Makapuku Forum

Makapuku Forum

Madereva wa Bodaboda na Bajaji wakiwemo wenye wameandamana hadi kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakishinikiza Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa kutengua tamko alilolitoa leo kuhusu bodaboda na bajaji kuingia wakisema tamko hilo limekinzana na makubaliano ya pamoja yaliyowekwa kati ya Waendesha Bajaji wenye ulemavu na Waendesha bodaboda wasio na ulemavu.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na bajaji za Watu wenye ulemavu kuruhusuwa kuingia katikati ya mji na kuegesha kwenye Vituo vitatu walivyopangiwa, bajaji za wasio na ulemavu kutoruhusiwa kuingia katikati ya mji, bodaboda zilizosajiliwa na kukidhi vigezo kuruhusuwa kuegesha kwenye vituo saba katikati ya mji na bodaboda zisizokuwa na vibali kuruhusiwa kuingia mjini Kwa kigezo cha kushusha abiria na kugeuza.

Katika jitihada za kutuliza maandamano hayo Mkuu wa Mkoa Amoss Makalla alilazimika kuwasiliana na Waziri Bashungwa kwa simu na kumuelezea hali halisi ya maandamano ambapo Waziri Bashungwa aliridhia kuendelea kwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa pikipiki na bajaji kuingia Katikati ya mji kwa mujibu wa makubaliano na maridhiano ya pamoja yaliyokuwa yamewekwa kati ya Waendesha bajaji wenye ulemavu na waendesha bodaboda.
Screenshot_20220421-184701_Instagram.jpg
Screenshot_20220421-184722_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo April 21,2022 imekutana na Timu ya Wataalam wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp ambapo kwa pamoja wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma hizo nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Screenshot_20220421-184912_Instagram.jpg
 
Rais Vladimir Putin ameliamuru leo Jeshi la Urusi kufuta mipango ya kukivamia kiwanda cha chuma ndani ya mji wa bandari wa Mariupol ambako maelfu ya Wanajeshi wa Ukraine na Raia wamejificha.

Putina amesema "Hakuna haja ya kupanda kwenye makaburi haya na kutambaa chini ya ardhi kupitia vituo hivi vya viwanda badala yake Wanajeshi wa Urusi zibeni eneo hili la viwanda ili hata inzi asitoroke"

Wakati akitangaza ushindi katika udhibiti wa mji huo baada ya karibu miezi miwili ya kuuzingira, Putin amesema hakuna haja ya kujaribu kuwaondoa wapiganaji waliojifungia katika kiwanda hicho kikubwa, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu amesema katika mkutano uliooneshwa kwenye televisheni katika Ikulu ya Urusi kuwa karibu Wapiganaji 2,000 wa Ukraine wamejificha ndani ya kiwanda hicho.

Putin amewataka wasalimu amri akisema Urusi itawashughulikia kwa heshima, Mjumbe mkuu wa Ukraine katika mazungumzo ya amani Mikhailo Podolyak amependekeza kuwa mazungumzo hayo yafanyike ndani ya Mariupol yenyewe kuhusu hatima ya Askari wa mwisho waliobaki mjini humo.
Screenshot_20220421-185230_Instagram.jpg
 
Club ya Manchester United imethibitisha kuwa Erik ten Hag (52) ndio atakuwa Kocha wao mpya baada ya msimu huu kumalizika.

Erik ten Hag Raia wa Uholanzi amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Man United wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Man United ili kukamilisha mchakato huo imelazimika kuilipa Ajax fidia ya pound milioni 1.7 (Tsh Bilioni 5) ili kumchukua Kocha huyo.
Screenshot_20220421-185444_Instagram.jpg
 
Waziri Jenista Mhagama amesoma Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Bungeni Dodoma leo ambapo amesema matokeo ya tafiti zilizofanywa na Taasisi mbalimbali za kitaifa, kikanda na kimataifa kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na rushwa zimedhihirisha kuwa Tanzania inafanya vizuri katika kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi nchini.

"Taarifa ya Transparency International ya mwaka 2021 iliyotoka Februari, 2022; kupitia Kiashiria cha Corruption Perception Index inaonesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwa kupata alama 39 na kushika nafasi ya 87 kati ya nchi 180, ikiwa imepanda kwa nafasi 7 ikilinganishwa na alama 38 katika nafasi ya 94 ya mwaka 2020, kwa mafanikio haya Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki"
Screenshot_20220421-185550_Instagram.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema Walimu walionufaika kwa kupandishwa madaraja (vyeo) katika Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu katika kipindi cha mwaka 2021/2022 pekee ni 92.9% ya Walimu wote ambao ni takribani 260,000.

Deus ametoa kauli hiyo akiwa Mwanza leo ambapo amesema "Ajira imetolewa kwa awamu nne, ya kwanza Walimu 13,000, ya pili 7000, ya tatu 6000 na ya nne ni hii ya juzi 12,000 kwa harakaharaka ni sawa na 15% ya Walimu waliopo"

"Kwa upande wa madaraja (vyeo) mwaka jana Walimu 127,000 wamepanishwa vyeo, mwaka huu zajdi ya 60,000, watakaonufaika na daraja la mserereko ni Walimu 52,0000 ambapo kwa haraka jumla ya walionufaika ma madaraja ni sawa na 92.9%"

"Ukiacha miundombinu ya madarasa/samani na vitabu tayari TAMISEMI imeanza zoezi la ujenzi wa nyumba za Walimu, unaachaje kusema asante kwa Mh. Rais kwa hatua hii kubwa kwa Walimu, Asante Mama"
Screenshot_20220421-185702_Instagram.jpg
 
Serikali imesema ujenzi wa Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara za maingilio (KM 3.8), unatarajiwa kuandika historia kubwa kwa kukamilika kabla ya muda uliopangwa kwenye mkataba.

Ujenzi huu ulioanza mwezi Oktoba, 2018 unatarajiwa kukamilika mapema ifikapo mwezi Julai, 2022 badala ya mwezi Novemba kama ilivyo kwa mujibu wa mkataba wake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati akishuhudia ukamilikaji wa sehemu ya kupita magari (deck) kwenye daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake umefikia 77% "Hii ni hatua kubwa sana kwa Daraja la aina hii, nimejionea linaendelea vizuri na naamini kutokana na kasi aliyonayo mkandarasi kwa hakika daraja hili litakamilika kabla ya muda" Prof. Mbarawa"

Prof. Mbarawa amesema Daraja la Wami la zamani ni jembamba na ni lenye njia moja hivyo magari hupishana kwa zamu kwa kusubiriana, vilevile barabara zinazounganisha daraja hilo zipo kwenye miteremko na miinuko mikali pamoja na kona mbaya na hivyo kupelekea ajali mbaya na vifo ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara katika eneo hilo la daraja.
Screenshot_20220421-185928_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limepiga marufuku, magari yanayosafirisha abiria kufanya safari usiku wa zaidi ya saa sita na kwamba atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Kauli hiyo ya RPC wa Tanga, Safia Jongo imekuja baada ya kujitokeza kwa matukio ya ajali katika barabara ya Tanga - Segera huku baadhi ya madereva wakibainika kughushi nyaraka.
Screenshot_20220421-190023_Instagram.jpg
 
Polisi Lindi wanamtafuta Saidi Haji Ngamila (30) wa Kijiji cha Barikiwa Wilaya ya Liwale kwa tuhuma za kumuua Mke wa Mtu (Mwajuma Ally Lipala miaka 49 ) ambaye alikua Mchepuko wake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali na kutengenganisha kichwa na kiwiliwili na kisha kuchimba shimo na kumfukia.

Mume wa marehemu Rashid Ally Mkumba (69) amesema Aprili 14,2022 yeye na Mkewe walikwenda kwenye shamba lao la mahindi na mihogo kwa ajili ya ujenzi wa kibanda cha kulinda wanyama waharibifu lakini wakati anaendelea na ujenzi Marehemu alimuaga kuwa anakwenda kukata nyasi za kuezekea kibanda lakini hakurudi tena.

Baada ya kutorejea kwa Mke wake, Rashid alikwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ambapo juhudi za kumtafuta zilianza na ilipofika Aprili 16,2022 mwili wake uligundulika kufukiwa pembeni mwa nyumba ya Mtuhumiwa Saidi Haji Ngamila ambapo Kamanda wa Polisi Lindi Mtatiro Kitinkwi amesema uchunguzi wa awali umeonesha wawili hao walikuwa Wapenzi.

Kamanda Kitinkwi pia amesema polisi kwa kushirikiana na ndugu wa Marehemu waliikuta mundu ya kukatia nyasi aliyokuwa anaitumia Marehemu siku aliyotoweka na viatu alivyovaa mara ya mwisho vilikuwa nyumbani kwa Mtuhumiwa.
Screenshot_20220421-190115_Instagram.jpg
 
Mtandao wa Google umezindua kituo cha ukuzaji wa bidhaa jijini Nairobi Kenya ambacho ni cha kwanza katika bara la Afrika ambacho kitakua kikifanya kazi ya kujenga bidhaa na huduma za 'mabadiliko' kwa soko la Afrika na dunia ambapo uzinduzi huu umefanyika baada ya kampuni hii ya Marekani October 2021 kutangaza mipango ya kufanya uwekezaji wa dola bilioni 1 katika miaka mitano ijayo.

Google ilisema itaajiri zaidi ya vipaji 100 vya teknolojia ikiwa ni pamoja na Wahandisi wa programu (software), Watafiti na Wabunifu katika miaka miwili ijayo ili kusaidia kutatua changamoto ngumu na za kiufundi kama vile kuboresha matumizi ya simu kwa Watu barani Afrika au kujenga miundombinu ya mtandao inayotegemewa zaidi.

Google inajiunga na orodha ya makampuni makubwa ya kiteknolojia yaliyoanzisha vituo vya uvumbuzi jijini Nairobi Kenya ambapo wiki mbili zilizopita Microsoft nao walizindua kituo cha utafiti na maendeleo jijini Nairobi, vilevile VISA nayo ilitangaza kuanzisha kituo chake cha kwanza cha uvumbuzi ili kuunda suluhu za malipo na biashara pamoja na Washirika.
Screenshot_20220421-190805_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom