Makapuku Forum

Hebu leta tofauti ya Point Auntie

Tuweke kumbukumbu sawa
 
MUUNDO MPYA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUANZIA 2024/25

•Kutakuwa na jumla ya timu 36

• Kila timu itacheza mechi nane dhidi ya timu nane tofauti

•Hakuna makundi bali ni kama mfumo wa ligi

• Timu nane za juu kwenye msimamo zitafuzu kwenye mtoano moja kwa moja

•Timu itakayoshika nafasi ya 9-24 zitacheza mtoano wa mechi mbili kufuzu hatua ya 16 bora
 
ANTONIO RUDIGER TO REAL MADRID DONE DEAL


Beki wa Chelsea, Toni Rudiger amekamilisha dili lake la miaka minne kujiunga na Real Madrid ya Hispania

Dili halitotangazwa mpaka mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kuiheshimu Chelsea
 
MREMBO KUNOGESHA FAINALI YA UEFA
.
Camila Cabello (25) mrembo mwenye asili ya Cuba
amethibitishwa kuongoza katika sherehe za ufunguzi wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Real Madrid, Mei 28, 2022.
.
“Nina furaha sana kupanda kwenye jukwaa la UEFA. Fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Paris mwezi huu. Ninakusudia kufanya onyesho maalum, kuleta pamoja ari ya urithi wangu wa Kilatini na hisia ya umoja kwa mashabiki wa michezo na muziki ulimwenguni kote, siwezi kungoja zaidi.”
.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kutazamwa na mataifa zaidi 200, hivyo inatajwa kati ya watu 380-400 milioni watatazama.
 
KAZE: MALALAMIKO YANAVUNJA MOYO WACHEZAJI
.
“Matokeo mabaya ni kweli yanaumiza hata sisi makocha hakuna anayefurahia kuona timu yake haipati matokeo mazuri, tunaumia sana lakini hatuna jinsi, cha msingi tunaangalia mechi zijazo tufanye vizuri.
.
“Najua wanaumia sana kuona timu haifanyi vizuri lakini wajue Mungu huenda kuna kitu kikubwa ametuandalia huko mbele, habari za kulalamika hadi kupitiliza sio vizuri zinatuvunja moyo wachezaji,” amesema Cedrick Kaze.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…