Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde amewataka Watu waache kumsema vibaya Hayati Magufuli kwasababu hayupo na hawezi kujibu.

"Ndugu zangu tusifikiri kumsema vibaya Magufuli kutatusaidia hawezi kujibu hayupo kama ulikuwa na tatizo naye maliza utakuja kukutana naye kwa Mungu, Mtu akishatangulia kitabu chake kinafungwa tunamuachia Mwenyezi Mungu kuja kutoa hukumu, Watu mnakuwa waoga Viongozi wakiwepo hamsemi wakiondoka ndio mnasema huu ni uoga uliopitiliza"

"Mtu mmoja tu alisema kwa vitendo kwamba yeye hawezi kufanya kazi na Magufuli, Nyalandu alichia ubunge hapa akaondoka tuliobaki hapa ni Watu wa Magufuli na tulifanya nae kazi na tulikuwa tunamsifu tusiweke unafiki, hawa wanaomsema vibaya Magufuli na kumsifu Samia ni wanafiki wakubwa Samia akiondoka watamsema hivyohivyo bora Mimi"
Screenshot_20220422-174327_OGInsta%2B.jpg
 
Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam umetoa taarifa kwa Watumiaji barabara inayopitia Daraja la Tanzanite kuwa inatarajia kufanya maboresho kwenye baadhi ya miundombinu ya Daraja hilo na hivyo barabara hiyo itafungwa Jumamosi April 23,2022 kuanzia saa 12 asubuhi na kufunguliwa Jumapili April 24,2022 saa 12 jioni.

"Katika kipindi chote cha maboresho ya Daraja hili vyombo vya moto pamoja na watembea kwa miguu hawataruhusiwa kupita katika Daraja kwasababu za kiusalama"

"TANROADS Mkoa wa Dar es salaam inawashauri Watumiaji wa Daraja hilo kutumia barabara mbadala ya Kaunda na Ali Hassan Mwinyi wakati wa maboresho husika"
Screenshot_20220422-174555_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde amewataka Watu waache kumsema vibaya Hayati Magufuli kwasababu hayupo na hawezi kujibu.

"Ndugu zangu tusifikiri kumsema vibaya Magufuli kutatusaidia hawezi kujibu hayupo kama ulikuwa na tatizo naye maliza utakuja kukutana naye kwa Mungu, Mtu akishatangulia kitabu chake kinafungwa tunamuachia Mwenyezi Mungu kuja kutoa hukumu, Watu mnakuwa waoga Viongozi wakiwepo hamsemi wakiondoka ndio mnasema huu ni uoga uliopitiliza"

"Mtu mmoja tu alisema kwa vitendo kwamba yeye hawezi kufanya kazi na Magufuli, Nyalandu alichia ubunge hapa akaondoka tuliobaki hapa ni Watu wa Magufuli na tulifanya nae kazi na tulikuwa tunamsifu tusiweke unafiki, hawa wanaomsema vibaya Magufuli na kumsifu Samia ni wanafiki wakubwa Samia akiondoka watamsema hivyohivyo bora Mimi"
View attachment 2196616
Bora yeye vipi?
 
Back
Top Bottom