Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,167
Wakati Mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani yakiendelea kutuma silaha
kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi, China imesema kuipa Ukraine silaha kunachochea vita na kutoa wito kwa Mataifa mbalimbali kuweka nguvu kubwa kwenye kumaliza vita na sio kuchochea.
Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, Zhang Jun amezitaka Urusi na Ukraine kufanya majadiliano ya amani na kumaliza vita huku akizitaka Nchi nyingine kushiriki kuleta amani badala ya kuendelea kuipa Ukraine silaha za kivita.
Kauli ya China inakuja wakati huu ambapo tayari Ukraine imepokea ndege za kivita kutoka Marekani kwa ajili ya kujilinda katika uvamizi unaofanywa na Urusi nchini humo huku Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskiy akiendelea kuitaka NATO itume msaada wa ndege za kivita nchini humo.
Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema nchi hiyo itaipa msaada wa silaha nzito za kijeshi Ukraine kufuatia wito wa msaada uliotolewa na Rais Zelenskiy.