Makapuku Forum

Makapuku Forum

Farhan Jr

Petr Cech anasema kuelekea fainali dhidi ya Bayern Munich, walikaa Makipa wote wa Chelsea! Yani yeye, Ross Turnbull na Hilario, pamoja na Kocha wa Makipa Christophe Lollichon

Walikaa kutazama penati zote za Bayern Munich kuanzia 2007 mpaka 2012 yani misimu mitano yote, wakizisoma penati zao kuanzia wapigaji na Makipa wao, kila taarifa muhimu waliinukuu kwa ajili yao na wapigaji wao

Ni kama waliota kwakuwa fainali hii ilikuwa na matuta sita jumla! Ambapo Chelsea walicheza matuta matatu, likiwemo lile la Arjen Robben dakika ya 105 tu

Cech aliwaambia wapigaji wote wa penati haswa wa mguu wa kushoto kuwa penati zote za wapigaji wa mguu huo basi Manuel Neur huwa anaruka upande wa kushoto hivyo namna pekee ni kupiga upande wa kulia, huwa hafuati, mara nyingi

Kwenye wapiga penati wa Chelsea usiku ule, wapjigaji wa mguu wa kushoto walikuwa Juan Mata na Ashley Cole! Hivyo walikuwa na taarifa hiyo muhimu kuhusu Manuel Neur

Bahati mbaya sana Juan Mata wakati anaenda kupiga licha ya kuwa na hiyo taarifa anasema alivyofika langoni aliamini Neur angeruka kulia hivyo akapiga kushoto, ambapo Neur alisafiri kweli na akaicheza penati ile

Mpigaji wa pili wa mguu wa kushoto alikuwa Ashley Cole ambaye nae alichagua kuiweka penati upande wa kushoto ambapo Neur alisafiri kweli na aliipangusa, bahat nzuri tu ni kuwa Cole alipiga jiwe haswa ikazama

Cech aliicheza penati ya Bastian wa Munich, anasema wakati wanazisoma penati za Bayern waligundua Bastian kwenye penati tano za mwisho kabadili style ya upigaji, hakai mbali na hakai karibu anajiposition kati kati

Hivyo Cech alifahamu Bastian atasita kisha ataupiga mpira kidogo sana, hivyo akachagua kumsubiri na akasafiri na mpira ule na kuicheza ile penati, hivyo kazi ikabaki kwa KING DD kumaliza mchakato

Drogba aliambiwa na Makipa kuhusu Neur na wapigaji wa mguu wa kushoto, hivyo akaigusa tu upande wa kulia wa Neur nae akaenda kushoto na kupotea kabisa! Chelsea tukashinda kwa penati

YEEES hivi ndivyo watu hushinda mechi, ichukue hii ilete kwenye maisha ya kawaida! Lazima uwekeze kwenye muda, ujitese kisha upate matunda’! Imagine kukesha na penati za Bayern kwa miaka mitano yote! Just imagine
View attachment 2231153
Thats the level of preparation and attention to detail that goes into professional football....😍😍😍😍. Talk about being pedantic!!!
 
Kila la heri mnyamaaa
Screenshot_20220528-152422_Instagram%20Lite.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom