Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mambo 10 nilioyaona Yanga Vs Prison

1: MECHI 3 BILA USHINDI. MECHI 3 BILA BAO. Sumu kubwa inayootesa Yanga kwa sasa ni kukosa 'CHAMPION MENTALITY'. Hofu ni kubwa sana kwenye vifua vya Viongozi, Benchi la Ufundi na Wachezaji. Ni kama Yanga wanacheza wakiwaza zaidi 'Gape' ya Pointi kuliko Dakika 90 za mchezo husika

2: Sumu nyingine inayowatesa Yanga ni MAYELE. 'Ushabiki' wa jukwaani umehamia uwanjani. Ni kama Yanga wamesahau kuwa jambo muhimu zaidi ni YANGA KUSHINDA sio MAYELE KUTETEMA

3: Kipindi cha pili Prison walirudi vyema kwenye 'Low Block' na kupunguza hatari tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza. Jambo pekee ambalo kocha wa Prison anatakiwa kulifanyia kazi ni kujua namna gani Timu yake inacheza ikiwa na mpira. Ni aibu kwa Timu ya Ligi kuu kuwa 'Poor' kiasi kile kwenye Positive Transition. Kwanini?

4: Yanga walicheza kwa presha sana. Muda waliosukuma watu wengi mbele, Safu yao ya ulinzi ilikuwa imevurugika kwenye mpangilio wao. Ilikuwa nafasi nzuri kwa Prison kutega 'counter Attack na kuwaadhibu Yanga

5: Well Done Golikipa wa Prison, Hussein Abel Ni nyota wa mchezo kwa upande wangu. Sahau kuhusu 'Saves' rudi na utazame jinsi alivyokuwa anaipanga safu yake ya ulinzi kudili na krosi za Yanga..

6: 'Sub' ya Makambo ilikuwa sahihi, kilichokosea ni mtu aliyetoka. Sure Boy alikuwa Plan B ya Yanga kwenye kupita katikati. Kumtoa kuliiacha Yanga na mpango wa krosi tu. Kitu ambacho walishaonekana kufeli kuanzia mwanzo

7: Jumanne Elfadhil.. What A Warrior! Mtu haswa. Alijitoa sana kwenye kugombea mipira ya 50/50 na akawa msaada kwa kudumbukia katikati ya Chona na Mwihambi kwenye kucheza krosi

8: Mliodhani shida ni Cedric Kaze pekee, Leo mmepata majibu. Shida ni benchi zima la Ufundi la Yanga. Hawana 'Plan' B ya kuifungua Timu inayozuia kwenye 'Low Block'

9: Bado Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga msimu huu atabaki kuwa YANICK BANGALA. Jinsi alivyokuwa anaitoa timu na kuiunga kwa viungo wake ni sanaa ya viwango vya juu sana

10: Well Done Mwihambi Well Done Asukile na Mwashilindi. Jasho lao limevuja haswa! Ile ndio DNA ya Prison wanapokuwa kwenye wakati mgumu kiwanjani

Nb: Wameacha Kutetema.. wameanza KUTETEMEKA View attachment 2218331
Hebu leta tofauti ya Point Auntie
Tuweke kumbukumbu sawa
 
MUUNDO MPYA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUANZIA 2024/25

•Kutakuwa na jumla ya timu 36

• Kila timu itacheza mechi nane dhidi ya timu nane tofauti

•Hakuna makundi bali ni kama mfumo wa ligi

• Timu nane za juu kwenye msimamo zitafuzu kwenye mtoano moja kwa moja

•Timu itakayoshika nafasi ya 9-24 zitacheza mtoano wa mechi mbili kufuzu hatua ya 16 bora
Screenshot_20220510-201519_OGInsta%2B.jpg
 
ANTONIO RUDIGER TO REAL MADRID DONE DEAL

Beki wa Chelsea, Toni Rudiger amekamilisha dili lake la miaka minne kujiunga na Real Madrid ya Hispania

Dili halitotangazwa mpaka mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kuiheshimu Chelsea
Screenshot_20220510-201701_OGInsta%2B.jpg
 
MREMBO KUNOGESHA FAINALI YA UEFA
.
Camila Cabello (25) mrembo mwenye asili ya Cuba amethibitishwa kuongoza katika sherehe za ufunguzi wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Real Madrid, Mei 28, 2022.
.
“Nina furaha sana kupanda kwenye jukwaa la UEFA. Fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Paris mwezi huu. Ninakusudia kufanya onyesho maalum, kuleta pamoja ari ya urithi wangu wa Kilatini na hisia ya umoja kwa mashabiki wa michezo na muziki ulimwenguni kote, siwezi kungoja zaidi.”
.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kutazamwa na mataifa zaidi 200, hivyo inatajwa kati ya watu 380-400 milioni watatazama.
Screenshot_20220510-202410_OGInsta%2B.jpg
 
KAZE: MALALAMIKO YANAVUNJA MOYO WACHEZAJI
.
“Matokeo mabaya ni kweli yanaumiza hata sisi makocha hakuna anayefurahia kuona timu yake haipati matokeo mazuri, tunaumia sana lakini hatuna jinsi, cha msingi tunaangalia mechi zijazo tufanye vizuri.
.
“Najua wanaumia sana kuona timu haifanyi vizuri lakini wajue Mungu huenda kuna kitu kikubwa ametuandalia huko mbele, habari za kulalamika hadi kupitiliza sio vizuri zinatuvunja moyo wachezaji,” amesema Cedrick Kaze.
Screenshot_20220510-202532_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom