Makapuku Forum

Anaitwa Szymon Marciniak, raia wa Poland ndie Mwamuzi wa mchezo wa leo kati ya Real Madrid na Chelsea, hatua ya robo fainali

Huyu bwana leo ni mara yake ya tano kuchezesha mechi za Real Madrid, ikiwa pia ni mara ya pili ndani ya msimu mmoja, alichezesha mechi muhimu ya Madrid vs Sherrif pia

Mechi nyingine ni;

Real Madrid vs AS ROMA
Real Madrid vs Dortmund
Real Madrid vs Tottenham
Real Madrid vs Sherrif

Lakini ikumbukwe alichezesha fainali ya SUPERCUP kati ya Real Madrid na Atletico Madrid msimu wa 2018/19

Leo tena yupo mzigoni

Photo Credit: Ian Cook via Getty Images
 
Hii mipira inaitwa ADIDAS FINALE 21 au Adidas Finale Pyrostorm, ndio mipira rasmi kwa ajili ya UEFA Champions League msimu wa 2021/22

Hii imepangwa tayari pale Bernabeu na inasubiri filimbi ya Mwamuzi
 
Tunaendelea kukumbushana tu kuwa usiku wa mwisho wa Ulaya pale Bernabeu au THE MUSEUM OF EUROPEAN FOOTBALL, Yes wenyewe wanapenda kupaita Makumbusho ya soka la Ulaya, hichi ndicho kilimkutaka PSG

Usiku wa leo tena ni Chelsea dhidi ya LOS GALACTICOS
 
Klabu ya Villareal inatokea Mashariki mwa nchi ya Hispania, mji wa Castellon ambao kwa mujibu wa sensa ya 2018 idadi ya watu kwenye mji huo ilikuwa 174,264

Wakati dimba la Bayern Munich yani Allianz Arena inaingiza mashabiki 75,024 ambapo leo wanaumana hapo Bavaria, kusini mwa Ujerumani

Usiku wa mabingwa jioni ya leo

 
Real Madrid wamefunga mabao 93 msimu huu, ambao mabao 54 kati ya hayo yamefungwa na Karim Benzema pamoja na Vinicius Jr

 
JE WAJUA?
|

Bablish (Chewing gum) ya mwisho ambayo Sir Alex Ferguson alitafuna kwenye mchezo wa EPL, kati ya Manchester United na West Brom iliuzwa kiasi cha Pauni 390,000 ambazo ni zaidi ya BILLION 1.1 za kitanzania

Ambapo thamani yake ni zaidi ya gari aina ya Lamborghin Aventador
 
“Kwa umri wa Cristiano, kufunga mabao zaidi ya 18 tena kwenye ligi ngumu kama EPL ni wazi anaendelea kuonesha ubora wake, sio rahisi kwa umri wake ndani ya EPL” Dimitar Berbatov
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere amewasilisha ripoti kwa Waandishi wa Habari leo ambapo ameyataja mapungufu ya udhibiti kwenye mfumo wa madai wa Mfuko wa Bima ya Afya ikiwemo madai 56 yanayoonesha Wanaume walipata huduma ya upasuaji (C/S) au huduma za kawaida za kujifungua wakati huduma hizi hutolewa kwa Wanawake, pia Wanachama 444 waliopata huduma ya kuchunguzwa picha kamili ya damu (full blood picture) zaidi ya mara moja kwa siku moja (hadi mara 30) kwenye kituo kimoja.

"Aidha, kuwapo kwa malipo ya madai yaliyorudiwa, pamoja na madai yanayoonesha wanachama wa NHIF waliopokea miwani ya kusomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja kwa mwaka"

"Udhaifu huu umesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika mfumo wa madai iliyosababisha hasara ya Sh. Milioni 14.41 kwa mfuko"

"Ninapendekeza kwamba Mfuko wa Bima ya Afya: (a) Kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa watoa huduma za afya husika; na (b) Kuboresha mfumo wa madai wa CMIS ili kuhakikisha kuwa unasaidia maafisa wanaohusika kuangalia uhalali wa madai yaliyowasilishwa"
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere amewasilisha ripoti kwa Waandishi wa Habari leo ambapo ameyataja Mashirika ya kibiashara yaliyopata hasara kwa miaka miwili 2019/20 na 2020/21 "Mashirika 14 ya kibiashara yalipata hasara mfululizo, hali hiyo ilisababishwa na hasara kwenye uwekezaji uliofanywa, ufanisi duni wa mashirika husika, na udhibiti hafifu wa mapato na matumizi"

"Mashirika hayo ni ATCL, Mkulazi, TTCL, Kituo cha Mikutano Arusha, EPZA, Watumishi Housing na Kampuni ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam"

"Naomba nifafanue kuhusu mwenendo Kampuni ya Ndege Tanzania, mwenendo wake umeimarika ukilinganisha na mwaka uliopita kwa sababu kwa mwaka 2020/21, kampuni iliongeza mapato kwa asilimia 11 na kupunguza matumizi kwa asilimia tatu"

"Hivyo, Kampuni ilipunguza hasara ya jumla kutoka Sh. bilioni 60.25 mwaka 2019/20 hadi kufikia Sh. bilioni 36.18 mwaka 2020/21"
 
Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne.

Mtuhumiwa huyo Latifa Bakari (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa Mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi Mtoto huyo.

Baada ya kubaini kuwa Mtotl huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa Mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side Ubungo.

Baada ya majirani kutomuona Mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa, mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.
 
Twitter imefungia kwa muda akaunti ya Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Uganda, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni Mtoto wa Rais Yoweri Museveni "Siku ya Jumatatu (Aprili 11), Twitter ilisimamisha akaunti ya Muhoozi kwa sababu zisizoeleweka"

Jenerali Kainerugaba hapo awali alikuwa amepost ujumbe kwa Wafuasi wake zaidi ya 500,000 kwenye Twitter akidai kwamba alikuwa akilengwa na kampuni kubwa za teknolojia".

Kamanda huyo anatajwa kuwa anatarajiwa kuwa mrithi wa Baba yake kwenye kiti cha Urais Uganda na amekuwa uongozini kwa muda mrefu na mtumiaji mahiri wa Twitter.

Jenerali Kainerugaba amekuwa akichapisha maoni ambayo yanaweza kuonekana kuwa ya kutatanisha, hivi karibuni aliwaonya wezi wa ng'ombe katika eneo lenye utajiri wa madini la Karamoja kwamba uvumilivu wa jeshi umepungua na wangewakabili.

Kamanda huyo aliwahi pia kutoa msimamo wa kuiunga mkono Urusi dhidi ya uvamizi wa Ukraine .
 
• Vijana 7 katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita mkoani GEITA wamekamatwa na Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Ulinzi Shirikishi kwa tuhuma za kutumia silaha za jadi na dawa za kienyeji (ushirikina) kuiba na kupora mali kwa Wananchi.

Kamanda wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kitongoji cha Ludete, kata ya Ludete Zablone Peter amesema wengine wamekamatwa wakiwa na mapanga ambayo huwa wanayatumia kwa uhalifu.

Mmoja ya Watuhumiwa hao Mayala John amekiri kuwa vitu anavyotumia kufanyia wizi ni mkasi kwa ajili ya kufungulia milango pamoja na dawa za kienyeji kama sehemu ya kinga “Dawa ninazozitumia ni za kuoga na pia unaweza ukazitumia kuosha ule mkasi kisha ndio tunaenda kufanya kazi japo dawa hiyo haifanyi kazi kama kuna kufuli mlangoni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…