Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,167
Waziri wa TAMISEMI,Innocent Bashungwa Bungeni leo amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Wamachinga katika kukuza uchumi, hivyo amewaelekeza Viongozi wote wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kuhakikisha vitendo vya kuwanyanyasa machinga na kutumia nguvu katika kuwaondoa na kuwapanga ikiwemo kuharibu bidhaa zao kama ilivyotokea kwa Jiji la Mwanza vinakomeshwa.
"Katika kuboresha miundombinu ya kufanyia biashara kwa Wamachinga, Serikali imechukua ya kuwapanga Machinga kwenye maeneo rasmi kwa utulivu pasipo kutumia nguvu katika Halmashauri zote zilizokuwa na machinga wengi kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa.
"Hatua nyingine iliyochukuliwa ni Serikali kutoa Shilingi bilioni 5.0 kwa ajili ya kuboresha maeneo ya kufanyia biashara machinga katika Halmashauri 11, hatua nyingine inayoendelea ni kuwepo kwa majadiliano na Wizara ya Fedha na Mipango ili kufanya marekebisho ya Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290 ili kuruhusu sehemu ya fedha za Mikopo ya 10% kutumika katika kuboresha miundombinu ya Machinga.
"Marekebisho ya Sheria hii yanapendekezwa kufanyika kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022, majadiliano hayo yakikamilika, tunatarajia kiasi cha Shilingi bilioni 38.01 zitapatikana kupitia mlango huo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Wafanyabiashara Wadogo (Machinga)"