Makapuku Forum

Simba, Pamba kusogezwa mbele
.
Mchezo huo ulipaswa kuchezwa Aprili 13 mwaka huu saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Hata hivyo imeelezwa kuwa mchezo huo umehairishwa na utapangiwa tarehe mpya baada ya wenyeji Simba kuomba kwa ajili ya kupata muda wa kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini utakaopigwa Aprili 17 jijini Dar es Salaam.
 
Simba yapewa Mashabiki 60,000 dhidi ya Orlando !!
.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeruhusu Simba kuingiza idadi hiyo ya mashabiki baada ya kupeleka ombi CAF.
 
Shaffih Dauda

Nilisema kitu kuhusu thamani ya Mchezaji na namna gani ambavyo anaweza kutengeneza pesa kupitia thamani yake, nilisema kuhusu mikataba lakini pia kuhusu corporates

Nilisema Mchezaji ni vyema akawa na viungo muhimu zaidi kwake, ambao ni WAKALA na Mwanasheria, kwakuwa hizi ni field muhimu zaidi kwenye football

Kwanini wachezaji wetu wengi wazawa wamekuwa wakilia kuhusu mikataba, kuhusu pesa wanazolipwa na wengi wakiamini hawapewi thamani kama wapewavyo wageni?

Majibu ni kuwa wanakosa Professionals wa kusimama kwa niaba yao! Mchezaji wetu anachojua ni kusaini na kuchukua pesa kisha kuondoka, hapitii mkataba, hasomi kilichomo yeye anaanguka tu saini

Wakati mwingine Mchezaji hafahamu hata umuhimu wa kutia saini kila page yake ya mkataba, wakati mwingine Mchezaji hapitii vifungu (clause) za kimkataba, ambazo zingine ni kandamizi

Mfano wengi hujifunga kwenye IMAGE RIGHTS (Haki za picha zao) nyingi hutumika bureee, wengi hujikuta wakipromote bidhaa ambazo dunia ya kimpira kwasasa zinaenda kwa mfumo wa comission, lakini huku ni ngumu kwakuwa hatuna watu muhimu nyuma yetu

Huku kwetu Mchezaji anacheza akiwa na stress kuwa anamaliza mkataba, akiwa na stress za pesa nzuri (Greener pasture) lakini vyote hivyo anapaswa kupigana mwenyewe, lakini ukiwa na WAKALA yeye anasimama kwa niaba yako kwakuwa ni Business, deals anakuwa nazo tayari

Ukiwa na Mwanasheria wako yeye ndie mtu wa kukutafsria kilichomo kwenye mkataba, yeye atakuelekeza kuhusu muhimu wa INITIALS kila ukurasa, yeye ndie anajua utaondoka vipi ukiwa ndani ya mkataba, hizi zote ndio dunia ya mpira

Mmoja atasema wachezaji hawana pesa ya kuwa na watu wote hao! Well simple, lakini mfumo wa dunia hivi sasa ni partnership, watu watasimamia deal na kuvuna kitu kutokana na deal, baada ya hapo watapambana tena

Tuwaambie kweli wachezaji wetu, mikataba ni CONFIDENTIAL sana, inahitaji akili sana ili kupata maslahi ya kimpira, nje na hapo tutaendelea kulalamika tu, WE NEED TO CHANGE

WHEN DIGALA SPEAK YOU LISTEN

 
Wakati Ligi ya NBC msimu huu [2021|22] Polisi Tanzania ilishaongoza Ligi, lakini taratibu timu imekuwa ikitoka kwenye nafasi za juu na sasa hivi ipo nafasi ya tisa (9) ikiwa na alama 23 sawa na KMC.

Kocha Msaidizi wa Polisi George Mketo ameeleza sababu ambayo inewafanya kushindwa kubaki kwenye nafasi ambazo walikuwa wamejiwekea malengo.

“Ligi sio nyepesi ligi ni ngumu, kwa namna ambavyo tulianza mwanzo, tulitarajia kuendelea hivyo na ndio malengo yetu. Malengo ya timu na Jeshi kwa ujumla ni kumaliza katika nafasi tatu za juu na malengo hayo bado yapo.”

“Kwa nafasi tuliopo na wale ambao wapo juu tofauti ya pointi ni chache kama tatu au nne. Naamini kwenye michezo iliyobaki tutapambana ili turudi kwenye nafasi tatu za juu.”
 
Mwanzoni nilihisi ilikuwa labda agenda ya kuzipa trend tuzo za Oscar, lakini haikuwa hivyo na wala haikuwa script, ni kweli Will Smith alicatch feelings na kumuadhibu comedian Chris Rock

Leo hii Academy imetoa hukumu kuwa Smith amefungiwa miaka 10 kutoshiriki shughuli zozote za Academy nae amekubali adhabu hiyo
 
Bado hatujakata tamaa, bado malengo yetu yapo vilevile, tumesaliwa na michezo 12 mbele, malengo yetu ni kushinda kila mchezo yote iliyopo mbele yetu na hatimaye mwisho wa msimu tutaangalia tuna nini mkononi. Hayo ni malengo ya kwenye Ligi ya NBC.

Tuna malengo sawasawa na kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports sambamba na Kombe la Shirikisho Afrika, ni kuto poteza hata mchezo mmoja.

- Ahmed Ally [@AhmedAlly_] kuhusu Malengo ya Simba.
 
Ni rahisi kusema WAZAWA hawathaminiki ila huu ni MCHAKATO

Huwezi kupata thamani kama Kiongozi wa timu inayokutaka anaongea na wewe, hufahamu sheria, hufahamu biashara, unachofahamu ni kwenda kusaini tu, hapo ni ngumu kupiga hatua
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…