zinazoongoza kwa ufisadi barani Afrika. Orodha hiyo ni kwa hisani ya kiashiria cha mtazamo wa ufisadi cha Transparency International (CPI) ambacho kinapanga nchi katika kiwango cha kuanzia 0 hadi 100; alama ya 0 ikiwa ni ufisadi mwingi zaidi na 100 ikiwa ndio ufisadi mdogo kurekodiwa.

1. South Sudan: alama 11, imerekodi ufisadi mkubwa zaidi duniani.
2. Somalia: alama 13.
3. Libya: alama 17.
4. Equatorial Guinea: alama 17.
5. Democratic Republic of Congo: alama 19.
6. Burundi: alama of 19.
7. Chad: alama 20.
8. Sudan: alama 20.
9. Comoros: alama of 20.

10. Guinea Bissau: alama 21.
11. Congo: alama 21.
12. Eritrea: alama 22.
13. Zimbabwe: alama 23.
14. Nigeria: Nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika ina alama 24 za mtazamo wa rushwa.
15. Central African Republic: alama 24.
16. Guinea: alama 25.
17. Mozambique: alama 26.
18. Madagascar: alama 26.
19. Uganda: alama 27.
20. Cameroon: alama 27.
Screenshot_20220530-202912_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Marekani Joe Biden amezitembelea familia ambazo Watoto au Ndugu zao waliuwawa kwenye shambulizi la bunduki la wiki iliyopita ambalo lilisababisha vifo vya Watoto 19 na Waalimu wawili wa shule ya msingi ya Robb iliyoko kusini mwa jimbo la Texas.

Akiwa ameambatana na mkewe Jill, Rais Biden alikutana na familia hizo kwa saa kadhaa kabla ya baadae kuwa na mazungumzo na Maafisa wa usalama walioshiriki kutoa msaada wakati wa shambulizi.

Biden na mkewe walitokwa machozi walipofika eneo la kumbukumbu ya ambako kuna picha za wanafunzi na walimu waliouwawa ambapo ziara hii imefanyika wakati ambapo Wananchi wana hasira kutokana na kuzagaa ripoti ya kuwepo uzembe kwa maafisa wa usalama waliofika kupambana na Mshambuliaji ikielezwa kwamba walichelelewa kuanza kukabiliana nae ambapo hii imefanya Wizara ya sheria ya Marekani kutangaza kufungua uchunguzi kubaini ukweli.
Screenshot_20220530-203046_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam @AmosMakalla amesema chanzo cha moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ni hitilafu ya umeme.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea soko hilo kujionea uharibifu wa mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha moto huo umeathiri vibanda 453.

RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na biashara na kuahidi kwamba hakuna Mfanyabiashara atakaeondolewa.

RC Makalla ametoa pole kwa Wafanyabiashara walioathiriwa na moto huo na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali yao inaendelea kutatua changamoto hiyo.

Kutokana na matukio ya moto kujirudia mara kwa mara, RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO, Halmashauri kuweka vifaa vya kudhibiti moto kwenye kila soko na Wafanyabiashara waache tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva na pia kutaka masoko yawe na ulinzi.
Screenshot_20220530-203216_OGInsta%2B.jpg
 
Mwekezaji wa Club ya Simba Mfanyabiashara Mohammed Dewji amesema kwamba miaka mitano iliyopita imekuwa ya mafanikio kwa Club ya Simba ambapo bajeti iliongezeka mara 5 na pia Timu hiyo ikashinda makombe mengi ya ndani na kuweka alama kimataifa kwa kufika robo fainali tatu za michuano ya Afrika.

"Najivunia kuweza kusema tupo katika orodha ya vilabu bora 12 Afrika, hii imekuwa mara ya kwanza Simba kuwa na muendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia yetu, hakuna kurudi nyuma, tunatakiwa kufanya mabadiliko katika maeneo ambayo tuna madhaifu na kwenda mbele, mapambano yanaendelea" ———
Screenshot_20220530-203339_OGInsta%2B.jpg
 
Mama Mzazi wa Mwanamke aitwae Swalha ambaye inadaiwa ameuwawa kwa risasi na Mume wake Jijini Mwanza amesema Mtoto wake alikua nyumbani kwake ( kwa Mama) saa chache kabla ya kuuwawa kwa risasi na kwamba alisikia Mume wa Mtoto wake huyo akimfokea alipompigia simu.

Akiongea akiwa nyumbani kwake Kirumba Mwanza, Mama Mzazi wa Marehemu amesema Mume wa Mtoto wake alimpigia simu na kuomba aongee na Mke wake na kusema yafuatayo "Mke wangu leo nimeshinda njaa toka asubuhi niko melini nasikia sana njaa naomba uwahi uje unipikie chakula, nilisikia kama anafokafoka kidogo kwamba ana njaa sana, kuhusu ugomvi huwa ni simu... mpaka saa tisa za usiku anapiga simu, Marehemu alikuta missed calls 42 Mwanaume anapiga tu simu na alivyopokea ile simu akaanza kumtukana"

Mama huyu amesema ndoa ya Mtoto wake ilikua inatimiza miezi mitano kwani ilifungwa December 2021 , Interview nzima ya Mama akisimulia yote ipo kwenye YouTube ya millardayo
Screenshot_20220530-203508_OGInsta%2B.jpg
 
“Al Ahly ni Real Madrid ya Afrika, wanajua kuingia fainali na wanajua kuicheza fainali, wana timu nzuri na imejiunda vyema sana ila sisi tutaingia kujitahidi kushinda” Walid Regagrui, Kocha wa Wydad Casablanca
Screenshot_20220530-203903_OGInsta%2B.jpg
 
“Maandalizi yetu ni kuelekea dakika 90 za mchezo, hatuwazi sana mambo ya nje ya uwanja ambayo ni siasa, itakuwa bora sana kushinda hapa na lazima tushinde hapa” Pitso Mosimane, Kocha wa Al Ahly
Screenshot_20220530-204004_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Kwanza kabisa pongezi kwako Mpiga picha @kasanga04 , nipo tayari kumuamini Mpiga picha kuliko Binadamu yoyote kwakuwa ni mkweli na anachokupa ni ukweli ulivyo pasipo kificho

Nivute kiti nikae mimi Farhan mwana wa Kihamu, nanukuu maneno ya Ansel Adams alisema “When words become unclear, I shall focus with photographs. When images become inadequate, I shall be content with silence”

Kuna wakati maneno pekee hayaelezeki, usimalize maneno kaa kimya tafakari na kuzifikiria zaidi picha, itafika siku maudhui yatakwisha ila Mpigapicha atakuwa Maudhui

Picha hii ikukumbushe Mwanangu mtaani, ofisini au majumbani usirithi ugomvi usioujua, usirithi vita ambavyo hujui chanzo chake na fahamu unaona padogo sana, ila wapo wanaotumia darubini kuona mbali

Mwijaku anaishi kwenye falsafa makini ya maisha, namkumbuka Askofu wetu aliwahi kusema “If opportunity doesn't knock, build a door.” Alinukuu maneno ya Milton Berle, ndio! Kama hakuna fursa inagonga mlango basi weka mlango

Mwijaku alimaliza kila maneno kuhusu Naseeb mwana wa Sandra, lakini ndio hesabu za maisha, hakuiona fursa kwahiyo kwakuwa haigongi mlango akaweka mlango, akageuka almasi mchangani

Hesabu za kawaida za biashara za Mtu kama Diamond ni lazima uwe na watu kama Mwijaku kwenye bus lako, italeta attention sahihi, akagonga mlango na Mwijaku akafungua kwa roho nyeupe, that’s life

Picha hii utaipenda sana picha hii inatukumbusha hakuna Rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu bali ni maslahi ya kudumu pekee, usisahau kanuni! Usirithi vita usiyoijua

Asante mpiga picha @kasanga04 nakuacha na hii “The best thing about a picture is that it never changes, even when the people in it do.”

Hata kama hao watu pichani watabadilika basi hii picha haitobadilika kamwe

Screenshot_20220530-204246_OGInsta%2B.jpg
 
ARSENAL WABADILI GIA ANGANI !!
.
Baada ya kuona dili la straika wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus lina ugumu kwenye kukamilika, Arsenal imeamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye dili la straika wa Atletico Madrid na Hispania ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Juventus, Alvaro Morata, 29.
.
Atletico imeripotiwa kuwa tayari kumuachia staa huyo ambaye mkataba wake unamalizika 2023.
Screenshot_20220530-205801_OGInsta%2B.jpg
 
| PERISIC SPURS
.
Kiungo wa Inter Milan na Croatia, Ivan Perisic, 33, amefikia makubaliano na mabosi wa Tottenham ya kujiunga na timu hiyo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa mkataba wa miaka miwili.
.
Chanzo cha karibu na mchezaji huyo kimefichua kuwa Chelsea na Juventus nazo zilihitaji sana kumpata lakini Peresic ameonekana kuipa nafasi kubwa Spurs kutokana na uwepo wa Antonio Conte.

……………..
Screenshot_20220530-205913_OGInsta%2B.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

Ninachokijua kuhusu Saido, kwanza amekuja Yanga akiwa umri umemtupa mkono, kwa bahati nzuri katika umri huohuo amecheza katika level ambayo asilimia kubwa ya vijana wameshindwa kuifikia, si wale walio ndani au nje ya Yanga.

Ninachokiamini Yanga imeacha moja ya wachezaji wao bora msimu huu, huwezi ukabeza mchango wa Saido hata kidogo labda kama humpendi au hutaki kusimama kwenye ukweli, ameamua alama nyingi za Yanga msimu huu na yupo kwenye tano bora yangu ya waliowaka zaidi.

Kwanza lazima tujue Yanga imepoteza mchezaji wa aina gani, wengi walimuona Saido kama ni winga kwa sababu tu katika mfumo wa 4-2-3-1 wa Mohammed Nabi alikuwa anatokea pembeni lakini jukumu lake la msingi lilikuwa ni kuchezesha timu, Playmaker.

Ni moja ya wachezaji bora ambao wanaweza kuzishambulia half spaces ( nafasi baina ya beki wa kati na beki wa pembeni ) anakimbia hapo au kuna muda anakuwa inverted ( kuvunjikia ndani ) ili kumsaidia kiungo wa kati mshambuliaji ( CAM ) na kuifanya timu iwe na viungo wawili wa juu washambuliaji.

Ukiniuliza mimi juu ya uwezo wake wa kupiga mipira iliyokufa nampa B, hana accuracy kubwa ya kutisha ingawa vipo vipindi ambavyo alikuwa akitishia amani, hiyo maana yake hakuwa na consistency katika aina hiyo ya mipira, hakuwa mzuri wala hakuwa mbaya kiasi cha kutompa credit zake.

Nimeona mijadala mitandaoni watu wanapendekeza asajiliwe Aziz Ki, em! tujiulize maswali, nani anamfatilia Aziz kwa sasa? nani anaijua perfomance yake ya sasa? kwa bahati mbaya utapata jibu kuwa wanaomtaka Aziz wengi wanasema hivyo kwa kukitazama kiwango cha CAF.

Mfano wewe unaesoma makala hii mara yako ya mwisho kumuona Aziz akicheza ilikuwa ni lini? jibu baki nalo.

Kumuacha Saido ni mtihani mgumu kwa Yanga kwa sababu daraja ambalo mwamba alifikia inahitaji umakini ili kumtafuta mbadala wa kuliziba pengo lake, kwa vyovyote vile sioni kama kuna mchezaji yeyote wa Kitanzania anaweza kulifikia labda kama Yanga watafanya scouting nje ya nchi.

Asante.
Screenshot_20220530-222021_OGInsta%2B.jpg
 
Biashara ya ukahaba imevamia kwa kasi baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, na kusababisha kero na adha kubwa katika makazi ya watu, hasa eneo la Sinza kiasi cha kuzifanya baadhi ya familia kuhama nyumba, Mwananchi limebaini.

Wazazi na walezi wanasema hali hiyo pamoja na kelele zinazosababishwa na muziki unaopigwa kwenye baa kubwa vimewasababishia ugumu usizoelezeka wa malezi ya watoto.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini biashara hiyo imekithiri katika mitaa mingi ya Sinza, hasa ile inayozunguka kumbi maarufu za starehe na hoteli kubwa.

Hali hiyo inayomulikwa kwa Sinza, ipo pia maeneo mengine kama Tabata, Ubungo, Kindondoni Buguruni na kwingineko, japokuwa ni kwa viwango tofauti.

Kutokana na hali ilivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe hivi karibuni alikutana na watendaji na wenyeviti wa mitaa ili kujadili mambo mbalimbali, likiwemo la biashara hiyo huku akiwataka viongozi wa dini kulikemea suala hilo akisema utamaduni huo si wa Tanzania.

Wakazi wa maeneo husika wanasema mbali na kuwaletea changamoto ya malezi, hali hiyo imewalazimisha kubadili mifumo ya maisha ili kuzilinda familia zao.


Youngblood njoo usome ulichokuwa unataka kujua
Screenshot_20220531-144802_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom