Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220420-040654_Instagram%20Lite.jpg
 
Club ya Simba SC kupitia kwa CEO wao Barbara Gonzalez leo imetangaza kuomba ulinzi kwa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakiwa wanaelekea Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano wa robo ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni siku mbili zimepita toka Kocha Msaidizi wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi kuituhumu Simba SC kwa mambo kadhaa ikiwemo mapokezi mabovu, kukosa ukarimu na madai ya VAR kutofanya kazi.
Screenshot_20220420-042454_Instagram.jpg
Screenshot_20220420-042523_Instagram.jpg
Screenshot_20220420-042547_Instagram.jpg
 
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi wamesema wanaendelea kuchunguza kwa kina kifo cha Padri Francis Kangwa (49), Raia Zambia aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mbezi Mshikamano iliyopo Wilaya ya Ubungo, Dar es salaam aliyekutwa amefariki ndani ya Tenki kubwa la maji lililoko nyuma ya nyumba ya makazi ya Mapadri iliyopo Mtaa wa Sokoine katika jengo la Ottoman, Dar es Salaam.

"Padri huyo alifika katika Kanisa la 'St. Joseph' lililopo Mtaa wa Sokoine April 12,2022 kwa ajili ya ibada maalum, na mara baada ya ibada alielekea kwenye makazi ya Mapadri kujipumzisha lakini hakuonekana mpaka April 15,2022 alipokutwa amefariki eneo hilo"

"Uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi unaonesha dalili kwamba Padri huyo anaweza kuwa amejiua, hata hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi iliyopelekea kifo cha Padri huyo"
Screenshot_20220420-043218_Instagram.jpg
 
Ofisi ya Rais- TAMISEMI imewataka Wananchi wapuuze tangazo la ajira za Ualimu na Afya ambalo linasambaa na kusema TAMISEMI haihusiki na maudhui yaliyopo kwenye tangazo hilo "Tunatambua uhitaji wa ajira uliopo hivi sasa na mara tu tutakapokamilisha mchakato tutatangaza ajira hizo kupitia vyombo vya habari, tovuti ya TAMISEMI pamoja na mitandao yetu yote ya kijamii"

"Wahalifu tumeshawaripoti kwenye Mamlaka zinazohusika wanafuatilia na watachukuliwa hatua Stahiki, kwa sasa tunaomba tuendelee kuwa watulivu wakati huu ambao tunakamilisha taratibu na ajira zitatangazwa karibuni"
Screenshot_20220420-043426_Instagram.jpg
 
Baada ya kuenea kwa taarifa kwamba Urusi imetangaza fursa kwa Vijana wa Mataifa mbalimbali kujiunga na Jeshi la Urusi ili wakapigane na Jeshi la Ukraine, Vijana wa Ethiopia wanaendelea kukusanyika katika Ubalozi wa Urusi nchini Ethiopia ulipo Mji Mkuu Addis Ababa, wakichangamkia fursa hiyo.

Wakati Vijana hao wakiendelea kukusanyika kwa wingi Ublaozini hapo, Msemaji wa Ubalozi huo, Maria Chernukhina, amesema hakuna ajira zinazotolewa kwenye Ubalozi huo nchini Ethiopia na kusema taarifa hizo ni uvumi tu.

"Tuna wageni wengi katika ubalozi huu wanaokuja kuunga mkono Urusi na baadhi yao wanasema wako tayari kusaidia kwa njia yoyote wanayoweza lakini sisi sio wakala wa kuajiri"

Baadhi ya Vijana hao wa Ethiopia katika ubalozi huo walionekana wakiwa na hati zao za kibinafsi, Vijana wa Ethiopia wamesema wanatafuta mshahara mzuri kama kuwa Wanajeshi au kuajiriwa katika kazi nyingine yoyote inayopatikana huku wakisema wamesikia fununu za mishahara mikubwa nchini Urusi.
Screenshot_20220420-043619_Instagram.jpg
 
Mwanaume mmoja wa Kentucky nchini Marekani amelipwa USD 450,000 baada ya kampuni yake kumfanyia tafrija ya kushtukiza (suprise) ya siku ya kuzaliwa kwake licha ya onyo alilolitoa kuwa ingeweza kumsababishia msongo wa mawazo na hofu.

Mlalamikaji, Kevin Berling, anadai kuwa tafrija ile ambayo hakuitaka ya siku ya kuzaliwa ya mwaka 2019 ilimsababishia matukio kadhaa ya kuwa na hofu, madai ya kesi ya Berling yanadai kuwa kampuni hiyo ilimbagua kwa sababu ya ulemavu wake, Kampuni hiyo imekanusha kufanya jambo lolote baya.

Kwa mujibu wa kesi iliyowasilishwa katika Kaunti ya Kenton, Kentucky, Berling ambaye ana matatizo ya kuwa na wasiwasi alimwomba Meneja wake asisherehekee siku yake ya kuzaliwa kazini kama ilivyo kawaida kwa Wafanyakazi wengine kwasababu inaweza kumsababishia mashambulizi ya hofu na kurejesha kumbukumbu zisizofurahi za utotoni ambapo licha ya ombi la Berling, kampuni hiyo, ambayo hufanya vipimo vya Covid-19, ilimfanyia sherehe ya kushtukiza Agosti 2019, na kusababisha shambulio la hofu.

Haraka alitoka kwenye sherehe na kumalizia chakula chake cha mchana kwenye gari lake, kesi hiyo inabainisha kuwa Berling alishutumiwa na kukosolewa katika mkutano siku iliyofuata, ambapo alishutumiwa kwa kutowafurahisha Wafanyakazi wenzake.

Mkutano huo wa mvutano ulisababisha shambulio la pili la hofu, baada ya hapo kampuni ikamrudisha nyumbani kwa muda uliosalia wa Agosti 8 na 9 Agosti.
Screenshot_20220420-043738_Instagram.jpg
 
Baadhi ya Wafungwa wa Gereza la Kamiti nchini Kenya lenye Wafungwa takribani 2500 wamebainika kufanya vitendo vya utapeli wakiwa Gerezani, Wafungwa hao wameoneshwa kupitia makala maalum ya Citizen TV wakiendesha shughuli zao za utapeli kwa Raia ambao wapo uraiani nchini Kenya.

Wafungwa hao matapeli wanaishi maisha yasiyo ya kawaida Gerezani wakitumia simu kuwatapeli Wakenya kibiashara au hata kifamilia, Walengwa wa utapeli huo pia ni Watu wanaoishi Mataifa ya nje kama Somalia na Raia wengine wa Kenya ambao wamethibitisha kupigiwa simu na kutapeliwa na Wafungwa hao.

Simu zinazotumika na Wafungwa hao zina uwezo wa kubadilisha sauti kuwa ya kiume, sauti ya kike au hata ya Mtoto.
Screenshot_20220420-043858_Instagram.jpg
 
Meya wa jiji la Moscow nchini Urusi, Sergei Sobyanin amesema takribani Wafanyakazi 200,000 wa makampuni ya kigeni wanakabiliwa na hatari ya kupoteza ajira zao kutokana na vikwazo ilivyowekewa Urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.

Sobyanin amesema wiki iliyopita, mamlaka iliidhinisha mpango wa dola milioni 41 kusaidia ajira katika mji mkuu wa Urusi na kwamba mpango huo unalenga Wafanyakazi wa makampuni ya kigeni ambayo yamesimamisha shughuli zao kwa muda au kuamua kuondoka nchini Urusi.

Mamia ya makampuni hasa ya Magharibi yametangaza kusimamisha shughuli zao au kuondoka nchini Urusi baada ya Rais Vladimir Putin kutuma Wanajeshi wake nchini Ukraine mnamo Februari 24.

Wataalamu wa uchumi wanaamini kwamba, vikwazo zaidi dhidi ya Urusi vinatarajiwa na hivyo kuitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi.
Screenshot_20220420-044028_Instagram.jpg
 
Madereva wa daladala zinazofanya safari kati ya Mlowo na Tunduma mkoani Songwe wamesitisha huduma za usafirishaji wa abiria wakidai wanasubiri tamko la Serikali la kupandisha nauli.

Madereva hao wamesiitisha huduma leo Jumanne Aprili 19, 2022 huku wananchi wakiteseka kutafuta njia mbadala kufika maeneo mbalimbali.

Baadhi ya abiria wamelazimika kutumia usafiri wa bajaji na bodaboda kufika kwenye maeneo wanakofanya shughuli zao.
Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva wa Haice za Tunduma na Mlowo, Fadhili Bernad amesema wameanza mgomo huo baada ya kuona ukimya wa Serikali kutotoa tamko lolote juu ya bei elekezi ya nauli za daladala kutokana na ongezeko la bei za mafuta ya dieseli na petroli.

Mwananchi imeshuhudia umati wa abiria katika kituo cha daladala cha Mpemba waliokwama kuendelea na safari kwenda Tunduma.

Screenshot_20220420-044149_Instagram.jpg
 
KLABU ya soka ya Simba imesikitishwa na shutuma za uongo za kocha msaidizi wa timu ya Orlando Pirates Mandla Ncikazi alizozitoa baada ya mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika ambapo Orlando ilipoteza kwa bao moja kwa bila.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez timu hiyo imechukizwa na maneno kashfa yaliyotolewa na Kocha Ncikazi ambayo yanatanabaisha ukosefu wa taaluma na ukiukwaji wa maadili katika kazi yake ya ukocha.

Maneno ya Kocha huyo yanakinzana na ukweli ambao Simba tumekua tukiiushi kwa kutoa huduma bora kwa wageni wote wanaokuja kucheza nasi hapa Tanzania.
“Simba tulishangazwa na vitendo vya Orlando tangu kuwasili kwao Tanzania ambapo kama wenyeji tuliandaa mazingira yote rafiki kwa ajili yao ikiwemo Usafiri wa Basi kubwa, na gari ndogo lakini kwa sababu zao walikataa kutumia huduma tulizowaandalia”
Screenshot_20220420-044357_Instagram.jpg
Screenshot_20220420-044421_Instagram.jpg
Screenshot_20220420-044441_Instagram.jpg
 
ULIMWENGU MAMBO MAGUMU MAZEMBE !!
.
Mshambuliaji wa Kitanzania, Thomas Ulimwengu [emoji1241] anatakiwa kuongeza makali yake maana zipo ripoti kuwa kocha mkuu wa Tp Mazembe, Mihayo Kazembe [emoji1078] havutiwi na kiwango chake cha sasa tofauti na mambo yalivyokuwa msimu uliopita ambapo alikuwa moto wa kuotea mbali.
Screenshot_20220420-050247_Instagram.jpg
 
Kuna muda zilitoka taarifa kuwa sehemu ya paa la Old Trafford linavuja kutokana na miundombinu mibovu na hakuna matengenezo kwa muda mrefu

Kuna muda ikaonekana Mchumi Ed Woodwrd ni kipenzi cha Maboss kutokana na faida anayozalisha, nadhani changamoto kubwa United wala sio Makocha ni mfumo wa utawala na umiliki

Hivi Eric Ten Haag atakuja kutafuna mfupa uliomshinda David Moyes, LVG, Mourinho, OGS mpaka sasa Ralph? Binafsi sina uhakika kama watawala na wamiliki ni wale wale
Screenshot_20220420-050718_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Ikatokea tu mfano Simba anatolewa kule Afrika Kusini na Orlando Pirates

Ikatokea tu timu zote nne ambazo zimefuzu kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao kutokana na mafanikio ya Simba zote nne zikafanya tu vibaya

Ikatokea kwa mfano zote nne zimetoka raundi ya kwanza, ikatokea Libya wamesogea na Nigeria wakatuzidi alama wakapeleka timu nne sisi tukazidiwa, unaonaje hiyo?

Yani sote tukishakuwa wa hapa hapa, tunapishana humu humu, unahisi kuna uwekezaji wa maana utaendelea kwenye sehemu hakuna faida?

Ziko wapi leo hii Gor Mahia na FC Leopards? Leo hii wapo kwenye ramani ya soka la Afrika? Zipo wapi tambo za Wakenya kwenye michuano ya Afrika? Zipo tena?? Vipi thamani ya ligi yao, ipo tena? Vipi kuhusu mpira wao kwa ujumla?

Mfano tu tukaipiga vita Simba kisha Mungu akaitikia dua zetu, kwahiyo tupo tayari kuwa kama Majirani? Tupo tayari kuona hata Wadhamini wanaoongezeka kisa thamani waondoke? Tunatamani hicho?

Leo hii Real Madrid na Barcelona wamesaini mkataba wa kuungana pamoja kwa kila kinachoitwa maslahi, leo hii PSL (Bodi ya ligi ambao ni mjumuiko wa klabu) pale Afrika Kusini, jambo la Pirates ni jambo la wote

Hakuna cha maana kwenye chuki, mwisho wa siku sote tukibaki hata kicheko kitaisha, hata tambo zitaisha, zitasalia Majuto mengi ambayo ndio Mjukuu

Jitazame tu unayo nafasi yako kwenye mpira wa hii nchi, kama huwezi kwa ajili ya Simba basi fanya kwa ajili ya bendera na nembo ya Visit Tanzania kifuani mwao

Unaweza kuniona Mshamba, unaweza kuniita Mshabiki sana au wa mchongo ukipenda ila hujachelewa sana kuutazama mpira kwa jicho yakinifu

“Dhambi ya ubaguzi haiwezi kuisha ni sawa na kula nyama ya Mtu” Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Screenshot_20220420-053612_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom