Makapuku Forum

MASHABIKI EVERTON HAWAMTAKI LAMPARD
.
Mashabiki wa Everton wanashinikiza mabosi wa klabu hiyo kumfukuza kocha Frank Lampard baada ya kipigo cha mabao 3-2 walichopata kutoka kwa Burnley ambayo ipo hatarini kushuka daraja msimu huu.
.
Lampard aliteuliwa kuwa kocha wa Everton mwishoni mwa mwezi Januari, lakini tangu alipotua kocha huyo wa zamani wa Chelsea hakuna alichobadilisha kwani imepoteza mechi sita mfululizo tangu alipopewa timu.
.
Everton haijawahi kushuka daraja tangu mwaka 1951, lakini sasa inaonyesha kila dalili za kuporomoka hadi Ligi Daraja la Kwanza ikiwa imejikita nafasi ya 17 kwenye msimamo wa EPL alama moja juu ya Burnley.
 
BANDA: PIRATES WAMTUMIE SENZO
.
"Ninachojua ni kwamba Pirates watafuzu na kuingia nusu fainali baada ya mechi hizo mbili. Ingekuwa hatari kama Pirates wangeaza kucheza Johannesburg (nyumbani) kwanza.
.
"Pirates lazima wamtumie Senzo(Mbatha) kwa safari ya kuja Tanzania kwa sababu anaijua Tanzania vizuri sana na alikuwa Simba kabla na sasa yupo Yanga.
.
"Yanga watafurahi kuwasaidia Pirates katika chochote wanachohitaji kwa sababu ni maadui wa Simba," amesema Banda via KickOffMagazine
 
DUHH!! BANDA AIPAKA MATOPE SIMBA
.
"Orlando Pirates wanapokuja Dar es Salaam, lazima watarajie kukutana na vitendo vichafu na wajue kwamba vita itakuwa nje ya mpira kwa sababu Simba anaungwa mkono na wanasiasa.”
.
"Simba watabebwa na mwamuzi kwa sababu watampa fedha. Simba utumia mbinu chafu wanapocheza nyumbani, lakini kiukweli hawana Ubora ambao Pirates anao na ili waweze kufuzu watajipanga kupata ushindi mkubwa nyumbani.”

- Abdi Banda via @kickoffmagazine
 
MAYELE: NAAMINI KATIKA UWEZO SIO MIKOSI
.
Katika kikosi cha Yanga, jezi namba 9 ilipewa jina la ‘Jezi ya Moto’ na anayeivaa lazima msimu uwe mbaya kwake na ataondoka tu. Ndani ya kikosi cha Simba haitumiki kabisa. Hakuna mchezaji anayeitaka. Kwa Mayele ambaye ni msimu wake wa kwanza Yanga imekuwa tofauti kwa sababu tayari ameifungia timu yake mabao 11 akiwa ametupia jezi namba 9.
.
“Mwanzo nilikuwa navaa jezi namba 10 kutokana na idadi ya watoto tuliozaliwa ndani ya familia, lakini baada ya kuondokewa na dada yangu na kubaki tisa nikaamua kubadili namba ambayo ndio naitumia hadi sasa,”
.
“Sina imani na utaratibu uliopita ndani ya Yanga kwamba namba tisa ina mkosi, kwa sababu naamini katika uwezo kwani namba na uwezo haviingiliani. Mbona navaa naanza kikosi cha kwanza na nafunga.”
 
SIMBA YATOA WANNE KIKOSI BORA CHA WIKI CAFCC
.
1. Hamza Akbi (Berkane)
2. Mahmoud Ghorbel (CS Sfaxien)
3. Dimitri Bisiki (AS Otoho)
4. Enock Inonga Baka (SIMBA SC)
5. Ismail Mokadem (RS Berkane)
6. Addam Bosu (TP Mazembe)
7. Abdallah El Said (Pyramids)
8. Sadio Kanoute (SIMBA SC)
9. Chriss Mugalu (SIMBA SC)
10. Mohamed Zougrana (Asec)
11. Bernard Morrison (SIMBA SC)

………
 
Shaffih Dauda

Kwenye nchi kama Tanzania kuna michezo mingi na wanamichezo wengi sana, hoja yangu ni kiwanda cha michezo kama biashara nje ya uwanja, uringo au court

Kampuni zinawekeza pesa au kutoa mikataba ya wadhamini kwa kutazama, POTENTIAL ya mchezo husika, RASILIMALI ya mchezo husika na mwisho MODE OF THE SPORT, nikimaanisha ni mtu mmoja mmoja au ni timu?

Hiyo ni sehemu ya kwanza, sehemu ya pili ni kuwa ICON IN SPORTS, yani kwenye michezo hiyo ni Staa?? Hapa watu hupenda kutumia neno COUNTRY STAR, mfano kwenye Football hii Tanzania tuna Mbwana Samatta ambaye alikuwa na endorsement na kampuni ya vinywaji

Kwenye country star kuna vingi wanavitazama, lakini inaweza kutokea nchi ikawa na Mastaa wengi tu na watu wakawatumia kama nembo zao kibiashara na kujipigia pesa nyingi nje ya mchezo wao

Mfano kwenye boxing namtazama sana Hassan Mwakinyo namna anavyojitofautisha, Boxer kama huyu ni rahisi kuwa COUNTRY STAR kwenye mchezo wake, nakumbuka aliwahi kuwa na mkataba mzuri sana na kampuni moja wapo nchini, anajibrand sana

Kuna kitu wanamichezo wetu wanapaswa kukibadilisha, kuamini ukiwa na Management basi pesa hupati nyingi ila HAPANA, unahitaji kuwa na watu wanaopush vitu vyako binafsi na kusimama kwa niaba

Wengi huamini jina ndio linauza hiyo ni HAPANA, kwenye dunia yetu Kampuni hufanya kazi na Wataalam, mfano Mtu wa masoko wa mchezaji anaweza kudraft proporsal akaipeleka kwenye kampuni kadhaa kisha akaidefend, mnapata endorsement nzuri tu

Kosa ni kuamini kuwa Kampuni zinafuata jina, kampuni zinafuata system na profesionalism, ikitokea tofauti wakupigie mchezaji ambaye una majukumu labda kuelekea kwenye game? Jibu ni HAPANA, wanaconsult na Menejiment au muwakilishi wako

Tumia akili kidogo, mpe mtu kazi, mpe copyrights zako akasake endorsement kisha mnagawana asilimia flani, hivi mnafahamu kuwa Ronaldo na Mendes hivi sasa ni Business Partners?? Mendes analeta dili, wanagawana percent na maisha yanaenda

Kama Ronaldo anafanya kwanini sio wewe? The corporate world works differently from streets

DIGALA WAS HERE
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…