Makapuku Forum

Makapuku Forum

"Kutoa nafuu kutokana na kasi ya kupanda kwa bei za mafuta hakuwezi kusubiri hadi mwaka ujao wa fedha”

“nimeamua...wananchi waanze kupata nafuu hiyo kuanzia tarehe mosi Juni mwaka huu, nimeelekeza kwamba serikali tujibane na tujinyime ili kupata fedha kutoka katika matumizi ya kawaida ya serikali ili ziende kutoa nafuu katika bei za mafuta kwenye kipindi kuelekea mwaka mpya wa fedha" Rais Samia
Screenshot_20220509-202144_OGInsta%2B.jpg
 
Na mpiraaaa umekwishaaaa dk za nyongeza 5 wamepewa mpaka 10 kwa kubebwa hawa watu wangekuwa simba hapo yanga wangelalamika tumeongezewa dk
 
Mambo 10 nilioyaona Yanga Vs Prison

1: MECHI 3 BILA USHINDI. MECHI 3 BILA BAO. Sumu kubwa inayootesa Yanga kwa sasa ni kukosa 'CHAMPION MENTALITY'. Hofu ni kubwa sana kwenye vifua vya Viongozi, Benchi la Ufundi na Wachezaji. Ni kama Yanga wanacheza wakiwaza zaidi 'Gape' ya Pointi kuliko Dakika 90 za mchezo husika

2: Sumu nyingine inayowatesa Yanga ni MAYELE. 'Ushabiki' wa jukwaani umehamia uwanjani. Ni kama Yanga wamesahau kuwa jambo muhimu zaidi ni YANGA KUSHINDA sio MAYELE KUTETEMA

3: Kipindi cha pili Prison walirudi vyema kwenye 'Low Block' na kupunguza hatari tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza. Jambo pekee ambalo kocha wa Prison anatakiwa kulifanyia kazi ni kujua namna gani Timu yake inacheza ikiwa na mpira. Ni aibu kwa Timu ya Ligi kuu kuwa 'Poor' kiasi kile kwenye Positive Transition. Kwanini?

4: Yanga walicheza kwa presha sana. Muda waliosukuma watu wengi mbele, Safu yao ya ulinzi ilikuwa imevurugika kwenye mpangilio wao. Ilikuwa nafasi nzuri kwa Prison kutega 'counter Attack na kuwaadhibu Yanga

5: Well Done Golikipa wa Prison, Hussein Abel Ni nyota wa mchezo kwa upande wangu. Sahau kuhusu 'Saves' rudi na utazame jinsi alivyokuwa anaipanga safu yake ya ulinzi kudili na krosi za Yanga..

6: 'Sub' ya Makambo ilikuwa sahihi, kilichokosea ni mtu aliyetoka. Sure Boy alikuwa Plan B ya Yanga kwenye kupita katikati. Kumtoa kuliiacha Yanga na mpango wa krosi tu. Kitu ambacho walishaonekana kufeli kuanzia mwanzo

7: Jumanne Elfadhil.. What A Warrior! Mtu haswa. Alijitoa sana kwenye kugombea mipira ya 50/50 na akawa msaada kwa kudumbukia katikati ya Chona na Mwihambi kwenye kucheza krosi

8: Mliodhani shida ni Cedric Kaze pekee, Leo mmepata majibu. Shida ni benchi zima la Ufundi la Yanga. Hawana 'Plan' B ya kuifungua Timu inayozuia kwenye 'Low Block'

9: Bado Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga msimu huu atabaki kuwa YANICK BANGALA. Jinsi alivyokuwa anaitoa timu na kuiunga kwa viungo wake ni sanaa ya viwango vya juu sana

10: Well Done Mwihambi Well Done Asukile na Mwashilindi. Jasho lao limevuja haswa! Ile ndio DNA ya Prison wanapokuwa kwenye wakati mgumu kiwanjani

Nb: Wameacha Kutetema.. wameanza KUTETEMEKA
Screenshot_20220509-213458_OGInsta%2B.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

FT: Yanga 0 - 0 Tanzania Prisons

Plan ya kwanza kwa Tanzania Prisons ilikuwa kuzuia, plan ya pili ikawa kuzuia na plan ya tatu ikawa kushambulia, walichagua kwanza kubaki kwenye eneo lao zaidi, wacheze low block ili kuziba mianya ya Yanga kutengeneza nafasi kutokea kwenye flanks na eneo la kiungo.

Tanzania Prisons hawakuonyesha madhara katika lango la Yanga walipokuwa na mpira, walishambulia wakiwa na idadi ndogo ya wachezaji, zilitokea 1 v 3 au 2 v 5 nyingi, Yanga walipokonya mipira mingi na kuanzisha wao mashambulizi.

Kama unachagua kukaa zaidi kwenye eneo lako hakikisha unakuwa na usahihi wa pasi mnapokuwa na mpira, kasi na mcheze direct ili kuitumia mianya baada ya walinzi wa timu pinzani kusogea katika high line, Prisons hawakufanya hivyo, walipoteza mipira mingi kirahisi.

Mohamed Nabi alitaka zaidi bao kuliko perfomance, alichagua kubadilisha game plan katika kipindi cha pili, watumie mipira mirefu inayodondoka katika eneo la kumi na nane kisha washindane kwenye aerial balls, hata sub ya Makambo ilikuwa katika mpango huo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mipira ya juu.

Labda kama namtazama tofauti, Saido Ntibazonkiza ameshuka kidogo kiwango chake, katika takriban mechi tano za mwisho hajacheza kama tunavyomjua.
Linapokuja swala la kuzuia na kutumia nguvu hii Prisons naifanyananisha na Burnley ya Uingereza, watakupa mechi hasa hata kama utashinda.

Jumanne Ninkaza, mwanaume wa shoka hasa, maana halisi ya defensive midfielder.
Nilisema katika analysis yangu kabla ya mechi hii kuanza, kama Prisons atafanikiwa kumzuia Yanga katika kipindi cha kwanza pengine akaokota alama, Prisons wamefanikiwa.
Screenshot_20220509-214503_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Ntibazonkiza kuomba mpira kwa Djuma Shaban kisha kumpa Fiston Mayele apige kwangu ilikuwa sahihi tu

Djuma kukubali bila kuleta utata ilikuwa sahihi zaidi, Mayele kwenda kupiga na kukosa ni jambo sahihi zaidi kwakuwa dhahabu safi huoshwa kwa moto

Ni time tu kuna mambo yanakataa na time yanakubali! Aliwahi kuchukua penati Bruno mbele ya Ronaldo, aliwahi kuomba Lucas Vasquez wa Real Madrid ile penati ya kwanza pale San Siro, UEFA Real vs Atletico! Mbele ya Ronaldo, Bale, Marcelo na Ramos

If you have the guts then step up and take it, mpira ni kama kuwa MWANAUME, unalia, unaamka na unasonga

Hivi ni vipindi ambayo lazima upitie kwenye ligi, hakuna sehemu kuna ubingwa rahisi, hata ile Arsenal Invicibles ilitwaa ubingwa bila kufungwa lakini walikuwa na sare 12

We call it football, the game we all love more than Ngono to be precise
Screenshot_20220509-215220_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom