Makapuku Forum

Makapuku Forum

Club ya Simba SC kupitia kwa CEO wao Barbara Gonzalez leo imetangaza kuomba ulinzi kwa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakiwa wanaelekea Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa robo ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni siku mbili zimepita toka Kocha Msaidizi wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi kuituhumu Simba SC kwa mambo kadhaa ikiwemo mapokezi mabovu, kukosa ukarimu na madai ya VAR kutofanya kazi.View attachment 2193603View attachment 2193604View attachment 2193605
Ulinzi wa nini? Wakawatende sawasawa na matendo yenu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji3578][emoji3578] Zakazakazi

Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo.

Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita.

Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF [emoji122][emoji122][emoji122]!

Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo.

Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu.

Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama watafika nusu fainali wanaweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

Na kama itakuwa hivyo, wanaweza kuingia 10 bora na kupata moja kwa moja haki ya kuanzia raundi ya pili ya mchujo.

Lakini kama watatolewa na Orlando Pirates, basi watabaki katika nafasi ya 12 na kuomba zali kama la msimu huu...yaani wa juu yake wasifuzu ligi ya Mabingwa.

Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchi mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani.

Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA![emoji35]

Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Anyway, Mwenyezi Mungu ni wa wote!
Screenshot_20220420-141429_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom