Imeandikwa na @swalehmawele

Ngoja niwaambieni kitu, mnaiona Azam? mnadhani ni timu ambayo inaweza kuwatingisha Simba na Yanga katika mbio za ubingwa? mnadhani Simba akitaka ubingwa anaifikiria Azam kama kikwazo? mnadhani Yanga akiutaka ubingwa anaifikiria Azam kama kikwazo? wanafikiriana wao kwa wao, Yanga anaamini akiwa juu ya Simba bingwa atakuwa yeye na hivyohivyo kwa Simba.

Twende hapa, kinachowafanya Simba na Yanga watambe katika soka la Tanzania ni wachezaji wa kigeni, yes, wachezaji wa kigeni ndo wanaoleta utofauti mkubwa ukiwalinganisha na wazawa wengi, wachezaji wazawa kwa asilimia kubwa ndio walewale wanaopatikana katika klabu za Mbeya City, Kagera Sugar, KMC na klabu nyingine, hakuna utofauti mkubwa wa uwezo baina yao.

Hii Yanga ya sasa asilimia kubwa ya wachezaji walioleta utofauti ni wachezaji wa kigeni, wale akina Bangala, Mayele, Djigui, Djuma na wengine ndio walioleta utofauti, ukichanganya na quality ya akina Bakari, Nondo na wengine Yanga inakuwa pale, hivyohivyo kwa Simba, asilimia kubwa wachezaji wa kigeni ndio walioleta utofauti ukichanganya na quality ya wazawa wachache.

Maana yangu ni hii, wachezaji wa kigeni wa Azam wengi hawaleti utofauti, hawawi chachu ya kubusti quality ya wachezaji wazawa ili kuipeleka timu katika levo fulani, tatizo la msingi linaanzia hapo, Azam inafelishwa sana na jambo hilo, yes inaweza kuwa ngumu kubeba ubingwa mbele ya Simba na Yanga lakini mkawa timu yenye ushindani hasa na itakayokuwa ngumu kudondosha alama.
Asante.