Polisi Tanga wanamshikilia Mkazi mmoja wa Bwembwela Wilayani Muheza kwa tuhuma za kumjeruhi Elias Omari (55) kwa panga mpaka kupelekea kufariki dunia akidai kuwa amemuibia unga na dagaa.
RPC wa Tanga Safia Jongo ameithibitishia @ayotv_ tukio hilo na kusema chanzo ni ugomvi wa kugombania unga na dagaa uliopelekea wawili hao kupigana kwa kutumia mapanga na kusababisha kifo kwa mmoja wao.
Kamanda Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia April 17,2022 na kwamba Mtuhumiwa (30) alijeruhiwa pia katika ugomvi huo na kwa sasa yupo Hospitali teule ya Muheza kwa matibabu zaidi.
Katika hatua nyingine Kamanda Jongo amesema kuelekea msimu wa Sikukuu ya Eid Jeshi la Polisi Tanga linaendelea na operesheni za usalama barabarani ili kuhakikisha Wasafiri wanatumia barabara katika hali ya usalama.
View attachment 2194795