[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Naam kwasasa nipo kwenye Mahakama wa mpira baada ya kukamatwa usiku wa jana kuwa nimedanganya umma wa Tanzania
Kesi yangu haina dhamana wamesema, hivyo baada ya jana kukaa lock up pamoja na Azam FC, Police Tanzania, Coastal Union, Mbeya Kwanza, Namungo, Mtibwa ambao wao wapo pia kwa makosa yao
Nimeambiwa nijiandae kusimama mbele ya Jaji Mfawidhi, kuelezea au kujitetea ule ulioitwa uongo! Nilisema Yanga jana ameshinda El derby de Mzizima bila KHALID AUCHO (Mahakama nzima imeshika kichwa)
Nikasema pia Yanga imeshinda bila FEISAL SALUM (Jaji nikamuona ananukuu vitu huku akiwa amekasirishwa na ule uitwao uongo wangu (Mahakama nzima inasikitika)
Nikaendelea kusema PAS DE YANNICK BANGALA, PAS DE PROBLEME, (Nikaona jopo la Wanasheria upande wa Jamhuri wananong’onezana) ghafla wakasema nitafsiri hiyo kauli yangu kwa Kiswahili
Kwa unyenyekevu mkubwa mbele ya Jaji nikajibu PAS DE BANGALA, PAS DE PROBLEME! Maana yake ni kuwa HAKUNA YANNICK BANGALA, HAKUNA TATIZO (Ghafla Mahakama nzima wakiwemo ndugu zangu walishika vichwa kuwa naendelea kuongopa mahakamani)
Baada ya ukimya basi Wakili upande wa Jamhuri aliniuliza swali, “Ndugu Farhan Kihamu, ni kweli kuwa hukuwa umelewa ama kutumia Bob Marley wakati unatoa kauli hizo?” Maana Wakili wako amekutetea hivyo
Kwa utulivu tena na unyenyekevu mbele ya Jaji, nikajibu, “Kwanini niwe muongo, kwanini niseme tofauti mbele ya Mamlaka? Nikiendelea kusema wameshinda bila Kibwana Shomari, bila Farid Mussa, mtanielewa”? (Mahakama yote vilio na Jaji akawa anafuta miwani)
Baada ya ukimya, ndipo Jaji akaanza kuzungumza “Tumesikia utetezi upande wa Mshitakiwa na Jamhuri, hivyo naghairisha kesi hii namba 2-1, mpaka April 30, ambapo itasomwa upya na Mshitakiwa anaruhusiwa kuja na jopo jipya la Mawakili”
Nawageukia Wanangu na kuwaambia waje na Lineup na clip za mechi hii, wamwambie Kaka @_babaparoko aje na sweta, aje na Wakili msomi @simon.esq na kibopa @caamil_88 na Kocha Nabi maana wao ndio wamenitia matatizoni[emoji3]