Makapuku Forum

Makapuku Forum

Hongera Wamama wote humu Jukwaani.
Mko sababu ya kutufanya tutabasamu muda wote. Kimbilio tunapokuwa kwenye matatizo.
Kuwa mama ni zaidi ya kuzaa, unapokuwa unatimiza kazi za mama wewe ni mama haijalishi ulipanua miguu, ulipigwa kisu au hukwenda leba. Happy mother's day
 
Lee nashukuru sana kwa salamu hapo juu, wewe ni anko wangu lakini ndiyo unaongoza kunifanyia fitna ila sina namna, undugu haununuliwi.

Salam zako ninazo, zipo nzuri na zile za kawaida za Halima, anasema kaokoka siku hizi,.jitahidi umsave kama Domitila
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameitisha kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na Makatibu Wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza Viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la upandaji wa bei ya mafuta nchini.
Screenshot_20220509-041104_OGInsta%2B.jpg
 
Kijana Tariq Mpemba aliyemwagiwa kitu kinachodaiwa kuwa ni tindikali Mkoani Kilimanjaro March 2022, ameondoka leo nchini Tanzania akielekea nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Tariq amesema amesema "Pua imeshikana na mdomo na hali imezidi kuwa mbaya zaidi, naona giza zaidi zinahitajika million 35”

Namba za kumsaidia ni 0764510774 (Tark Kipemba) Au Benki kupitia account namba
3012111594790 (Tariq Kipemba).
Screenshot_20220509-041226_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi ametangaza ongezeko la mshahara kwa 15% , ambapo ongezeko hilo litazingatia mfumo wa uzoefu, elimu na ujuzi.

"Serikali imetenga Tsh. Billion 12.7 kwa mwezi sawa na Tsh. Billion 153 kwa mwaka ili kugharamia utekelezji wa zoezi hili katika mwaka ujao wa fedha"
Screenshot_20220509-041429_OGInsta%2B.jpg
 
Uingereza imesema itatoa dola Bilioni 1.6 za ziada kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine, Uingereza imetoa ahadi hiyo kuelekea kwa mkutano utakaofanyika kwa njia ya video leo Jumapili wa kundi la mataifa yenye uchumi mkubwa duniani G7 pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.

Waziri Mkuu Boris Johnson amekuwa muungaji mkono imara wa juhudi za Ukraine za kupambana na vikosi vya Urusi tangu kuanza kwa vita hivyo mnamo Februari 24.

Serikali ya Uingereza tayari imeshatuma silaha kadhaa nchini Ukraine ikiwemo makombora ya kuharibu vifaru na mifumo ya ulinzi wa anga, ahadi hiyo ya fedha inakaribia mara mbili ya fedha za awali zilizotolewa na Serikali hiyo kwa ajili ya kuisaidia Ukraine, na pia ndio kiwango cha juu zaidi kilichotumiwa katika mzozo tangu vita vya Iraq na Afghanistan.

Viongozi wa kundi la G7- Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani watashiriki mkutano kwa njia ya video na rais wa Ukraine leo Jumapili, siku moja kabla ya Urusi kuadhimisha Siku ya Ushindi, kukumbuka kumalizika kwa vita kuu vya pili vya dunia barani Ulaya.
Screenshot_20220509-041731_OGInsta%2B.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema utaratibu wa ajira za ualimu mwaka huu kila muombaji atatakiwa kuchagua Shule, Wilaya na Mkoa anaotaka kufanyia kazi na hivyo sio rahisi kwa Mwalimu kupata ajira na kutaka kubadilisha kituo.

Deus ametoa kauli hiyo kufuatia tabia ya baadhi ya Walimu kuomba ajira na wakishapata huomba kuhamishiwa maeneo mengine. "Niwakumbushe pia kuwa CWT sio Mamlaka ya kuhamisha Walimu"

"Kwa mfano unafundisha Biology unataka uende Kilimanjaro unaingia Mkoa wa Kilimanjaro unaenda Wilaya ya Same inakuambia nafasi ya kufundisha Biology ipo Mkoa fulani"

"Kwahiyo naamini Walimu wetu watakaokuja kwenye ajira hilo wameshajua kwamba mfano unaambiwa anaenda kuziba nafasi ya Mwalimu wa Physics aliyopo Ukerewe au Chunya sio kwenda kuchukua kibali cha kuajiriwa ili arudi Dodoma"
Screenshot_20220509-041927_OGInsta%2B.jpg
 
Muungano wa Mashirika ya Ndege nchini Nigeria umesema utasimamisha safari zote za ndege kuanzia kesho Jumatatu kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, Muungano huo umesema bei ya mafuta ya ndege imepanda kutoka Naira 190 za Nigeria (Tsh. 1,064) hadi Naira 700 (Tsh. 3,922) kwa lita.

Muungano huo umesema hakuna Shirika lolote la Ndege Duniani linaloweza kustahamili gharama kubwa ya uendeshaji ambapo umesema itamlazimu abiria kulipa hadi dola 289 kwa safari ya ndege ya saa moja kiasi ambacho Raia wengi wa Nigeria ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, hawataweza kumudu.

Wizara ya usafiri wa anga imeutolea mwito muungano huo kuzingatia athari za kusitisha safari za ndege kwa Wanigeria na wasafiri wa kimataifa.

Nigeria inazalisha mapipa milioni 1.4 ya mafuta ghafi kwa siku, japo inasafisha kiasi kidogo tu cha mafuta hayo, Nchi hiyo hutegemea mafuta yanayoagizwa kutoka nje na kufanya soko la ndani kutatizika iwapo kutatokea uhaba wa bidhaa hiyo.
Screenshot_20220509-042027_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari katika Barabara ya Tanga- Segera eneo la Hale Wilayani Korogwe.

Kaimu RPC wa Tanga, David Mwasimbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo "Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa Dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, Dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea"

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dk Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo DC Mwanukuzi "Majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo DC na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu na majeruhi mmoja tumempatia rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi"
Screenshot_20220509-042522_OGInsta%2B.jpg
 
Kapombe mechi ya 100 Simba

BEKI wa Simba, Shomari Kapombe anatimiza mchezo wake wa 100 kuichezea klabu hiyo tangu alipojiunga nayo akitokea Azam FC.

Kapombe ametimiza mchezo wake huo leo Jumapili Mei 8, 2022 dhidi ya Ruvu Shooting unaoendelea kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kapombe alisaini mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC, Juni 2017 na sasa ni msimu wake wa tatu akiwa Simba.
Screenshot_20220509-042657_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Nape Nnauye ametoa onyo kwa baadhi ya watu wanaonunua mitaa ili ipewe majina yao katika uwekaji wa anwani za makazi.

Nnauye ametoa onyo hilo leo Jumapili Mei 8, 2022 wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua uwekaji wa anwani za makazi.
Screenshot_20220509-043216_OGInsta%2B.jpg
 
Maonesho ya kimataifa ya biashara ya utalii ‘Karibu-Kilifair 2022’ yanatarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Juni 3 hadi 5 kwa lengo la kutengeneza fursa mpya za biashara.

Kilifair iliahirishwa kwa miaka miwili iliyopita kutokana na janga la Uviko-19

Maonesho hayo ya siku tatu yanatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya wafanyabiashara 450 kutoka pande zote za Afrika Mashariki, zaidi ya wanunuzi 600 wa kimataifa kutoka pande zote za dunia na wageni zaidi ya 7,000.
Screenshot_20220509-043320_OGInsta%2B.jpg
 
Tariq Awadhi (31) leo Jumapili Mei 8, 2022 ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa macho.

Tariq ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) baada ya kumwagiwa tindikali anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa macho katika Hospitali ya Apollo iliyopo nchini India.

Tariq anahitaji Sh35 milioni ili aweze kufanyiwa upasuaji wa macho katika hospitali ya Apollo.

Akizungumza na Mwananchi digital leo kabla ya kuondoka uwanja wa Ndege wa Kimataifa (KIA), Tariq amewashukuru Watanzania waliomchangia kiasi cha Sh14 milioni.

"Nawashukuru Watanzania wenzangu ambao wanaendelea kunichagia naomba wasikate tamaa waendelee kunisaidia ili niweze kufanikiwa kurudisha macho yangu katika hali yake ya kawaida kwani maumivu ni makali.

"Mpaka sasa wananchi wameweza kunichagia kiasi cha Sh14 milioni, nawashukuru sana kwa upendo wao kwangu, naomba mzidi kuniombea ili niweze kufanikisha matibabu yangu, naamini msaada wenu na maombi yenu ni muhimu sana kwangu nawategemea sana,"amesema Tariq

Tariq ameendelea kuwaomba Watanzania na Serikali kumsaidia ili afanikishe matibabu yake
Kwa yeyote atakayeguswa kumchangia Tariq, namba zake ni 0764510774 Au Akaunti namba zake ni :3012111594790 Equity Benki kwa jina la Tariq Kipemba
Screenshot_20220509-043414_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom